Zaburi 35
Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui
Zaburi ya Daudi.
135:1 1Sam 24:15; Kut 14:14Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,
upigane na hao wanaopigana nami.
235:2 Za 3:3, 7; Ay 17:3; Mwa 50:24; 35:3; Hes 25:7; Za 27:1; Yos 8:18Chukua ngao na kigao.
Inuka unisaidie.
3Inua mkuki wako na fumo35:3 Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi. lako
dhidi ya hao wanaonifuatia.
Iambie nafsi yangu,
“Mimi ni wokovu wako.”
435:4 Za 38:12; 40:14; 69:6, 19; 70:2; 83:17; 25:3; 129:5; Yer 4:30; Mal 2:9; Isa 45:16Wafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu.
Wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.
535:5 Ay 13:25; Za 1:4; 34:7Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
malaika wa Bwana akiwafukuza.
6Njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika wa Bwana akiwafuatilia.
735:7 Ay 18:8; 9:31; Za 7:4; 7:15; 55:23Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
na bila sababu wamenichimbia shimo,
835:8 Isa 47:11; 1The 5:3; Za 7:15; Mit 5:22maafa na yawapate ghafula:
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao.
935:9 Za 2:11; 9:14; 13:5; 27:1; Lk 1:47; 1Sam 2:1; Isa 61:10; Ebr 3:18Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana
na kuufurahia wokovu wake.
1035:10 Kut 9:14; Za 12:5; 71:19; 18:17, 31; 113:5; 37:14; 86:1; 74:21; 109:16; 140:12; Isa 41:17Nitapaza sauti yangu nikisema,
“Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana?
Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao,
maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!”
1135:11 Kut 23:1; Mt 26:60Mashahidi wakatili wanainuka,
wananiuliza mambo nisiyoyajua.
1235:12 Yer 18:20; Za 38:20; 109:5; Mit 17:13Wananilipa baya kwa jema
na kuiacha nafsi yangu ukiwa.
1335:13 2Sam 3:31; 1Fal 20:31; Za 30:11; 69:10, 11; 109:24; Ay 30:25Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia
na nikajinyenyekesha kwa kufunga.
Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,
1435:14 Za 38:6; 42:9; 43:2niliendelea kuomboleza
kama vile wao ni rafiki au ndugu.
Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni
kama ninayemwombolezea mama yangu.
1535:15 Ay 31:29; 16:10Lakini nilipojikwaa,
walikusanyika kwa shangwe;
washambuliaji walijikusanya dhidi yangu
bila mimi kujua.
Walinisingizia pasipo kukoma.
1635:16 Za 22:7; Mk 10:34; 9:18; Ay 16:9; Mdo 7:54Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki,
wamenisagia meno.
1735:17 Za 6:3; 22:20, 21; 57:4; 58:6Ee Bwana, utatazama mpaka lini?
Niokoe maisha yangu na maangamizi yao,
uhai wangu wa thamani
kutokana na simba hawa.
1835:18 Za 22:20, 25; 42:4; 109:30Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
nitakusifu katikati ya watu wengi.
1935:19 Za 9:13; 38:19; 69:4; Yn 15:25; Mit 6:13; 10:10Usiwaache wale wanaonisimanga,
wale ambao ni adui zangu bila sababu;
usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu
wakonyeze jicho kwa hila.
2035:20 Za 38:12; 55:21; Yer 9:8; Mik 6:12Hawazungumzi kwa amani,
bali wanatunga mashtaka ya uongo
dhidi ya wale wanaoishi
kwa utulivu katika nchi.
2135:21 Ay 16:10; Eze 25:3; Za 40:15; 70:3Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha!
Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.”
2235:22 Kut 3:7; Za 10:1, 14Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya.
Usiwe mbali nami, Ee Bwana.
2335:23 Za 7:6; 80:2; 17:13; 1Sam 24:15Amka, inuka unitetee!
Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu.
2435:24 Za 22:17; 7:8; 26:11; 2The 1:6Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu,
sawasawa na haki yako;
usiwaache wakusimange.
2535:25 Mit 1:12; Za 35:21; 124:3; Mao 2:16Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!”
Au waseme, “Tumemmeza.”
2635:26 Za 22:17; 4:1; 109:29; 38:16; Ay 8:22; 19:5; Mik 7:10Wote wanaofurahia dhiki yangu
waaibishwe na wachanganyikiwe;
hao wanaojiinua dhidi yangu
wavikwe aibu na dharau.
2735:27 Za 9:4; 20:5; 33:3; 147:11; 149:4; Ay 17:3Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki
wapige kelele za shangwe na furaha;
hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe,
ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”
2835:28 Za 5:8; 51:14; 71:15, 24; 72:15Ulimi wangu utanena haki yako
na sifa zako mchana kutwa.
第 35 篇
求上帝申冤
大卫的诗。
1耶和华啊,
求你与我的敌人为敌,
攻击那些攻击我的人。
2求你拿起大小盾牌来帮助我,
3举起矛枪攻击追赶我的人。
求你对我说:
“我是你的拯救。”
4愿谋杀我的人蒙羞受辱,
谋害我的人落荒而逃!
5愿耶和华的天使驱散他们,
如风吹散糠秕!
6愿他们的道路漆黑泥泞,
有耶和华的天使在后追赶!
7因为他们无故设网罗,
挖陷阱要害我。
8愿他们突遭祸患,
作茧自缚,自食恶果!
9我要因耶和华而欢欣,
因祂的拯救而快乐。
10我从心底发出赞叹:
耶和华啊,谁能像你?
你拯救弱者免受欺压,
拯救穷人免遭掠夺。
11恶人诬告我,
盘问我毫无所知的事情。
12他们对我以恶报善,
令我伤心欲绝。
13他们生病时,
我披上麻衣,
谦卑地为他们禁食祷告,
但上帝没有垂听。
14我为他们哀伤,
视他们为朋友、弟兄;
我低头为他们哭泣,
如同哀悼自己的母亲。
15我遭遇患难时,
他们却聚在一起幸灾乐祸,
合伙诽谤我。
素不相识的人也群起攻击我,
不住地毁谤我。
16他们肆无忌惮地嘲弄我,
咬牙切齿地憎恶我。
17耶和华啊,
你袖手旁观要到何时?
求你救我的性命免遭残害,
救我脱离这些狮子。
18我要在大会中称谢你,
在众人面前赞美你。
19求你不要让无故攻击我的人幸灾乐祸,
不要让无故恨我的人沾沾自喜。
20他们言语暴戾,
谋害安分守己的人。
21他们高喊:“哈哈!哈哈!
我们亲眼看见了。”
22耶和华啊,这一切你都看见了,
求你不要再缄默,不要远离我。
23我的上帝,我的主啊,
求你起来为我辩护,为我申冤。
24我的上帝耶和华啊,
求你按你的公义宣告我无罪,
别让他们幸灾乐祸。
25别让他们说:
“哈哈,我们如愿以偿了!”
别让他们说:
“我们除掉他了!”
26愿幸灾乐祸的人蒙羞受辱,
自高自大的人无地自容!
27愿盼望我冤屈得雪的人扬声欢呼!
愿他们常说:“耶和华当受尊崇!
祂乐意赐福给自己的仆人。”
28我要诉说你的公义,
终日赞美你。