Zaburi 133
Sifa Za Pendo La Undugu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1133:1 Mwa 13:8; Yn 17:11; 1Kor 1:10; Rum 12:10Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
2133:2 Kut 29:7; 30:25Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.
3133:3 Ay 29:19; Mit 19:12; Isa 18:4; 26:19; 45:8; Hos 14:5; Mik 5:7; Kum 3:8; Kut 15:17; Law 25:21; Za 2:6; 74:2; 21:4; Dan 12:2-3; Yn 4:14; Ebr 7:25; 1Yn 5:20Ni kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.