Zaburi 132
Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni
Wimbo wa kwenda juu.
1Ee Bwana, mkumbuke Daudi
na taabu zote alizozistahimili.
2132:2 Mwa 49:24; Isa 49:26; 60:16Aliapa kiapo kwa Bwana
na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3132:3 2Sam 7:2, 27“Sitaingia nyumbani mwangu
au kwenda kitandani mwangu:
4132:4 Rut 3:18sitaruhusu usingizi katika macho yangu,
wala kope zangu kusinzia,
5132:5 1Fal 8:17; Mdo 7:46mpaka nitakapompatia Bwana mahali,
makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
6132:6 1Sam 7:2; 17:12; Yos 9:17; 18:1; 1Nya 13:5Tulisikia habari hii huko Efrathi,
tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:132:6 Yaani Kiriath-Yearimu.
7132:7 2Sam 15:25; Za 5:7; 122:1; 1Nya 28:2“Twendeni kwenye makao yake,
na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
8132:8 Hes 10:35inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,
wewe na Sanduku la nguvu zako.
9132:9 Ay 27:6; Zek 3:4; Isa 61:3, 10; Mal 3:3; Ay 29:14Makuhani wako na wavikwe haki,
watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”
10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,
usimkatae mpakwa mafuta wako.
11132:11 Za 89:3-4, 35; 1Nya 17:11-14; Mt 1:1; Lk 3:31Bwana alimwapia Daudi kiapo,
kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:
“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe
katika kiti chako cha enzi,
12132:12 2Nya 6:16; Za 25:10; Lk 1:32; Mdo 2:30kama wanao watashika Agano langu
na sheria ninazowafundisha,
ndipo wana wao watarithi
kiti chako cha enzi milele na milele.”
13132:13 Kut 15:17; Za 48:1, 2; 68:16; 1Fal 18:13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni,
amepaonea shauku pawe maskani yake:
14132:14 Za 80:1; 68:16; 2Sam 6:2“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;
hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:
15132:15 Za 107:9; 147:14Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele:
nitashibisha maskini wake kwa chakula.
16132:16 2Nya 6:41; Ay 8:21; Za 149:5Nitawavika makuhani wake wokovu,
nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.
17132:17 1Sam 2:10; Za 18:28; 84:9; 92:10; Eze 29:21; Lk 1:69; 1Fal 11:36; 2Fal 8:19; 2Nya 21:7“Hapa nitamchipushia Daudi pembe,132:17 Pembe inawakilisha nguvu.
na kuweka taa kwa ajili ya masiya132:17 Masiya yaani mpakwa mafuta. wangu.
18132:18 Ay 8:22; 2Sam 12:30Adui zake nitawavika aibu,
bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”
Песнь 132
Песнь восхождения, Довуда.
1Как хорошо и как приятно
жить братьям вместе!
2Это – как возлитое на голову драгоценное масло,
стекающее на бороду главного священнослужителя Хоруна,
стекающее на края его одежды132:2 См. Исх. 29:7; 30:22-33.;
3как если бы роса горы Хермон132:3 Хермон – гора на северной границе Исроила, известная тем, что на её склонах выпадает чрезвычайно обильная роса.
сошла на горы Сионские.
Там Вечный обещал дать Своё благословение –
вечную жизнь.