Zaburi 120
Kuomba Msaada
Wimbo wa kwenda juu.
1120:1 2Sam 22:7; Za 18:1; 118:5Katika dhiki yangu namwita Bwana,
naye hunijibu.
2120:2 Za 31:18; 52:4Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
3Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4120:4 Kum 32:23Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5120:5 Mwa 25:13; 2:10; Yer 2:10; 49:28; 1Sam 25:1Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.