Yeremia 50 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 50:1-46

Ujumbe Kuhusu Babeli

150:1 Isa 13:1; Za 137:8; Mwa 10:10Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:

250:2 Kum 30:4; Yer 4:16; 51:31, 47; Isa 21:9; Za 20:5; Isa 13:2; Yer 46:6; Law 26:30“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa,

twekeni bendera na mkahubiri;

msiache kitu chochote, bali semeni,

‘Babeli utatekwa;

Beli ataaibishwa,

Merodaki atajazwa na hofu kuu.

Sanamu zake zitaaibishwa

na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’

350:3 Isa 14:22-23; Yer 9:11; Sef 1:3; Isa 13:17; 41:25; Yer 25:26Taifa kutoka kaskazini litamshambulia,

na kuifanya nchi yake ukiwa.

Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake,

watu na wanyama wataikimbia.

450:4 Eze 37:22; Ezr 3:12; Yer 31:9; Isa 9:13; Hos 3:5; Yer 3:18“Katika siku hizo, wakati huo,”

asema Bwana,

“watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda

wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.

550:5 1Sam 29:1; Yer 33:7; Kum 29:14; Ebr 8:6-10; Isa 11:16; Yer 31:21; 32:40Wataiuliza njia iendayo Sayuni

na kuelekeza nyuso zao huko.

Watakuja na kuambatana na Bwana

katika agano la milele

ambalo halitasahaulika.

650:6 Isa 53:6; Mt 10:6; Yer 3:6; Eze 34:6; Za 119:176; Mt 9:36; Yer 10:21; Za 95:10“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea;

wachungaji wao wamewapotosha

na kuwasababisha kuzurura

juu ya milima.

Walitangatanga juu ya mlima na kilima,

na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.

750:7 Yer 2:3; 14:8; Za 22:4; Yer 5:17; 10:25; Eze 35:12Yeyote aliyewakuta aliwala;

adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia,

kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi,

Bwana, aliye tumaini la baba zao.’

850:8 Isa 48:20; Ufu 18:4; Yer 51:6“Kimbieni kutoka Babeli;

ondokeni katika nchi ya Wakaldayo

tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.

950:9 Isa 13:17; Yer 25:14; Isa 41:25; Yer 25:26Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli

muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.

Watashika nafasi zao dhidi yake,

naye kutokea kaskazini atatekwa.

Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,

ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.

10Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara;

wote wamtekao nyara watapata za kutosha,”

asema Bwana.

1150:11 Isa 47:6; Yer 31:18“Kwa sababu hushangilia na kufurahi,

wewe utekaye urithi wangu,

kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka,

na kulia kama farasi dume,

1250:12 Yer 51:47; 25:12; 51:26mama yako ataaibika mno,

yeye aliyekuzaa atatahayari.

Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote,

atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.

1350:13 Eze 27:36; Hab 2:6; Kum 29:22; Yer 49:17; 9:11; 48:9; 51:62; 18:16Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu,

lakini ataachwa ukiwa kabisa.

Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki

kwa sababu ya majeraha yake yote.

14“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli,

enyi nyote mvutao upinde.

Mpigeni! Msibakize mshale wowote,

kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.

1550:15 Yer 51:14; 2Nya 30:8; Yer 51:44-58; 2Fal 25:4; Yer 51:6; Ufu 18:6; Isa 10:3; Hab 2:7-8Piga kelele dhidi yake kila upande!

Anajisalimisha, minara yake inaanguka,

kuta zake zimebomoka.

Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana,

mlipizeni kisasi;

mtendeeni kama alivyowatendea wengine.

1650:16 Yer 25:38; Isa 13:14; Yer 51:9Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli,

pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna.

Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu

kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe,

kila mmoja na akimbilie

kwenye nchi yake mwenyewe.

1750:17 2Fal 24:1; Yer 2:15; Kum 4:27; 2Fal 17:6; 24:10-17; 1Pet 2:25; Yer 2:15; Hes 24:8“Israeli ni kundi lililotawanyika

ambalo simba wamelifukuzia mbali.

Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru,

wa mwisho kuponda mifupa yake

alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”

1850:18 Isa 10:12; Eze 31:3; Sef 2:13Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

“Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake

kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.

1950:19 Yer 31:10; Eze 34:13; Yer 33:12; Isa 65:10; Mik 7:14; Zek 10:10Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe

naye atalisha huko Karmeli na Bashani;

njaa yake itashibishwa

juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.

2050:20 Za 103:12; Zek 3:4-9; Isa 33:24; Yer 31:34; Rum 9:27; Isa 10:20-22; Eze 36:16Katika siku hizo, wakati huo,”

asema Bwana,

“uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli,

lakini halitakuwepo,

kwa ajili ya dhambi za Yuda,

lakini haitapatikana hata moja,

kwa kuwa nitawasamehe

mabaki nitakaowaacha.

2150:21 Eze 23:23; Isa 10:6“Shambulieni nchi ya Merathaimu

na wale waishio huko Pekodi.

Wafuatieni, waueni

na kuwaangamiza kabisa,”

asema Bwana.

“Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

2250:22 Yer 4:19-21; 51:54Kelele ya vita iko ndani ya nchi,

kelele ya maangamizi makuu!

2350:23 Isa 14:16; Yer 51:20; Isa 10:5Tazama jinsi nyundo ya dunia yote

ilivyovunjika na kuharibika!

Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa

miongoni mwa mataifa!

2450:24 Yer 51:12; Dan 5:30-31; Yer 51:31; Ay 9:4Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli,

nawe ukakamatwa kabla haujafahamu;

ulipatikana na ukakamatwa

kwa sababu ulimpinga Bwana.

2550:25 Isa 13:5Bwana amefungua ghala lake la silaha

na kuzitoa silaha za ghadhabu yake,

kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote

anayo kazi ya kufanya

katika nchi ya Wakaldayo.

2650:26 Isa 14:22-23; Yer 51:11; Rut 3:7Njooni dhidi yake kutoka mbali.

Zifungueni ghala zake za nafaka;

mlundikeni kama lundo la nafaka.

Mwangamizeni kabisa

na msimwachie mabaki yoyote.

2750:27 Za 68:30; Yer 48:15; Ay 18:20; Yer 25:34Waueni mafahali wake wachanga wote;

waacheni washuke machinjoni!

Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia,

wakati wao wa kuadhibiwa.

2850:28 Isa 48:20; Yer 51:10; 2Fal 24:13; Yer 52:13Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli

wakitangaza katika Sayuni

jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi,

kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.

2950:29 Ay 21:19; Ufu 18:6; Oba 1:15; Dan 5:23; Isa 14:13-14; Mao 3:24; Isa 13:18; Kum 32:41“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli,

wote wale wavutao upinde.

Pigeni kambi kumzunguka kabisa,

asitoroke mtu yeyote.

Mlipizeni kwa matendo yake;

mtendeeni kama alivyotenda.

Kwa kuwa alimdharau Bwana,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

3050:30 Isa 13:18; Yer 49:26; 51:4Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;

askari wake wote watanyamazishwa siku ile,”

asema Bwana.

3150:31 Yer 21:13; Ufu 18:7-8“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

“kwa kuwa siku yako imewadia,

yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.

3250:32 Yer 21:14; 49:27; Amo 5:2; Za 20:8; 119:21Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka,

wala hakuna yeyote atakayemuinua;

nitawasha moto katika miji yake,

utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”

3350:33 Isa 58:6; 14:17Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Watu wa Israeli wameonewa,

nao watu wa Yuda pia.

Wote waliowateka wamewashikilia sana,

wanakataa kuwaachia waende.

3450:34 Yer 31:35; 51:19; Za 119:154; Mao 3:58; Kut 6:6; Ay 19:25; Isa 49:25Lakini Mkombozi wao ana nguvu;

Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Atatetea kwa nguvu shauri lao

ili alete raha katika nchi yao,

lakini ataleta msukosuko

kwa wale waishio Babeli.

3550:35 Yer 47:6; Dan 5:7; Isa 37:13; 45:1“Upanga dhidi ya Wakaldayo!”

asema Bwana,

“dhidi ya wale waishio Babeli

na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!

36Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo!

Watakuwa wapumbavu.

Upanga dhidi ya mashujaa wake!

Watajazwa na hofu kuu

3750:37 Yer 25:20; 2Fal 19:23; Isa 19:16; Yer 51:21; Nah 3:13; Isa 45:3Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita

pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake!

Wao watakuwa kama wanawake.

Upanga dhidi ya hazina zake!

Hizo zitatekwa nyara.

3850:38 Isa 11:15; Yer 51:36; Ufu 16:12Ukame juu ya maji yake!

Nayo yatakauka.

Kwa kuwa ni nchi ya sanamu,

wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.

3950:39 Isa 34:13-15; Ufu 18:2; Isa 13:19-22; Za 74:14; Yer 51:37“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo,

nao bundi watakaa humo.

Kamwe haitakaliwa tena

wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

4050:40 Mwa 19:24; Mt 10:15; 2Pet 2:6; Yer 51:62Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora

pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”

asema Bwana,

“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote

atakayeishi humo.

Naam, hakuna mtu yeyote

atakayekaa humo.

4150:41 Isa 41:25; Yer 6:22; Isa 13:14; Yer 51:22-28; Ufu 17:16; Isa 23:17“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini;

taifa kubwa na wafalme wengi

wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.

4250:42 Isa 13:18; 5:30; 47:1; Yer 6:23; Ay 30:21Wamejifunga pinde na mikuki;

ni wakatili na wasio na huruma.

Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma

wanapoendesha farasi zao;

wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita

ili kukushambulia, ee Binti Babeli.

4350:43 Yer 47:3; 6:22-24Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu,

nayo mikono yake imelegea.

Uchungu umemshika,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

4450:44 Hes 16:5; Ay 41:10; Isa 46:9; Yer 12:5; 49:19Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani

kuja kwenye nchi ya malisho mengi,

ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula.

Ni nani aliye mteule,

nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?

Ni nani aliye kama mimi,

na ni nani awezaye kunipinga?

Tena ni mchungaji yupi

awezaye kusimama kinyume nami?”

4550:45 Isa 24:14; Mdo 4:28; Isa 48:14; Yer 51:11Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli,

kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo:

Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali.

Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.

4650:46 Ay 24:12; Ufu 18:9-10; Amu 5:4; Yer 49:21Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka;

kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.

Japanese Contemporary Bible

エレミヤ書 50:1-46

50

バビロンについてのメッセージ

1次は、主が預言者エレミヤを通して、カルデヤ人の国バビロンについて語ったことばです。

2「全世界の人に、バビロンは滅びると告げなさい。

その国の神であるメロダクは恥をかく。

3北から一つの国が攻め上り、この地を二度と人が住めないほど徹底的に荒らすからだ。人も家畜も逃げる。 4その時、イスラエルとユダの民は泣きながら、彼らの神であるわたしを尋ね求める。 5シオン(エルサレム)に通じる道を尋ね、故国をめざして帰る。『二度と破られない永遠の誓いを立て、主にしっかり結びつこう』と、彼らは言う。 6わたしの民は迷った羊だ。羊飼いたちはとんでもない方向に彼らを連れて行き、山の中に置き去りにした。彼らは道に迷い、どうすれば元の場所へ帰れるかと途方にくれた。 7彼らを見つけた者は彼らをさんざん食い物にし、『彼らを好きなように料理しよう。彼らは、正義の神であり、彼らの先祖の望みであった主に罪を犯したのだから』と言った。

8しかし今度は、

カルデヤ人の国バビロンから逃げ出すのだ。

わたしの民を故国に連れ帰りなさい。

9わたしは北方の強い国々の軍隊を奮い立たせ、

バビロンに敵対させるからだ。

バビロンは滅びる。

敵の矢は的をめがけて飛んで来て、一本もはずれない。

10バビロンは丸裸になる。

11わたしの民から身ぐるみはぎ取ったカルデヤ人よ。

おまえたちは喜び、

みずみずしい草の茂る放牧地の牛のように肥え太り、

種馬のようにいなないても、

12おまえたちの母は恥をかいて顔を伏せる。

おまえたちは一番弱い国となり、

荒野となり、乾ききった砂漠となるからだ。

13わたしの怒りによって、

バビロンはさびれた荒れ地となる。

そこを通り過ぎる者は血の気を失い、

そのすべての傷を見てあざける。

14周りを囲むすべての国々よ、

バビロンと戦う準備をしなさい。

弓を引く者は、バビロンをめがけて矢を放て。

彼は神に逆らって罪を犯したのだから、矢を惜しまず、

容赦なく射かけるのだ。

15四方から、いっせいにときの声を上げなさい。

城壁はくずれ、バビロンは降伏する。

わたしはとうとう復讐した。

バビロンがしたとおりのことを、やり返しなさい。

16畑で働く外国人は、みな逃げなさい。

敵の軍勢が攻めて来るから、

自分の国に走って帰りなさい。

17イスラエル人はライオンに追われる羊のようだ。初めはアッシリヤの王がその肉を食い、次にはバビロンのネブカデネザル王が、骨まで食いつくした。」 18そこで、イスラエルの神である天の軍勢の主は、こう言います。「わたしは今度は、アッシリヤを罰したように、バビロンの王とその国に罰を加える。 19わたしはイスラエル人を故国に連れ戻す。彼らはカルメルとバシャンで草を食べ、もう一度、エフライムとギルアデの山々で幸せに暮らすようになる。 20その日には、イスラエルにもユダにも、罪は一つも見当たらなくなる。わたしは残った者たちを赦すからだ。

21わたしの勇士たちよ。

メラタイム(南部バビロニヤ)と

ペコデ(東部バビロニヤ)に攻め上りなさい。

わたしがさばこうとしている反逆の国バビロンに、

威勢よく進撃しなさい。

命令しておいたとおり、彼らを根絶やしするのだ。

22国中に戦いの雄たけび、

大きな破滅の叫びが上がるように。

23地上のすべての国々を打った強力な金槌は、

粉々になった。

バビロンは国々の中で、荒れ果てた地となった。

24バビロンよ。

わたしがおまえに罠をしかけ、おまえを捕まえた。

おまえがわたしに戦いをいどんだからだ。

25わたしは兵器庫を開き、

敵に怒りを表そうと武器を取り出した。

バビロンに降りかかった恐怖は、

天の軍勢の主であるわたしが指図したものだ。

26遠くから来てバビロンに攻めかかりなさい。

穀物倉に押し入り、城壁と家々を壊して高く積み上げ、

とことん荒らすのだ。

めぼしいものは何一つ残してはならない。

27家畜にまで、のろいが下るように。

それを一頭残らず殺すのだ。

バビロンの荒廃の時がきたのだから。

28だが、わたしの民は逃げ出す。

彼らは故国に逃れ、

彼らの神であるわたしが怒りに燃え、

神殿を壊した者たちに仕返ししたと報告する。

29弓を引く者をバビロンに呼び集めなさい。

この都を包囲し、

蟻一匹はい出るすきもないようにするのだ。

バビロンがほかの国々にしたとおりに報いなさい。

彼らはイスラエルのきよい神であるわたしに

大言壮語し、公然と反抗したからだ。

30若者は路上に倒れて死に、勇士は皆殺しになる。

31思い上がっている者たちよ。

わたしはおまえたちの敵になる。

おまえたちのさばきの日が、ついにきたのだ。

32高ぶる国よ。

おまえはつまずいて倒れるが、だれも起こしてくれない。

わたしが町々に火をつけ、何もかも灰にするからだ。」

33天の軍勢の主はこう言います。「捕虜になったイスラエルとユダの民は虐待されている。主人たちは彼らを釈放しようとしない。 34だが、彼らを救い出す者は強く、その名は天の軍勢の主だ。わたしは彼らの訴えを聞き、彼らが自由の身となり、再びイスラエルの地で平穏に暮らせるように取り計らう。だが、バビロンの住民に安息はない。

35破滅の剣がカルデヤ人に切りかかる。

その剣はバビロンの住民を、

重立った者も知恵のある者も区別なしに切りまくる。

36賢い助言者も愚かになり、

何ものをも恐れない勇士もあわてふためく。

37戦いが起こって、馬も戦車ものみ尽くす。

同盟を結んだほかの国々の者たちは、

女のように弱くなり、財宝はみな略奪される。

38そればかりか、水の補給さえなくなる。

どうして、このようになるのだろうか。

国中に神々の像が立ち、

民が熱心に偶像を慕っているからだ。

39バビロンの都は、だちょうや山犬、荒野の野獣の住みかとなり、人は二度と住みつかない。永久に荒れ果てた地となる。 40わたしは、ソドムとゴモラとその近くの町々を滅ぼしたように、バビロンを滅ぼす。これらの町々に人が住まなくなったように、バビロンにも人が寄りつかなくなる。」

41北から大軍が押し寄せて来ます。神が多くの国から呼び集めた王たちが、この軍隊を指揮しています。 42彼らは完全武装していて、残忍で容赦しません。その雄たけびは、海辺に打ち寄せる波のように響き渡ります。バビロンよ。彼らは戦いのしたくを整え、馬に乗って攻めかかります。 43バビロンの王は、敵が来たという報告を受けると、肩を落としました。産みの苦しみをしている女のように、恐怖の苦痛に取りつかれたからです。 44「ヨルダンの密林から出て、草を食べている羊に飛びかかるライオンのような侵略者が、彼らに突然襲いかかるようにする。彼らを守る者たちを追い払い、わたしの気に入った指導者を立てる。わたしのような者がいるだろうか。わたしの決めたことに反抗する支配者が、どこにいるだろうか。だれがわたしを呼びつけて、説明を求めることができようか。 45カルデヤ人の国バビロンへの、わたしの計画を聞きなさい。

小さな子どもたちでさえ、奴隷になって引かれて行く。

身の毛もよだつほど恐ろしいことではないか。

46バビロンの倒れる地響きで、全地は揺れ動く。

その断末魔の叫びは、世界の隅々に届く。」