Wimbo 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wimbo 7:1-13

17:1 Za 45:13Ee binti wa mwana wa mfalme,

tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu!

Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani,

kazi ya mikono ya fundi stadi.

2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo

ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa.

Kiuno chako ni kichuguu cha ngano

kilichozungukwa kwa yungiyungi.

37:3 Wim 4:5Matiti yako ni kama wana-paa wawili,

mapacha wa paa.

47:4 Hes 21:26; Wim 4:4; 5:15; Za 144:12Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu.

Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni

karibu na lango la Beth-Rabi.

Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni

ukitazama kuelekea Dameski.

57:5 Isa 35:2Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli.

Nywele zako ni kama zulia la urujuani;

mfalme ametekwa na mashungi yake.

67:6 Wim 1:15; 4:10Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza,

ee pendo, kwa uzuri wako!

77:7 Wim 4:5Umbo lako ni kama la mtende,

nayo matiti yako kama vishada vya matunda.

87:8 Wim 2:5Nilisema, “Nitakwea mtende,

nami nitayashika matunda yake.”

Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu,

harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,

97:9 Wim 5:16na kinywa chako kama divai

bora kuliko zote.

Mpendwa

Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu,

ikitiririka polepole juu ya midomo na meno.

107:10 Wim 2:16; 6:3; Za 45:11; Gal 2:20Mimi ni mali ya mpenzi wangu,

nayo shauku yake ni juu yangu.

11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani,

twende tukalale huko vijijini.

127:12 Za 63:3-8; Wim 6:11; 4:13; 2:13-15Hebu na twende mapema

katika mashamba ya mizabibu

tuone kama mizabibu imechipua,

kama maua yake yamefunguka,

na kama mikomamanga imetoa maua:

huko nitakupa penzi langu.

137:13 Gal 5:227:13 Mwa 30:14; Wim 4:16Mitunguja hutoa harufu zake nzuri,

kwenye milango yetu kuna matunda mazuri,

mapya na ya zamani,

ambayo nimekuhifadhia wewe,

mpenzi wangu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

雅歌 7:1-13

1我的公主啊,你的双脚配上鞋子多么美啊!

你美玉般圆润的腿是巧匠的杰作。

2你的肚脐好像圆杯,

不缺调和的酒。

你的腰好比一堆麦子,

四周围绕着百合花。

3你的胸脯好像一对孪生的小鹿。

4你的脖子如象牙塔,

眼睛好像希实本境内巴特·拉并门旁的水池。

你的鼻子好像眺望大马士革黎巴嫩塔。

5你的头如同迦密山,

你的秀发好像紫黑色的缎子,

君王的心被你的缕缕青丝系住。

6我的爱人,你是多么美丽,

多么讨人喜爱,令人陶醉啊!

7你亭亭玉立如同棕榈树,

胸脯就像树上的果串。

8我要攀上这棵树,

握住树上的果子。

愿你的胸脯像葡萄串,

你的气息如苹果般清香。

9你的亲吻像上好的美酒。

女子:

愿美酒流入我良人的口中,

缓缓注入他陶醉的唇齿间。

10我属于我的良人,

是他所恋慕的。

11我的良人,来吧!

让我们到田间去,

在村庄里住宿吧。

12我们清晨去葡萄园,

看看葡萄树是否已经发芽开花,

石榴树是否正在开花。

我要在那里把我的爱情献给你。

13那里风茄飘香,

门口有各样上好的新陈美果。

我的良人,这都是我为你存留的。