Walawi 17 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 17:1-16

Kunywa Damu Kumekatazwa

1Bwana akamwambia Mose, 217:2 Law 10:6, 12“Sema na Aroni na wanawe, pamoja na Waisraeli wote, uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana aliloagiza: 317:3 Law 3:7; 7:23Mwisraeli yeyote atakayetoa dhabihu ya maksai, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake, 417:4 1Fal 8:4; 2Nya 1:3; Kum 12:5-21; Mwa 17:14badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Bwana mbele ya Maskani ya Bwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 517:5 Law 3:1; Eze 43:27; Mwa 21:33; 22:2; 1Fal 14:22-23Hii ni ili Waisraeli wamletee Bwana dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Bwana, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kama sadaka za amani. 6Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Bwana katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 717:7 Kut 12:14; 22:20; 34:15; 34:15; Yer 3:6-9; Eze 23:3; 1Kor 10:20; Mwa 9:12; Kum 32:17; 2Nya 11:15; Za 106:37Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’

8“Waambie: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu 917:9 Law 1:3; 3:7bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa Bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

1017:10 Mwa 9:4; Kum 12:16, 23; 1Sam 14:33; Law 26:17; Yer 44:11; Eze 15:7“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakunywa damu yoyote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake. 1117:11 Mwa 9:4; Ebr 9:22Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu. 12Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kunywa damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kunywa damu.”

1317:13 Law 7:26; Eze 24:7; 33:25; Mdo 15:20; Kum 12:16“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo, 1417:14 Mwa 9:4; Law 7:24; 14:8; 11:40; Kol 1:14; Kum 14:21; Kut 22:31; Mk 14:24; Rum 5:9kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; yeyote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”

1517:15 Kut 22:31; Kum 14:2; Eze 4:14“ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi. 1617:16 Law 5:1; Hes 19:20; Ebr 9:28Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 17:1-16

殺祭牲的條例

1耶和華對摩西說: 2「你把以下條例告訴亞倫父子們及全體以色列人。

3「任何在營內或營外宰殺公牛、綿羊或山羊的以色列人, 4若沒有把牲畜帶到會幕門口,在耶和華的聖幕前獻給耶和華,便是犯了流血之罪,要將他從民中剷除。 5這是為促使以色列人把祭牲帶到會幕門口交給祭司,獻給耶和華作平安祭,而非在野外殺祭牲獻祭。 6祭司要將祭牲的血灑在會幕門口耶和華的祭壇上,把脂肪焚燒獻給耶和華作馨香之祭。 7他們不可再獻祭物給山羊神,與其苟合。這是一條永遠不變的律例,他們世世代代都要遵守。 8不論是以色列人,還是寄居在以色列人中間的外族人,獻燔祭或其他祭物時, 9如果有人沒把祭物帶到會幕門口獻給耶和華,要將他從民中剷除。

禁止吃血

10「任何以色列人或寄居在以色列人中間的外族人若吃血,耶和華必嚴懲,把他從民中剷除。 11因為生命在血中,耶和華把血賜給你們,使你們可以用血在祭壇上為自己贖罪。血可以為人的生命贖罪。 12所以耶和華吩咐以色列人和寄居在以色列人中間的外族人不可吃血。 13以色列人或寄居在以色列人中間的外族人如果捕到可吃的鳥或獸,必須放盡牠的血,用土掩埋, 14因為眾生的生命都在血中。因此,耶和華吩咐以色列人不可吃任何動物的血,因為血就是生命。凡吃血的都要被剷除。 15不論以色列人還是外族人,若吃了自然死亡或被野獸撕裂的動物,就不潔淨。他必須洗衣、沐浴,等到傍晚才能潔淨, 16否則他要承擔罪責。」