Walawi 16 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 16:1-34

Siku Ya Upatanisho

116:1 Law 10:1; 16:2; Kut 26:33-34; 25:22; 30:10; 40:34; Ebr 9:7, 25; 10:19; 6:19; 2Sam 22:10Bwana akasema na Mose baada ya kifo cha wale wana wawili wa Aroni waliokufa walipokaribia mbele za Bwana. 2Bwana akamwambia Mose: “Mwambie ndugu yako Aroni asije wakati wowote atakavyo yeye ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, nyuma ya pazia pale mbele ya kiti cha rehema kile kilichoko juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema.

316:3 Law 4:1-12; Ebr 9:24-25“Hivi ndivyo Aroni atakavyoingia katika mahali patakatifu: atachukua fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 416:4 Kut 28:29, 42; 29:4, 29-30; Law 21:10; Hes 20:26-28; Ebr 10:22; Eze 9:2; 44:17-18Atavaa koti takatifu la kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani; atafunga mshipi wa kitani kiunoni, na kuvaa kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu, kwa hiyo ni lazima aoge kwa maji kabla ya kuyavaa mavazi hayo. 516:5 Law 4:3, 13-21; 2Nya 29:23; Za 50:9; Ezr 6:17; Eze 45:22Atachukua mbuzi dume wawili kutoka kwa jumuiya ya Israeli kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

616:6 Law 9:7; Ebr 7:27; 9:7-12“Aroni atamtoa huyo fahali kwa ajili ya sadaka yake ya dhambi ili afanye upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na nyumba yake. 7Kisha atawachukua wale mbuzi dume wawili na kuwaleta mbele za Bwana kwenye ingilio la Hema la Kukutania. 816:8 Hes 26:55-56; 33:54; 34:13; Yos 14:2; 18:6; Amu 20:9; Neh 10:34; Es 3:7; 9:24; Za 22:18; Mit 16:33Aroni atapiga kura kwa ajili ya hao mbuzi wawili, mmoja kwa ajili ya Bwana na mwingine kwa ajili ya kubebeshwa dhambi.16:8 Yaani Azazeli, maana yake mbuzi wa ondoleo la dhambi; pia ms. 10, 26. 9Aroni atamleta yule mbuzi ambaye kura ya Bwana imemwangukia na kumtoa dhabihu kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 1016:10 Isa 53:4-10; Rum 3:25; 1Yn 2:2Lakini mbuzi aliyechaguliwa kwa kura kuwa wa kubebeshwa dhambi atatolewa akiwa hai mbele za Bwana, atumike kwa kufanya upatanisho kwa kumwacha aende jangwani akiwa amebebeshwa dhambi.

1116:11 Ebr 9:7“Aroni atamleta yule fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake na nyumba yake, naye atamchinja huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe. 1216:12 Law 10:1; Ufu 8:5; Kut 25:6; 30:34-38Atachukua chetezo kilichojaa makaa yanayowaka kutoka madhabahuni mbele za Bwana, na konzi mbili za uvumba laini uliosagwa vizuri wenye harufu, na kuvipeleka nyuma ya pazia. 1316:13 Kut 25:17; 28:43; Law 22:9; Kut 31:7-8; Hes 16:7, 18; Ufu 8:3-4Ataweka uvumba juu ya moto mbele za Bwana, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili asife. 1416:14 Law 4:5-6; Ebr 9:7-13, 25Atachukua sehemu ya damu ya fahali, na kwa kidole chake atanyunyiza sehemu ya mbele ya kiti cha rehema; kisha atanyunyiza sehemu ya hiyo damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kiti cha rehema.

1516:15 Law 4:7, 13-21; Ebr 9:3, 7-12; 13:11; 7:27; Hes 19:19; Isa 52:15; Eze 36:25“Kisha atamchinja mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, na kuichukua damu yake nyuma ya pazia, na aifanyie kama alivyofanya kwa damu ya fahali: Atanyunyiza juu ya kiti cha rehema na mbele yake. 1616:16 Kut 26:33; 29:4, 36; 40:2; Rum 3:25; Ebr 9:25Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu kwa sababu ya unajisi na uasi wa Waisraeli, kwa dhambi zao zozote. Atafanya hivyo kwa ajili ya Hema la Kukutania, ambalo liko miongoni mwao katikati ya unajisi wao. 17Mtu yeyote haruhusiwi kuwa ndani ya Hema la Kukutania, kuanzia wakati Aroni anapoingia kufanya upatanisho katika Patakatifu pa Patakatifu, hadi atakapotoka nje, baada ya kujifanyia upatanisho yeye mwenyewe na nyumba yake, pamoja na jumuiya yote ya Israeli.

1816:18 Law 4:7, 24-25“Kisha atatoka aje kwenye madhabahu yaliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi, na kuiweka kwenye pembe za madhabahu. 1916:19 Eze 43:20; Ebr 9:12Atanyunyiza baadhi ya hiyo damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, ili kuitakasa na kuiweka wakfu kutokana na unajisi wa Waisraeli.

20“Aroni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai. 2116:21 Kut 29:10; Law 5:5Aroni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, ili kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo. 2216:22 Kut 28:38; Isa 53:12; Za 103:1-13; Mt 8:17; Yn 1:29; 1Pet 2:24Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.

2316:23 Kut 28:42; Eze 42:14; Flp 2:6-11“Kisha Aroni ataenda ndani ya Hema la Kukutania na kuvua yale mavazi ya kitani aliyoyavaa kabla ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu, naye atayaacha pale. 2416:24 Law 6:16; 1:3; 16:25; Kut 29:13; Law 4:10Ataoga kwa maji katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake ya kawaida. Kisha atatoka na kutoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yake na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya watu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, na kwa ajili ya watu. 25Pia atachoma mafuta ya mnyama wa sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.

2616:26 Law 11:25; 14:8; Ebr 9:10“Yule mtu anayemwachia yule mbuzi wa kubebeshwa dhambi ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji; baadaye anaweza kuingia kambini. 2716:27 Kut 29:14; Ebr 13:11; Law 8:17; 4:12Yule fahali na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi. Ngozi zao, nyama, na matumbo pamoja na mavi vitateketezwa kwa moto. 2816:28 Hes 19:8-10Mtu atakayevichoma ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; baadaye ataweza kuingia kambini.

2916:29 Kut 12:14, 19; 31:15; Law 25:9; 23:27, 28, 32; Hes 29:7; Isa 58:3“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge, wala msifanye kazi yoyote, iwe mzawa au mgeni anayeishi miongoni mwenu, 3016:30 Kut 30:10; Za 51:2; Yer 33:8; Eze 36:33; Zek 13:1; Efe 5:26kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha mtakuwa safi mbele za Bwana kutokana na dhambi zenu zote. 3116:31 Ezr 8:21; Isa 58:3-5; Dan 10:12; Mdo 27:9Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu. 3216:32 Kut 30:30; 28:2; Hes 20:26Kuhani ambaye ametiwa mafuta na kuwekwa wakfu ili kuingia mahali pa baba yake kama kuhani mkuu atafanya upatanisho. Atavaa mavazi matakatifu ya kitani, 3316:33 Eze 45:18na kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, na pia kwa ajili ya makuhani, pamoja na jumuiya yote ya watu.

3416:34 Kut 27:21; Ebr 9:7, 25; Law 23:31; Hes 29:7“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Upatanisho utafanywa mara moja tu kwa mwaka kwa ajili ya dhambi zote za Waisraeli.”

Ndivyo ilivyofanyika, kama vile Bwana alivyomwamuru Mose.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

利未记 16:1-34

赎罪日的条例

1亚伦的两个儿子死在耶和华面前以后, 2耶和华对摩西说:“告诉你哥哥亚伦,他不可随意进入幔子里面的至圣所,走到约柜上的施恩座前,免得死亡,因为我要在施恩座之上的云彩中显现。 3亚伦进入圣所时,要带一只作赎罪祭的公牛犊和一只作燔祭的公绵羊。 4他要穿上圣洁的细麻内袍、细麻裤子,束上细麻腰带,戴上细麻礼冠。这些是圣洁的衣物,他必须沐浴后才可穿戴。 5他要从以色列会众那里取两只公山羊作赎罪祭、一只公绵羊作燔祭。 6亚伦要先献上那头公牛犊作赎罪祭,为自己和全家赎罪。 7然后,他要把两只公山羊带到会幕门口,放在耶和华面前, 8抽签决定哪只归耶和华、哪只归阿撒泻勒16:8 阿撒泻勒”是希伯来文的音译,意义不确定。9亚伦要献上那只归耶和华的公山羊作赎罪祭, 10要将那只归阿撒泻勒的公山羊活着献给耶和华,然后把它放到旷野归阿撒泻勒,用来赎罪。

11亚伦要把那只为他作赎罪祭的公牛犊牵来宰杀,为自己和全家赎罪, 12然后拿一个香炉,盛满从耶和华面前的祭坛上取的火炭,再拿两把磨细的香带进幔子里。 13他要在耶和华面前烧香,使香的烟笼罩约柜上的施恩座,免得他死亡。 14他要取一些牛血,用手指弹洒在施恩座的东面,也要在施恩座前用手指弹洒七次。 15然后,亚伦要出去宰杀那只为民众作赎罪祭的公山羊,把羊血带进幔子里,像洒牛血一样洒在施恩座的上面和前面。 16以色列人的污秽、叛逆和罪恶,他要这样为至圣所赎罪。他也要同样为会幕赎罪,因为会幕座落在以色列人中间,处在他们的污秽中。 17从他进入圣所为自己全家和以色列全体会众赎罪开始,直到他赎完罪出来为止,任何人都不可待在会幕里。 18之后,他要来到耶和华面前的祭坛那里,为祭坛赎罪。他要取一些牛血和羊血,抹在祭坛的四角上, 19用手指向祭坛洒血七次,除掉以色列人的污秽,使祭坛圣洁。

20“他为至圣所、会幕和祭坛赎罪后,要牵来那只活山羊, 21把双手放在羊头上,承认以色列人的过犯、叛逆和罪恶,将这一切罪归到公山羊的头上,然后派人把它送到旷野。 22这只公山羊担当他们的一切罪,将这一切罪带到荒无人烟的地方。

23亚伦要走进会幕,脱下他进至圣所时穿的细麻衣服,放在会幕里。 24他要在圣洁之处沐浴,穿上平时的衣服出去为自己和民众献燔祭,为自己和民众赎罪。 25他要将赎罪祭牲的脂肪焚烧在坛上。 26把羊送交阿撒泻勒的人要洗衣、沐浴,然后才可回到营里。 27作赎罪祭的公牛和公山羊的血被带进圣所用来赎罪,要把公牛和公山羊带到营外,用火焚烧它们的皮、肉和粪。 28负责焚烧的人要洗衣、沐浴,然后才可回到营里。

29“每年七月十日,不论是你们,还是寄居在你们中间的外族人,都要禁食,停止所有工作。这是你们要永远遵守的律例。 30因为在这一天要为你们赎罪,使你们在耶和华面前洁净。 31这天是你们的安息日,你们要禁食。这是一条永远不变的律例。 32那受膏、承受圣职、替代父亲做大祭司的要献祭赎罪。他要穿上圣洁的细麻衣, 33为至圣所、会幕和祭坛赎罪,也要为祭司和全体会众赎罪。 34这是你们要永远遵守的律例——每年一次为以色列人赎罪。”

于是,摩西遵行了耶和华的吩咐。