Kutoka 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 1:1-22

Waisraeli Waonewa

11:1 Mwa 46:8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake: 2Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; 3Isakari, Zabuloni na Benyamini; 41:4 Mwa 35:22-26; Hes 1:20-43Dani na Naftali, Gadi na Asheri. 51:5 Mwa 46:26Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri.

61:6 Mwa 50:26; Mdo 7:15Basi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, 71:7 Mwa 12:2; Kum 7:13; Eze 16:7lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

81:8 Yer 43:11; 46:2Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri. 91:9 Mwa 26:16Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi. 101:10 Mwa 15:13; Kut 3:7; 18:11; Za 64:2; 71:10; 83:3; 105:24-25; Isa 53:3; Mdo 7:17-19Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

111:11 Kut 3:7; 5:4, 10-14; 6:6-7; 2:11; Mwa 15:13; 47:11; Yos 9:27; Isa 60:10; 1Fal 9:19, 21; 1Nya 22:2; 2Nya 8:4Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao. 12Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli, 131:13 Mwa 15:13-14; Kut 5:21; 16:3; Law 25:43-53; Kum 4:20; 26:6; 1Fal 8:15; Za 129:1; Isa 30:6; 48:10; Yer 11:4kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili. 141:14 Kum 26:6; Ezr 9:9; Isa 14:3; Mwa 11:3; Kut 2:23; 3:9; Hes 20:15; Mdo 7:19; 1Sam 10:11; 2Sam 13:4Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

151:15 Mwa 35:17Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, 16“Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 171:17 Mit 16:6; 1Sam 22:17; Dan 3:16-18; Mdo 4:18-20; 5:29Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. 18Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

191:19 Law 19:11; Yos 2:4-6; 1Sam 19:14; 2Sam 17:20Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

201:20 Mit 11:18; 22:8; Mhu 8:12; Isa 3:10; Ebr 6:10Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. 211:21 1Sam 2:35; 2Sam 7:11, 27-29; 1Fal 11:38; 14:10Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

221:22 Mwa 41:1; Mdo 7:19Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

出埃及记 1:1-22

以色列人受欺压

1以色列的众子带着家眷跟雅各1:1 雅各”就是“以色列”,上帝为雅各改名以色列,故事参考创世记32:28一起去了埃及,以下是他们的名字: 2吕便西缅利未犹大3以萨迦西布伦便雅悯4拿弗他利迦得亚设5雅各的子孙总共有七十人。那时,约瑟已经住在埃及6后来,约瑟和他的弟兄以及同辈的人都相继去世。 7以色列人生养众多,人口大增,很快就遍布埃及,成为一个强大的民族。 8那时,埃及有一位不认识约瑟的新王登基, 9对他的百姓说:“你们看,以色列人比我们多,又比我们强。 10来吧!我们要设法阻止他们人口增长,否则一遇到战争,他们便会加入我们敌人的阵营来攻打我们,然后一走了之。”

11于是,埃及人派监工强迫以色列人服劳役,在比东兰塞两地为法老兴建储货城。 12以色列人越受奴役,人口增长得越快,散居的范围也越广,令埃及人感到恐惧。 13于是,埃及人更残酷地奴役他们, 14强迫他们和泥造砖,并做田间一切的苦工,使他们痛苦不堪。 15埃及王又命令两个希伯来的接生婆施弗拉普阿16“你们在替希伯来妇女接生的时候,如果看到生下的是男婴,就把他杀掉;如果是女婴,就让她活下来。” 17但这两个接生婆敬畏上帝,没有执行王的命令,而是保留了男婴的性命。 18埃及王召见那两个接生婆,质问她们:“你们为什么这样做?为什么让男婴活着?” 19她们回答说:“因为希伯来妇女跟埃及妇女不同。她们身体强健,我们还没有赶到,婴儿就生下来了。” 20-21因此,以色列人口继续增加,更加繁盛。因为这两个接生婆敬畏上帝,上帝便赐福给她们,使她们生儿育女。 22后来,法老命令全埃及的人把以色列人生的所有男婴都抛进尼罗河里,只让女婴活着。