Walawi 14 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 14:1-57

Kutakasa Kutoka Maambukizo Ya Magonjwa Ya Ngozi

1Bwana akamwambia Mose, 214:2 Law 13:57; Kum 24:8; Mt 8:2-4; Mk 1:40-44; Lk 5:12-14; 17:14“Haya ndiyo masharti yamhusuyo mtu mgonjwa wakati wa kufanyiwa ibada ya utakaso wakati aletwapo kwa kuhani: 3Kuhani atakwenda kumchunguza nje ya kambi. Kama mtu huyo atakuwa amepona ugonjwa wake wa ngozi wa kuambukiza, 414:4 Kut 12:22; Hes 19:6; Za 51:7; Ebr 9:19kuhani ataagiza vitu vifuatavyo viletwe kwa ajili ya mtu atakayetakaswa: ndege wawili safi walio hai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu, na hisopo. 5Kisha kuhani ataagiza kwamba mmoja wa ndege wale achinjwe kwenye chungu chenye maji safi. 6Kisha kuhani atamchukua ndege aliye hai na kumtumbukiza pamoja na mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo ndani ya damu ya yule ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi. 714:7 2Fal 5:10-14; Isa 52:15; Eze 36:25; Law 8:11; Ebr 10:22Atamnyunyizia yule mwenye ugonjwa wa kuambukiza maji hayo mara saba, na kumtangaza kuwa safi. Kisha atamwachia yule ndege aliye hai aende zake kwenye mashamba.

814:8 Law 11:25; 13:11; 15:5; 17:15; 22:6; Kut 29:4; Hes 5:2-3; 12:14-15; 19:7-8; 20; 31:24; 2Nya 26:21“Huyo mtu atakayetakaswa ni lazima afue nguo zake, anyoe nywele zake zote, na aoge kwa maji; ndipo atakapokuwa safi kwa desturi ya ibada. Baada ya hili anaweza kuingia kambini, lakini ni lazima akae nje ya hema lake kwa siku saba. 914:9 Law 13:5-6; Hes 6:9; Kum 21:12Siku ya saba ni lazima anyoe nywele zake zote; yaani anyoe nywele za kichwa, ndevu zake, kope zake na nywele nyingine zote. Ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa safi.

1014:10 Hes 6:10; 15:9; 28:20; Mt 8:4; Mk 1:44; Lk 5:14; Law 2:1; 4:32“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efa14:10 Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3. za unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja14:10 Logi ni kipimo cha ujazo ambacho ni sawa na lita 0.3. ya mafuta. 1114:11 Hes 6:10, 16Kuhani atakayemtangaza kuwa safi atahitaji kumkabidhi mgonjwa aliyepona pamoja na sadaka zake zote mbele za Bwana katika ingilio la Hema la Kukutania.

1214:12 Law 5:18; 6:6-7; Kut 29:24“Kisha kuhani atamchukua mmoja wa wale kondoo dume na kumtoa kuwa sadaka ya hatia, pamoja na ile logi moja ya mafuta; ataviinua mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 1314:13 Kut 29:11; Law 6:24-30; 7:7; Isa 53:7; Yn 1:29; 1Pet 1:19; Ufu 5:6Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjiwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; nayo ni takatifu sana. 1414:14 Kut 29:20; Law 8:23; Ufu 12:11; Ebr 9:9-14; Kol 1:14; 2Kor 7:1Kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya hatia na kuitia kwenye ncha ya sikio la kuume la yule atakayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. 15Kuhani atachukua sehemu ya ile logi ya mafuta, ayamimine kwenye kiganja cha mkono wake mwenyewe wa kushoto, 16na achovye kidole chake cha shahada cha mkono wake wa kuume kwenye mafuta yaliyoko kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho anyunyize mafuta hayo mara saba mbele za Bwana. 1714:17 Rum 6:13-22; 1Kor 6:20Kuhani atampaka yule anayetakaswa sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio lake la kuume, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia. 1814:18 Law 15:15; 4:26; Hes 15:28; Dan 9:24; Rum 3:23-25; 5:11; Efe 2:12-22; Kol 1:19-22Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake juu ya kichwa cha yule anayetakaswa, na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana.

1914:19 Law 5:3; 15:15“Kisha kuhani atatoa dhabihu ya sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwa ajili ya yule atakayetakaswa kutoka unajisi wake. Baada ya hayo, kuhani atachinja sadaka ya kuteketezwa 2014:20 Law 15:30na kuitoa juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya nafaka ili kumfanyia upatanisho, naye atakuwa safi.

2114:21 Law 5:7; 12:8; Ay 34:19; Mt 11:30; Lk 6:20; Mit 17:5; 1Yn 5:3“Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, lazima achukue mwana-kondoo mmoja kama sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho, pamoja na sehemu ya kumi ya efa14:21 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na lita 2. ya unga laini uliochanganywa na logi moja ya mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka, 2214:22 Law 5:7; 15:30; 12:8; Lk 2:24na hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kile atakachoweza kupata, mmoja kwa sadaka ya dhambi, na mwingine kwa sadaka ya kuteketezwa.

23“Katika siku ya nane, lazima avilete vitu hivyo kwa kuhani, kwa ajili ya kutakaswa kwake kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. 2414:24 Hes 6:14; 1The 5:23; 1Yn 1:7; Ufu 7:14Kuhani atamchukua mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia, pamoja na ile logi ya mafuta ya kuinuliwa mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 2514:25 Kut 29:20Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Pia ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. 26Kuhani atamiminia sehemu ya mafuta kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto, 27na kwa kidole chake cha shahada cha mkono wa kuume, atamnyunyizia yule anayetakaswa yale mafuta yaliyo kwenye kiganja chake mara saba mbele za Bwana. 28Atampaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake katika sehemu zote, kama alivyompaka damu ya sadaka ya hatia: yaani, kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. 29Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki katika kiganja chake kwenye kichwa cha yule anayetakaswa, na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana. 3014:30 Rum 8:3Kisha atatoa dhabihu wale hua ama yale makinda ya njiwa ambayo mtu ataweza kuwapata, 3114:31 Law 5:7; 15:15, 30mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele za Bwana kwa ajili ya yule anayetakaswa.”

3214:32 Law 13:2; 14:34; Mwa 12:5; 17:8; 48:4; Kut 6:4; Hes 13:2; 27:12; 32:22; Kum 3:27; 32:49; Isa 45:7; Amo 3:6Haya ndiyo masharti kwa mtu yeyote mwenye ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, na ambaye hana uwezo wa kutoa sadaka za kawaida kwa ajili ya kutakaswa kwake.

Kutakaswa Upele

33Bwana akawaambia Mose na Aroni, 34“Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani ambayo ninawapa kuwa milki yenu, nami nikaweka upele ueneao kwenye nyumba katika nchi ile, 3514:35 Za 91:10; Mit 3:33; Zek 5:4ni lazima mwenye nyumba hiyo akamwambie kuhani, ‘Nimeona kitu fulani kinachofanana na upele kwenye nyumba yangu.’ 3614:36 Hes 19:18; Za 51:7; Isa 52:11; 1Tim 5:22; Ufu 18:4Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba, kabla hajaenda kuchunguza kama ina ugonjwa huo, ili kitu chochote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili, kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba. 3714:37 Law 13:19; 14:38; 13:4-5Atachunguza upele huo katika kuta za nyumba hiyo, nazo kama zina rangi ya kijani kibichi au wekundu, na kuna mibonyeo ndani ya ukuta, 38kuhani atatoka na kufunga mlango wa nyumba hiyo kwa siku saba. 39Siku ya saba, kuhani atarudi kuikagua nyumba. Kama upele umeenea juu ya kuta, 40ataagiza kwamba mawe yote yaliyoambukizwa yaondolewe na kutupwa katika eneo lililo najisi nje ya mji. 41Kuta zote za ndani ya nyumba hiyo ni lazima zikwanguliwe, na kifusi chake kitupwe mahali najisi nje ya mji. 42Kisha watachukua mawe mengine na kujenga palipobomolewa kwa udongo mpya wa mfinyanzi, na kuipiga nyumba hiyo lipu mpya.

43“Ikiwa upele huo utatokea tena ndani ya ile nyumba baada ya mawe kuondolewa na nyumba kukwanguliwa na kuwekwa lipu mpya, 4414:44 Law 13:51kuhani atakwenda kuikagua, na kama upele umeenea ndani ya nyumba, basi ni upele uharibuo; nyumba hiyo ni najisi. 45Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na lipu yake, vyote vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi.

4614:46 Law 11:24; 17:15; 22:6; Hes 19:7-10; 1Kor 15:33“Yeyote atakayeingia katika nyumba hiyo ikiwa imefungwa, atakuwa najisi mpaka jioni. 4714:47 Law 11:25Yeyote atakayelala au kula ndani ya nyumba hiyo ni lazima afue nguo zake.

4814:48 Law 13:6; Kum 32:29; Ay 5:18; Hos 6:1; Mk 5:29; Lk 7:21“Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa upele haujaenea tena baada ya nyumba kupigwa lipu, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu upele umekwisha. 4914:49 1Fal 4:33Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo. 50Atamchinja mmoja wa wale ndege kwenye chungu chenye maji safi. 5114:51 Za 51:7; 1Fal 4:33Kisha atachukua mti wa mwerezi, hisopo, kitani nyekundu na ndege aliye hai, na kuvitumbukiza ndani ya damu ya ndege aliyechinjwa pamoja na maji safi, na kuinyunyizia nyumba ile mara saba. 52Ataitakasa nyumba kwa damu ya yule ndege, maji safi, ndege aliye hai, mti wa mwerezi, hisopo na kitani nyekundu. 53Kisha atamwachia yule ndege aliye hai huru mashambani nje ya mji. Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ile, nayo itakuwa safi.”

5414:54 Law 13:2Haya ndiyo masharti kuhusu aina yoyote ya ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, mwasho wowote, 5514:55 Law 13:47-52upele ndani ya nguo au ndani ya nyumba, 5614:56 Law 13:2; 14:57; 10:10; Kut 15:26; Kum 24:8; Za 78:5; 119:96; Mit 6:23kwa uvimbe, vipele au kipaku kingʼaacho, 57kupambanua wakati kitu fulani ni safi au najisi.

Haya ndiyo masharti kuhusu magonjwa ya ngozi ya kuambukiza na upele.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 14:1-57

痲瘋病患者的潔淨條例

1耶和華對摩西說: 2「以下是有關痲瘋病患者的潔淨條例。

「痲瘋病患者痊癒後,要通知祭司。 3祭司要到營外去檢查,如果發現他的病已痊癒, 4要吩咐人為他拿來兩隻潔淨的鳥、香柏木、朱紅色線和牛膝草。 5祭司要吩咐人在一個盛清水的陶器上宰殺一隻鳥, 6然後祭司要把另一隻鳥,連同香柏木、朱紅色線和牛膝草一起蘸在摻了清水的鳥血裡。 7祭司要用鳥血在他身上灑七次,宣佈他是潔淨的,然後放走那隻活鳥,讓牠飛向田野。 8他要洗淨衣服,剃去所有毛髮,沐浴之後便潔淨了,可以回到營內,但要住在自己的帳篷外七天。 9第七天,他要再次剃掉頭髮、鬍鬚和眉毛等各處毛髮,並洗衣、沐浴,之後便潔淨了。

10「第八天,他要帶來兩隻毫無殘疾的公羊羔、一隻毫無殘疾的一歲母羊羔、三公斤作素祭的調油的細麵粉和一杯油。 11主持潔淨禮的祭司要把他及其祭物帶到會幕門口、耶和華面前, 12並獻上一隻公羊羔和一杯油作贖過祭,作為搖祭在耶和華面前搖一搖。 13他要在殺贖罪祭牲和燔祭牲的聖潔之處宰公羊羔。贖過祭的祭物要歸祭司,像贖罪祭一樣,這是至聖之物。 14祭司要拿一些贖過祭祭牲的血抹在求潔淨者的右耳垂、右手大拇指和右腳大腳趾上。 15祭司要拿那杯油,倒一些在自己左手掌中, 16用一根右手指蘸左手掌裡的油,在耶和華面前彈灑七次, 17然後用手掌中剩下的油抹求潔淨者的右耳垂、右手大拇指和右腳大腳趾,就是抹了贖過祭祭牲血的地方。 18祭司要把手掌裡剩下的油抹在求潔淨者的頭上。這樣,祭司在耶和華面前為他贖了罪。 19祭司要獻上贖罪祭,為求潔淨者贖罪。然後,祭司要宰殺燔祭牲, 20在祭壇上獻燔祭和素祭,為他贖罪,他就潔淨了。

21「他如果貧窮,獻不起那麼多祭物,可以獻一隻公羊羔作贖過祭,用搖祭的方式贖罪;也要獻一公斤作素祭的調油的細麵粉和一杯油; 22還要按自己的能力獻兩隻斑鳩或雛鴿,一隻作贖罪祭,一隻作燔祭。 23第八天,他必須把這些祭物帶到會幕門口,在耶和華面前交給祭司。 24祭司要用作贖過祭的羊羔和一杯油作搖祭,在耶和華面前搖一搖。 25接著,祭司要宰殺作贖過祭的羊羔,拿一些羊血抹在他的右耳垂、右手大拇指和右腳大腳趾上。 26祭司也要把一些油倒在自己左手掌中, 27用一根右手指蘸左手掌中的油,在耶和華面前彈灑七次, 28然後把手掌中的一些油抹在他的右耳垂、右手大拇指和右腳大腳趾上,就是抹了贖過祭祭牲血的地方。 29祭司要把手掌裡剩下的油抹在他頭上,在耶和華面前為他贖罪。 30然後獻上那人按自己能力帶來的兩隻斑鳩或雛鴿, 31一隻作贖罪祭,一隻作燔祭。這樣,祭司在耶和華面前為他贖了罪。 32這是獻不起潔淨禮所需祭物的痲瘋病患者應當遵守的條例。」

處理房子發黴的條例

33耶和華對摩西亞倫說:

34「你們到了我賜給你們作產業的迦南以後,如果我使那裡的房屋中有發黴現象, 35屋主必須去告訴祭司,『我的房子裡好像有發黴現象。』 36祭司進去檢查前,要吩咐人把房子騰空,免得房子裡的一切都變得不潔淨。之後,祭司要進去檢查, 37如發現牆壁上出現紅色或綠色黴斑,並且侵入牆中, 38就要封閉房子七天。 39第七天,祭司要回去檢查。若發現牆壁上的黴斑蔓延, 40就要下令拆掉有黴斑的石塊,丟到城外不潔淨的地方, 41然後命人刮掉屋內牆壁上的灰泥,倒在城外不潔淨的地方。 42要另找石塊補被拆掉的地方,並用灰泥重新粉刷房子。

43「如果拆掉石塊、刮掉灰泥、重新粉刷以後,黴斑再度出現並蔓延, 44祭司要去檢查,若發現黴斑已蔓延,那房子就不潔淨。 45房主要拆掉房子,把石塊、木料和所有灰泥都丟到城外不潔淨的地方。 46房子封閉期間,任何人進去,都不潔淨,要等到傍晚才能潔淨。 47凡在房內睡覺或吃飯的人,都必須洗淨衣服。

48「祭司檢查粉刷後的房子,若發現房內沒有再度出現黴斑,就要宣佈房子是潔淨的。 49為潔淨房子,祭司要取兩隻鳥、香柏木、朱紅色線和牛膝草, 50在一個盛清水的陶器上宰殺一隻鳥, 51然後用香柏木、牛膝草、朱紅色線和另一隻活鳥蘸摻了清水的鳥血,向房子灑七次。 52祭司用鳥血、清水、活鳥、香柏木、牛膝草和朱紅色線潔淨那房子後, 53要放走那隻活鳥,讓牠飛到城外的田野。這樣,祭司為那房子贖了罪,房子就潔淨了。」

54以上是有關痲瘋病、疥癬、 55衣物或房子發黴、 56腫包、皮疹或白斑的條例。 57根據這些條例,可以分辨有關的人或物何時潔淨、何時不潔淨。