Mhubiri 8 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mhubiri 8:1-17

1Ni nani aliye kama mtu mwenye hekima?

Ni nani ajuaye maelezo ya mambo?

Hekima hungʼarisha uso wa mtu na kubadili ugumu wa uso wake.

Mtii Mfalme

2Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. 38:3 Rum 13:5; Mhu 10:4Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lolote apendalo. 48:4 Ay 9:12; 34:18; Dan 4:35; Es 1:18-19Kwa kuwa neno la mfalme ndilo lenye mamlaka ya mwisho, nani awezaye kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?”

5Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika,

moyo wa hekima utajua wakati muafaka

na jinsi ya kutenda.

68:6 Mhu 3:1Kwa maana kuna wakati muafaka

na utaratibu wa kila jambo,

ingawa huzuni ya mwanadamu

huwa nzito juu yake.

7Kwa vile hakuna mtu ajuaye siku zijazo,

ni nani awezaye kumwambia linalokuja?

8Hakuna mwanadamu

awezaye kushikilia roho yake asife,

wala hakuna mwenye uwezo

juu ya siku ya kufa kwake.

Kama vile hakuna yeyote arudishwaye nyuma wakati wa vita,

kadhalika uovu hautawaweka huru wale wautendao.

98:9 1Sam 18:12Yote haya niliyaona, nilipokuwa natafakari kila kitu kinachotendeka chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu hujifanya bwana juu ya wengine kwa madhara yake mwenyewe. 10Ndipo pia, nikaona waovu wakizikwa, wale ambao walizoea kuingia na kutoka mahali patakatifu na kupewa sifa katika mji ambapo walikuwa wamefanya haya. Hili nalo ni ubatili.

118:11 Ay 21:14-15; Rum 2:4-5; Isa 26:10Wakati hukumu juu ya tendo ovu haitekelezwi upesi, mioyo ya watu hujaa mipango ya kutenda maovu. 128:12 Za 37:18-19; Isa 3:10-11; 65:20; Mhu 3:14; Kum 4:40Ingawa mtu mwovu hufanya maovu mia moja na akaendelea kuishi maisha marefu, najua kwamba itakuwa bora zaidi kwa watu wanaomwogopa Mungu, wamchao Mungu. 138:13 Mhu 3:14; Kum 4:40; Ay 5:26; Za 34:12; Isa 65:20Lakini kwa sababu waovu hawamwogopi Mungu, hawatafanikiwa, maisha yao hayatarefuka kama kivuli.

148:14 Za 73:14; Mal 3:15; Mhu 2:14; 7:15; Ay 21:7Kuna kitu kingine ambacho ni ubatili kinachotokea duniani: Watu waadilifu kupata yale yanayowastahili waovu, nao waovu kupata yale yanayowastahili waadilifu. Hili nalo pia, nasema ni ubatili. 158:15 Law 26:5; Mhu 3:12-13; Kut 32:6; Za 42:8Kwa hiyo mimi ninasifu kufurahia maisha, kwa sababu hakuna kitu bora zaidi kwa mwanadamu chini ya jua kuliko kula, kunywa na kufurahi. Kisha furaha itafuatana naye kazini mwake siku zote za maisha yake ambazo amepewa na Mungu chini ya jua.

168:16 Mhu 1:13-17Nilipotafakari akilini mwangu ili nijue hekima na kuangalia kazi ya mwanadamu duniani, jinsi ambavyo macho yake hayapati usingizi mchana wala usiku, 178:17 Ay 5:9; 28:3, 23; Isa 40:28; Rum 11:33ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

传道书 8:1-17

1谁像有智慧的人呢?

谁知道事情的原委呢?

智慧能使人容光焕发,

使冷酷的面孔柔和。

2我劝你遵守王的命令,因为你曾在上帝面前这样发誓。 3不要在王面前鲁莽行事,也不要参与恶行,因为王可以随意行事。 4况且,王的命令至高无上,谁敢质问他呢? 5遵从王命的必免遭祸患,因为智者心里懂得做事的时机和方法。 6尽管人面临重重困难,但做任何事都有时机和方法。 7无人知道未来的事,谁能告诉人将来的事呢? 8无人能掌管生命8:8 生命”也可译作“风”或“气息”。,留住生命,也无人能掌管死期。无人能免于这场争战,邪恶也救不了作恶者。 9这一切我都见过了,我用心思考日光之下的一切事。有时人欺压人、伤害人。 10我看见恶人生前出入圣所,死后安葬,还在他们作恶的城中受到称赞,这也是虚空。 11对犯罪者的刑罚不迅速执行,世人便尽情作恶。 12虽然罪人作恶多端仍得长寿,我却认为敬畏上帝的人必亨通。 13然而,恶人得不到祝福,他们必像幻影一样不能长久,因为他们不敬畏上帝。 14世上有一件虚空的事,就是义人遭受了恶人当受的报应,恶人却享受了义人该享的福乐。我认为这也是虚空。 15因此,我便赞赏享乐,因为在日光之下没有什么比吃喝快乐更好。这是人在上帝所赐的年日里,从劳碌中当得的享受。 16我全心去寻求智慧,观察世上所发生的事,甚至昼夜不眠, 17思想上帝所做的一切,便知道人无法理解日光之下所发生的事。尽管人努力不懈地去寻找,也不能明白;即使智者自以为明白,他其实仍不能参透。