Mathayo 6 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 6:1-34

Kuwapa Wahitaji

16:1 Mt 5:16; 23:5; Rum 12:8“Angalieni msitende wema wenu mbele ya watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu aliye mbinguni.

2“Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na watu. Amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao. 36:3 Rum 12:8Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya, 46:4 Mt 6:6, 18; Kol 3:23-24ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo Baba yako wa mbinguni, yeye aonaye sirini atakupa thawabu kwa wazi.

Kuhusu Maombi

(Luka 11:2-4)

56:5 Mk 11:25; Lk 18:10-14“Nanyi msalipo, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupata thawabu yao. 66:6 1Fal 4:33Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako. 76:7 Mhu 5:2; 1Fal 18:26-29Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 86:8 Mt 6:32Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.

96:9 Lk 11:2-4; Yn 17:6“Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba:

“ ‘Baba yetu uliye mbinguni,

Jina lako litukuzwe.

10Ufalme wako uje.

Mapenzi yako yafanyike

hapa duniani kama huko mbinguni.

116:11 Mit 30:8Utupatie riziki yetu

ya kila siku.

126:12 Mt 18:21-35Utusamehe deni zetu,

kama sisi nasi tulivyokwisha

kuwasamehe wadeni wetu.

136:13 Yak 1:13; Mt 5:37Usitutie majaribuni,

bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu

[kwa kuwa Ufalme ni wako, na nguvu,

na utukufu, hata milele. Amen].’

146:14 Efe 4:32; Kol 3:13Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. 156:15 Mk 11:25-26; Mt 18:35Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Kuhusu Kufunga

166:16 Isa 58:5-9; Zek 8:19“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu. 176:17 Rut 3:3; Dan 10:3Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu 186:18 Mt 6:4, 6ili kufunga kwenu kusionekane na watu wengine ila Baba yenu aketiye mahali pa siri; naye Baba yenu aonaye sirini atawapa thawabu yenu kwa wazi.

Akiba Ya Mbinguni

(Luka 12:33-34)

196:19 Mt 23:4; Lk 12:16-21; Yak 5:2-3“Msijiwekee hazina duniani, mahali ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba. 206:20 1Tim 6:19; Mt 19:20; Lk 12:33-34; Kol 3:1-3Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba. 216:21 Lk 12:34Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa.

Jicho Ni Taa Ya Mwili

(Luka 11:34-36)

226:22 Lk 11:34-36“Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. 236:23 Mt 20:15Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani!

Mungu Na Mali

(Luka 16:13; 12:22-31)

246:24 Lk 16:9, 13“Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.6:24 Mali (au Utajiri) hapa inatoka neno Mamoni kwa Kiaramu au Mamona kwa Kiyunani.

Msiwe Na Wasiwasi

256:25 Flp 4:6; 1Pet 5:7“Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 266:26 Za 104:21; 136:25; Mt 10:29-31Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege? 276:27 Za 39:5Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake?

28“Nanyi kwa nini mnajitaabisha kwa ajili ya mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. 296:29 1Fal 10:4-7Lakini nawaambia, hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. 306:30 Mt 16:8; Lk 12:28Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 326:32 Mt 6:8Watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. 336:33 Za 37:4, 25; Rum 14:17; Mk 10:29-30Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia. 34Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 6:1-34

论周济穷人

1“你们要小心,行善的时候不可张扬,故意叫人看见,否则就不能得你们天父的赏赐了。

2“因此,周济穷人的时候,不要大吹大擂,像那些伪君子在会堂和街市上所行的一样,以博取人们的赞赏。我实在告诉你们,他们得到的赏赐仅此而已。 3你们周济穷人的时候,右手所做的别叫左手知道, 4要不声不响地去做。这样,鉴察隐秘事的天父必赏赐你们。

论祷告

5“你们祷告时,不要像伪君子那样。他们喜欢站在会堂里和十字路口上公开祷告,故意让人看见。我实在告诉你们,他们得到的赏赐不过是人的赞赏。 6你们祷告的时候,要进入内室,关上门,向你们肉眼看不见的父祈祷,鉴察隐秘事的父必赏赐你们。

7“你们祷告时不可像外族人那样喋喋不休,他们以为长篇大论,就必蒙上帝垂听。 8不可像他们那样,因为在你们祷告以前,你们的父已经知道你们的需要了。

9“你们应当这样祷告,

“‘我们天上的父,

愿人们都尊崇你的圣名,

10愿你的国度降临,

愿你的旨意在地上成就,就像在天上成就一样。

11求你今天赐给我们日用的饮食。

12饶恕我们的罪,

就像我们饶恕了得罪我们的人。

13不要让我们遇见诱惑,

救我们脱离那恶者。

因为国度、权柄、荣耀都是你的,直到永远。阿们!’

14“如果你们饶恕别人的过犯,你们的天父也必饶恕你们的过犯。 15如果你们不饶恕别人的过犯,你们的天父也不会饶恕你们的过犯。

论禁食

16“你们禁食的时候,不要像伪君子那样愁眉苦脸,因为他们故意蓬头垢面,好让别人知道他们在禁食。我实在告诉你们,他们得到的赏赐不过是人的赞赏。 17你禁食的时候要梳头洗脸, 18不叫人们看出你在禁食,只让你肉眼看不见的父知道,鉴察隐秘事的父必赏赐你。

论积财

19“不要为自己在世上积攒财宝,世上有虫子咬,会生锈,又有贼闯进来偷。 20你们要把财宝积攒在天上,天上没有虫子咬,不会生锈,也没有贼闯进来偷。 21要知道,你的财宝在哪里,你的心也在哪里。

22“眼睛是身上的灯。如果你的眼睛明亮,全身都光明; 23要是你的眼睛昏花6:23 昏花”或作“邪恶”。,全身就黑暗。如果你里面的光黑暗了,那黑暗是多么大啊!

24“一个人不能服侍两位主人,因为他不是恨这位、爱那位,就是重这位、轻那位。你们不能又事奉上帝,又崇拜金钱。

不要忧虑衣食

25“所以我告诉你们,不要为生活忧虑,如吃什么、喝什么,也不要为身体忧虑,如穿什么。难道生命不比饮食重要吗?身体不比穿着重要吗?

26“你们看天上的飞鸟,它们不种,不收,也不在仓里积存粮食,你们的天父尚且养活它们,难道你们还不如飞鸟贵重吗? 27你们谁能用忧虑使自己多活片刻呢?

28“何必为穿着忧虑呢?你们看看野地的百合花是如何生长的,它们既不劳苦,也不纺织。 29但我告诉你们,就连所罗门王最显赫时的穿戴还不如一朵百合花! 30你们的信心太小了!野地里的草今天还在,明天就丢在炉中化为灰烬,上帝还这样装扮它们,何况你们呢? 31所以,你们不要忧虑‘吃什么?喝什么?穿什么?’ 32因为这些都是外族人的追求,你们的天父知道你们的需要。

33“你们要先寻求上帝的国和祂的义,这一切都会赐给你们。 34所以,不要为明天忧虑,因为明天自有明天的忧虑,一天的难处一天担就够了。