Mathayo 25 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 25:1-46

Mfano Wa Wanawali Kumi

125:1 Mt 13:24; Mdo 20:8; Ufu 4:5; 19:7; 21:2“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 225:2 Mt 24:45Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. 3Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, 4lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. 525:5 1The 5:6Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

625:6 Mt 24:31; 1The 3“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’

725:7 Lk 12:35“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. 825:8 Lk 12:35Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’

9“Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’

1025:10 Ufu 19:9“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

1125:11 Lk 13:25, 27; Mt 7:21; 2:23“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’

1225:12 Mt 7:23; Za 5:5; Hab 1:12; Yn 9:31“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’

1325:13 Mk 13:35; Lk 12:40“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

Mfano Wa Watumishi Watatu Na Talanta

(Luka 19:11-27)

1425:14 Mt 21:33; Lk 19:21“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao. 1525:15 Mt 18:24-25Mmoja akampa talanta25:15 Talanta moja ilikuwa sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15. tano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri. 16Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi. 17Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi. 18Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake.

1925:19 Mt 18:23“Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao. 20Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta nyingine tano zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta tano zaidi.’

2125:21 Mt 24:45-47; Lk 16:10“Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’

22“Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, uliweka kwenye uangalizi wangu talanta mbili. Tazama nimepata hapa talanta mbili zaidi.’

2325:23 Mt 25:21“Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’

24“Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya mbegu. 25Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako.’

26“Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu. 27Vyema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, ili nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake.

28“ ‘Basi mnyangʼanyeni hiyo talanta, mkampe yule mwenye talanta kumi. 2925:29 Mk 4:25; Lk 19:26Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa. 3025:30 Mt 8:12Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

Kondoo Na Mbuzi

3125:31 Mt 16:27; Lk 17:30; Mt 19:28“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake. 3225:32 Mal 3:18; Eze 34:17-20Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi. 3325:33 Eze 34:17Atawaweka kondoo upande wake wa kuume, na mbuzi upande wake wa kushoto.

3425:34 Gal 5:21; Yak 2:5; Ebr 9:26; Ufu 17:8“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu; urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 3525:35 Isa 58:7; Ebr 13:2Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, 3625:36 Eze 18:7; Yak 2:15-16; 1:17; 2Tim 1:16nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’

3725:37 Mt 6:3“Ndipo wale wenye haki watakapomjibu, ‘Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa tukakulisha, au ukiwa na kiu tukakunywesha? 38Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha, au ukiwa uchi tukakuvika? 39Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza, au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’

4025:40 Mit 19:17; Ebr 6:10“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’

4125:41 Mt 7:23; Isa 66:24; 2Pet 2:4; Lk 3:17“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. 42Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha, 43nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza, na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’

44“Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’

4525:45 Mit 14:31; 17:5“Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’

4625:46 Gal 6:8; 1Yn 1:2; Dan 12:2; Yn 5:29“Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 25:1-46

十個伴娘的比喻

1「那時,天國就像十個伴娘提著燈去迎接新郎, 2其中五個是糊塗的,五個是聰明的。 3五個糊塗的只顧拿著燈,卻不預備油; 4那些聰明的不但拿著燈,還用器皿預備了足夠的油。 5新郎遲遲未到,她們等得困倦,便打盹睡著了。

6「到了半夜,忽然聽見有人喊道,『新郎來了!出來迎接吧!』 7伴娘們醒來,把燈點亮。 8糊塗的伴娘對聰明的伴娘說,『請給我們一些油吧,因為我們的燈快要滅了!』

9「聰明的伴娘回答說,『不行,我們的油不夠大家用的,你們去油店買吧!』

10「當糊塗的伴娘去買油的時候,新郎來了。那些預備好的伴娘跟他一同進去參加婚宴,門就關了。 11後來,其他伴娘回來了,喊道,『主啊!主啊!請給我們開門吧!』

12「新郎卻說,『我實在告訴你們,我不認識你們。』

13「所以,你們要警醒,因為你們不知道我回來的日子和時辰。

才幹的比喻

14「天國就像一個人即將遠行,他召來自己的奴僕,把產業託付給他們, 15按各人的才幹分別交給一個人五千銀幣,一個人兩千銀幣,一個人一千銀幣,然後便離開了。 16得到五千銀幣的立刻去做買賣,結果賺了五千; 17得到兩千銀幣的也賺了兩千; 18可是得到一千銀幣的卻挖了一個洞,把主人的錢藏在地裡。 19過了很久,這些奴僕的主人回來了,要跟他們結帳。 20得到五千銀幣的奴僕帶來了另外的五千,說,『主人,你交給我五千銀幣,請看,我又賺了五千。』

21「主人說,『做得好!你真是個又良善又忠心的奴僕。既然你在小事上忠心,我要把更大的事交給你。進來分享你主人的快樂吧!』

22「得到兩千銀幣的奴僕也上前說,『主人,你交給我兩千銀幣,請看,我又賺了兩千。』

23「主人說,『做得好!你真是個又良善又忠心的奴僕,既然你在小事上忠心,我要把更大的事交給你。進來分享你主人的快樂吧!』

24「得到一千銀幣的奴僕也上前說,『主人,我知道你為人苛刻,沒有播種的地方也要收割,沒有撒種的地方也要收穫。 25我很害怕,就去把你的錢藏在地裡。請看,這是你的錢。』

26「主人說,『你這又可惡又懶惰的奴僕!既然你知道我沒有播種的地方也要收割,沒有撒種的地方也要收穫, 27就應該把錢存入錢莊,等我回來時,可以連本帶利還給我。』

28「主人接著說,『收回他的一千銀幣,賞給那個有一萬銀幣的奴僕。 29因為凡有的,還要給他更多,使他豐富有餘;凡沒有的,連他僅有的,也要奪去。 30把這沒用的奴僕扔進外邊的黑暗裡,他必在那裡哀哭切齒。』

末日的審判

31「當人子在祂的榮耀中與眾天使降臨的時候,祂要坐在榮耀的寶座上, 32萬民要聚集在祂面前。祂要把他們分開,就像牧人把綿羊和山羊分開一樣。 33祂要把綿羊放在右邊,山羊放在左邊。 34那時,王會對右邊的人說,『我父所賜福的人啊,來承受創世以來為你們預備的國度吧。 35因為我饑餓時,你們給我吃的;我口渴時,你們給我喝的;我身在異鄉時,你們接待我; 36我赤身露體時,你們給我穿的;我生病時,你們照顧我;我坐牢時,你們來看我。』

37「那些義人會回答說,『主啊!我們什麼時候見你餓了就給你吃的?見你渴了就給你喝的? 38見你身在異鄉就接待你?見你赤身露體就給你穿的呢? 39我們又什麼時候見你生病或坐牢,就去看你呢?』

40「王會回答說,『我實在告訴你們,你們幫助我最卑微的一個弟兄,就是幫助我了。』

41「王又對左邊的人說,『你們這些被咒詛的人,走開!到專為魔鬼及其使者預備的永遠不滅的火裡去吧! 42因為我饑餓時,你們不給我吃的;我口渴時,你們不給我喝的; 43我身在異鄉時,你們不接待我;我赤身露體時,你們不給我衣服;我生病時,你們不照顧我;我坐牢時,你們不來看我。』

44「他們會問,『主啊,我們什麼時候見你餓了,或渴了,或身在異鄉,或赤身露體,或病了,或坐牢,卻沒有幫助你呢?』

45「王會回答說,『我實在告訴你們,你們沒有幫助我最卑微的一個弟兄,就是沒有幫助我。』 46這些人要受永遠的刑罰,但義人要得到永遠的生命。」