Mathayo 24 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 24:1-51

Kubomolewa Kwa Hekalu Kwatabiriwa

(Marko 13:1-2; Luka 21:5-6)

124:1 Mk 13:1; Lk 21:5Yesu akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu. 224:2 Lk 19:44; 1Fal 9:7; Yer 26:18; Mik 3:12Ndipo Yesu akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

Ishara Za Nyakati Za Mwisho

(Marko 13:3-23; Luka 21:7-24)

324:3 Mt 21:1Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

424:4 Efe 5:6; Kol 2:8, 18; 2The 2:3; 1Yn 4:1Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 524:5 Mt 24:11, 23-24; 1Yn 2:18Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’24:5 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. nao watawadanganya wengi. 624:6 Dan 2:26Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 724:7 Isa 19:2; Mdo 11:28Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

924:9 Mt 10:17; Yn 16:2“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. 1024:10 Dan 11:41Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. 1124:11 Mt 7; 15Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. 12Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, 1324:13 Mt 10:22lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 1424:14 Mt 4:23; Rum 10:18; Ufu 3:10Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.

1524:15 Mdo 6:13; Dan 11:31; 12:11“Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), 16basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. 1724:17 1Sam 9:25; Lk 12:3Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba. 18Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 1924:19 Lk 23:29Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! 2024:20 Mdo 1:12Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. 2124:21 Eze 5:9; Dan 12:1Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe. 2224:22 Isa 65:8, 9Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa. 2324:23 Lk 17:23; 21:8Wakati huo kama mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ Au, ‘Kristo yuko kule,’ msisadiki. 2424:24 Kut 7:11, 22; Ufu 16:14Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa. 25Angalieni, nimekwisha kuwaambia mapema.

26“Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. 2724:27 Lk 17:24; Mt 8:20Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 2824:28 Lk 17:37Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai.

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Marko 13:24-31; Luka 21:25-33)

2924:29 Sef 1:15; Ufu 8:12“Mara baada ya dhiki ya siku zile,

“ ‘jua litatiwa giza,

nao mwezi hautatoa nuru yake;

nazo nyota zitaanguka kutoka angani,

na nguvu za anga zitatikisika.’

3024:30 Dan 7:13; Ufu 1:7“Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 3124:31 Mt 13:41; Zek 9:14; 1The 4:16Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

3224:32 Lk 21:29“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 3324:33 Yak 5:9Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 3424:34 Mt 16:28; 23:36Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 3524:35 Mt 5:18Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

(Marko 13:32-37; Luka 17:26-30, 34-36)

3624:36 Mdo 1:7“Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. 3724:37 Mwa 6:5; 7:6-23Kama ilivyokuwa wakati wa Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 3824:38 Mt 22:30Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina. 3924:39 Lk 15Nao hawakujua lolote mpaka gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu. 4024:40 Lk 17:34-35Watu wawili watakuwa shambani, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. 4124:41 Lk 17:30Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa.

4224:42 Mt 25:13; Lk 12:40“Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. 4324:43 Lk 12:39Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. 4424:44 1The 5:6Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.

Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu

(Luka 12:41-48)

4524:45 Mt 25:21-23“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 4624:46 Ufu 16:15Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 4724:47 Mt 25:21, 23; Lk 22:29Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 4824:48 Mhu 8:11Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ 4924:49 Lk 21:34kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi. 50Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. 5124:51 Mt 8:12Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 24:1-51

預言聖殿被毀

1耶穌離開聖殿時,門徒上前把宏偉的聖殿指給祂看。 2耶穌對他們說:「你們看見這殿宇了嗎?我實在告訴你們,將來它要被完全拆毀,在這裡找不到兩塊疊在一起的石頭。」

世界末日的預兆

3耶穌正坐在橄欖山上,門徒私下來問祂:「請告訴我們,這事什麼時候會發生?你再來和世界末日的時候會有什麼預兆?」

4耶穌回答說:「你們要小心,免得被人迷惑。 5因為將來會有許多人冒我的名而來,說『我是基督』,欺騙許多人。 6你們聽見戰爭爆發、戰訊頻傳時,不要驚慌,因為這些事必然發生,只是末日還沒有到。 7民族將與民族互鬥,國家將與國家相爭,各處將有饑荒和地震。 8這些只是災難24·8 災難」希臘文是「生產之痛」。的開始。

9「那時,你們將遭人迫害、殺害,並因我的名而被萬民憎恨。 10那時,許多人會放棄信仰,互相出賣,彼此憎恨。 11許多假先知也會出現,迷惑許多人。 12由於罪惡氾濫,許多人的愛逐漸冷淡。 13但堅忍到底的必定得救。 14這天國的福音將傳遍天下,讓萬民都聽見,然後末日才會來臨。

15「當你們看見但以理先知所說的『那帶來毀滅的可憎之物』站立在聖地的時候(讀者須會意), 16住在猶太地區的人要趕快逃到山上去, 17在屋頂上的人不要下來進屋收拾行李, 18在田間工作的人也不要回家取外衣。 19那時,孕婦和哺育嬰兒的母親們可就遭殃了! 20你們要祈求上帝,不要讓你們在冬天或安息日逃難, 21因為那時世上將有空前絕後的大災難。 22如果不縮短災期,恐怕沒有人能活命。但為了選民的緣故,災期必被縮短。

23「那時,如果有人對你們說,『看啊!基督在這裡』,或說,『基督在那裡』,你們不要相信。 24因為假基督和假先知將出現,行很大的神蹟奇事來迷惑人,如果可能,甚至要迷惑上帝揀選的子民。 25你們要記住,我已經預先告訴你們了。

26「因此,如果有人對你們說,『看啊!基督在曠野』,你們不要出去;或者說,『看啊!基督在屋裡』,你們也不要相信。 27人子降臨時的情形就像閃電從東方發出一直照到西方。 28屍體在哪裡,禿鷹就會聚集在哪裡。

29「當災難的日子一過,

『太陽變黑,

月亮無光,

眾星隕落,

天體震動。』

30「那時,天上會出現人子降臨的預兆,地上的萬族都要哀哭,他們將看見人子帶著能力和極大的榮耀駕著天上的雲降臨。 31在響亮的號聲中,祂將差遣天使從四面八方、天涯海角招聚祂揀選的人。

無花果樹的比喻

32「你們可以從無花果樹學個道理。當無花果樹發芽長葉的時候,你們就知道夏天快來了。 33同樣,當你們看見這一切事發生時,就知道人子快來了,就在門口。 34我實在告訴你們,這個世代還沒有過去,這一切都要發生。 35天地都要過去,但我的話永遠長存。

警醒準備

36「但沒有人知道那日子和時辰何時來到,連天上的天使也不知道,人子24·36 人子」希臘文是「子」。也不知道,只有天父知道。 37人子降臨時的情形就像挪亞的時代。 38洪水來臨之前,人們吃吃喝喝,男婚女嫁,一直到挪亞進方舟那天; 39他們懵然不知,直到洪水來把他們全沖走了。人子降臨時的情形也是這樣。 40那時,兩個人在田裡,一個將被接去,一個將被撇下; 41兩個婦人推磨,一個將被接去,一個將被撇下。 42所以,你們要警醒,因為你們不知道你們的主會在哪一天來。 43你們都知道,如果一家的主人知道賊會在半夜幾點來,就必警醒,不讓賊入屋偷竊。 44同樣,你們也要做好準備,因為在你們意想不到的時候,人子就來了。

兩種奴僕

45「誰是那個受主人委託管理家中大小僕役、按時分糧食給他們、又忠心又精明的奴僕呢? 46主人回家時,看見他盡忠職守,他就有福了。 47我實在告訴你們,主人一定會把所有產業都交給他管理。 48但如果奴僕邪惡,以為主人不會那麼快回來, 49就毆打同伴,跟醉漢一起吃喝玩樂, 50主人會在他想不到的日子、不知道的時辰回來, 51嚴厲地懲罰24·51 嚴厲地懲罰」或作「腰斬」。他,判他和偽君子同樣的罪。他必在那裡哀哭切齒。