Kutoka 37 – NEN & PCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 37:1-29

Sanduku La Agano

(Kutoka 25:10-22)

137:1 Kut 31:2; 30:6; 39:35; Kum 10:3; Kut 35:30; 25:10Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu,37:1 Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13. upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. 2Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. 3Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 437:4 Hes 4:6Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 537:5 Hes 1:50; 2Sam 6:3Akaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba.

637:6 Kut 26:34; 31:7; Ebr 9:5; Kut 25:17Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 737:7 Eze 41:18Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 8Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 937:9 Ebr 9:5; Kum 10:3; Mwa 3:24; Kut 25:22; 1Fal 6:23; 2Nya 3:10; Za 80:1; Eze 1:5-28; 10:1; Yn 1:51; Flp 2:10; 1Tim 3:16; 1Pet 1:12Makerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko.

Meza

(Kutoka 25:23-30)

1037:10 Kum 31:8; Ebr 9:2; Kut 15:23; Mal 1:7, 12Akatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,37:10 Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90. upana wa dhiraa moja,37:10 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 12Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,37:12 Nyanda nne ni sawa na sentimita 8. na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 13Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 1437:14 Ebr 9:4Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. 15Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. 1637:16 Kut 25:29Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji.

Kinara Cha Taa

(Kutoka 25:31-40)

1737:17 Ebr 9:2; Ufu 1:12; Kut 25:31; Law 24:4; 1Nya 28:15; Zek 4:2; Mt 5:15, 16; Yn 5:35; Flp 2:15; 1Pet 2:9; Ufu 1:20Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. 18Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 19Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. 2037:20 Hes 17:8; Yer 1:11Juu ya kinara chenyewe kulikuwepo na vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. 21Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla. 2237:22 Hes 8:4Matovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi.

2337:23 Kut 40:4, 25; Ufu 1:20; 4:5Akatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. 24Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta37:24 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. moja ya dhahabu safi.

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

(Kutoka 30:1-5)

2537:25 Kut 30:34-36; Lk 1:11; Ebr 9:4; Ufu 8:3; Kut 27:2; Ufu 9:13; 1Fal 9:25; 1Nya 29:6, 7; Isa 60:6; Mal 1:11; 1Pet 2:5Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. 26Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. 27Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko iliyotumika kuyabebea madhabahu. 2837:28 Kut 25:13Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.

2937:29 Kut 31:11; 30:1, 25; 39:38; Isa 61:1; 11:2; Za 133:2; 1Yn 2:20; Za 141:2; Wim 4:14; Mal 1:11; Ebr 5:7; 7:25; Ufu 5:8; 8:3, 4Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako, na uvumba safi wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato.

Persian Contemporary Bible

خروج 37:1-29

ساختن صندوق عهد

(خروج 25‏:10‏-22)

1بصل‌ئيل، صندوق عهد را از چوب اقاقيا كه درازای آن يک متر و ۲۵ سانتی متر و پهنا و بلندی آن هر كدام هفتاد و پنج سانتی متر بود، ساخت. 2بيرون و درون آن را با طلای خالص پوشانيد و نواری از طلا دور لبهٔ آن كشيد. 3برای صندوق چهار حلقه از طلا آماده كرد و آنها را در چهار گوشهٔ قسمت پايين آن متصل نمود، يعنی در هر طرف دو حلقه. 4‏-5بعد دو چوب بلند تهيه شده از درخت اقاقيا با روكش طلا برای برداشتن صندوق فراهم ساخت و چوبها را در داخل حلقه‌های دو طرف صندوق گذاشت.

6سرپوش صندوق يعنی تخت رحمت را به درازای يک متر و ده سانتيمتر و پهنای هفتاد سانتيمتر، از طلای خالص درست كرد. 7‏-8سپس دو مجسمهٔ فرشته از طلا در دو سر تخت رحمت ساخت. فرشته‌ها را طوری روی تخت رحمت ساخت كه با آن يكپارچه شد. 9مجسمهٔ فرشته‌ها، روبروی هم و نگاهشان به طرف تخت و بالهايشان بر بالای آن گسترده بود.

ساختن ميز نان مقدس

(خروج 25‏:23‏-30)

10آنگاه بصل‌ئيل، ميز نان مقدس را از چوب اقاقيا به درازای يک متر و پهنای نيم متر و بلندی ۷۵ سانتی متر ساخت. 11آن را با روكشی از طلای خالص پوشانيد و قابی از طلا بر دور تا دور لبهٔ آن نصب كرد. 12حاشيهٔ دور لبهٔ ميز را به پهنای چهار انگشت درست كرد و دور حاشيه را با قاب طلا پوشانيد. 13‏-14چهار حلقه از طلا برای ميز ساخت و حلقه‌ها را به چهار گوشهٔ بالای پايه‌های ميز نصب كرد. اين حلقه‌ها برای چوبهايی بود كه به هنگام برداشتن و جابه‌جا كردن ميز می‌بايست در آنها قرار گيرد. 15اين چوبها را از درخت اقاقيا با روكش طلا ساخت. 16همچنين بشقابها، كاسه‌ها، جامها و پياله‌هايی از طلای خالص برای ريختن هدايای نوشيدنی درست كرد تا آنها را روی ميز بگذارند.

ساختن چراغدان

(خروج 25‏:31‏-40)

17چراغدان را نيز از طلای خالص درست كرد. پايه و بدنهٔ آن را يكپارچه و از طلای خالص ساخت و نقش گلهای روی آن را نيز كه شامل كاسبرگ و غنچه بود از طلا درست كرد. 18بر بدنهٔ چراغدان شش شاخه قرار داشت، يعنی در هر طرف سه شاخه. 19روی هر يک از شاخه‌ها سه گل بادامی شكل بود. 20‏-21خود بدنه را با چهار گل بادامی شكل تزيين كرد طوری كه گلها بين شاخه‌ها و بالا و پايين آنها قرار گرفتند. 22تمام اين نقشها و شاخه‌ها و بدنه از يک تكه طلای خالص بود. 23هفت چراغ آن و انبرها و سينی‌هايش را از طلای خالص ساخت. 24برای ساختن اين چراغدان و لوازمش سی و چهار كيلو طلا به کار رفت.

ساختن قربانگاه بخور

(خروج 30‏:1‏-5)

25قربانگاه بخور را به شكل چهارگوش به ضلع نيم متر و بلندی يک متر از چوب اقاقيا درست كرد. آن را طوری ساخت كه در چهار گوشهٔ آن چهار زائده به شكل شاخ بود. 26روكش قربانگاه و شاخهای آن از طلای خالص بود. قابی دور تا دور آن از طلا درست كرد. 27در دو طرف قربانگاه، زير قاب طلايی، دو حلقه از طلا برای قرار گرفتن چوبها ساخت تا با آنها قربانگاه را حمل كنند. 28اين چوبها از درخت اقاقيا تهيه شده بود و روكش طلا داشت.

تهيهٔ روغن مسح و بخور

(خروج 30‏:22‏-38)

29سپس روغن مسح مقدس و بخور خالص معطر را تهيه كرد.