Isaya 65 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 65:1-25

Hukumu Na Wokovu

165:1 Rum 10:20; Efe 2:12-13; Rum 9:30; Za 22:27; Hos 1:10; Rum 9:24-26; Isa 43:7“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’

265:2 Za 78:8; Rum 10:21; Za 81:11-12; Mit 24:2; Isa 66:18Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu

kwa watu wakaidi,

wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,

wafuatao mawazo yao wenyewe:

365:3 Isa 1:29; Law 17:5; Ay 1:11; Yer 41:5; Eze 23:41; Yer 44:17taifa ambalo daima hunikasirisha

machoni pangu,

wakitoa dhabihu katika bustani

na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali;

465:4 Law 11:7; Isa 8:19; Law 19:31; Kum 18:11watu waketio katikati ya makaburi

na kukesha mahali pa siri,

walao nyama za nguruwe,

nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,

565:5 Za 40:4; Lk 7:39; Yud 19; Mt 9:11; Lk 18:9-12; Mit 10:26wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,

kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’

Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,

ni moto uwakao mchana kutwa.

665:6 2Nya 6:23; Kum 32:34; Za 50:3; Yer 16:18; Lk 6:38; Isa 59:18; Za 79:12; Eze 9:10“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:

sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;

nitalipiza mapajani mwao:

765:7 Kut 20:5; Yer 32:18; Law 26:39; Isa 22:14; Mit 10:24; Isa 10:12; 57:7dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”

asema Bwana.

“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima

na kunichokoza mimi juu ya vilima,

nitawapimia mapajani mwao

malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”

865:8 Isa 5:2; 54:17; Kut 4:22; Yer 3:4; Isa 29:16; Rum 9:20-21; Ay 10:3Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana

katika kishada cha zabibu,

nao watu husema, ‘Usikiharibu,

kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’

hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;

sitawaangamiza wote.

965:9 Isa 45:19; Hes 34:13; Amo 9:11-15; Isa 32:18; Yer 50:19Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,

na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,

nao watu wangu wateule watairithi,

nako huko wataishi watumishi wangu.

1065:10 1Nya 27:29; Hos 2:15; Mdo 9:35; Yos 7:26; Isa 35:2; Yer 31:12; Eze 34:13-14Sharoni itakuwa malisho

kwa ajili ya makundi ya kondoo,

na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia

kwa makundi ya ngʼombe,

kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta.

1165:11 Eze 23:41; Yer 19:4; 1Kor 10:21; Kum 29:24-25; 32:15; Yer 2:13; 19:4“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana

na kuusahau mlima wangu mtakatifu,

ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,65:11 Bahati alikuwa mungu wa Wakaldayo ambaye pia alijulikana kama Gadi.

na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa

kwa ajili ya Ajali,65:11 Ajali au Meni alikuwa mungu wa majaliwa.

1265:12 Mit 1:24-25; Yer 7:27; 2Nya 36:15-16; Yer 13:11; Isa 1:20; 30:25; Mik 5:15nitawaagiza mfe kwa upanga,

nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa;

kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika,

nilisema lakini hamkusikiliza.

Mlitenda maovu machoni pangu,

nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.”

1365:13 Isa 1:19; Ay 18:12; Lk 6:25; Isa 33:16; 60:5; 44:9Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Watumishi wangu watakula,

lakini ninyi mtaona njaa;

watumishi wangu watakunywa

lakini ninyi mtaona kiu;

watumishi wangu watafurahi,

lakini ninyi mtaona haya.

1465:14 Isa 15:2; Lk 13:28; Za 109:28; Sef 3:14-20; Yak 5:13; Mt 8:12Watumishi wangu wataimba

kwa furaha ya mioyo yao,

lakini ninyi mtalia

kutokana na uchungu wa moyoni,

na kupiga yowe kwa sababu

ya uchungu wa roho zenu.

1565:15 Hes 5:27; Mdo 11:26; Zek 8:13; Za 102:8; Mwa 32:28; Ufu 2:17Mtaliacha jina lenu

kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa;

Bwana Mwenyezi atawaua ninyi,

lakini watumishi wake atawapa jina jingine.

1665:16 Za 31:5; Ufu 3:14; Isa 19:18; Kum 29:19; Ay 11:16; Za 63:11Yeye aombaye baraka katika nchi

atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli;

yeye aapaye katika nchi

ataapa kwa Mungu wa kweli.

Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika

na kufichwa kutoka machoni pangu.

Mbingu Mpya Na Dunia Mpya

1765:17 2Kor 5:17; 2Pet 3:13; Yer 3:16; Ufu 7:17; Isa 41:22; 43:18“Tazama, nitaumba

mbingu mpya na dunia mpya.

Mambo ya zamani hayatakumbukwa,

wala hayatakuja akilini.

1865:18 Kum 32:43; Za 98:1-9; Isa 25:9; Ufu 21:2Lakini furahini na kushangilia daima

katika hivi nitakavyoumba,

kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,

nao watu wake wawe furaha.

1965:19 Isa 35:10; 62:5; Ufu 7:17; Kum 30:9; Isa 25:8Nami nitaifurahia Yerusalemu

na kuwafurahia watu wangu;

sauti ya maombolezo na ya kilio

haitasikika humo tena.

2065:20 Mwa 15:15; Mhu 8:12; Zek 8:4; Isa 11:8; Mwa 5:1-32“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake

mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu,

au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake.

Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja

atahesabiwa kwamba ni kijana tu,

yeye ambaye hatafika miaka mia moja,

atahesabiwa kuwa amelaaniwa.

2165:21 Isa 32:18; 2Fal 19:29; Eze 28:26; Isa 61:4; 37:30; Amo 9:14Watajenga nyumba na kuishi ndani yake;

watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.

2265:22 Za 92:12-14; 21:4; 91:16; Kum 28:30; Isa 14:1Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,

au kupanda mazao na wengine wale.

Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,

ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,

wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi

kazi za mikono yao.

2365:23 Mwa 12:2; Kum 28:3-12; Mdo 2:39; Hos 9:12; Isa 49:4; 1Kor 15:58; Yer 3:4Hawatajitaabisha kwa kazi bure,

wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga,

kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana,

wao na wazao wao pamoja nao.

2465:24 Dan 9:20-23; 10:12; Mt 6:8; Isa 55:6; Ay 8:6; Zek 10:6; Isa 30:19Kabla hawajaita, nitajibu,

nao wakiwa katika kunena, nitasikia.

2565:25 Mwa 3:14; Rum 16:20; Mik 7:17; Isa 11:6; Dan 2:35; Ay 40:15; 5:23; Isa 2:4Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja,

naye simba atakula nyasi kama maksai,

lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.

Hawatadhuru wala kuharibu

katika mlima wangu mtakatifu wote,”

asema Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以赛亚书 65:1-25

惩罚与拯救

1耶和华说:“我向没有求问我的人显现,

让没有寻找我的人寻见,

对没有求告我的国家说,

‘我在这里,我在这里!’

2我整天伸出双手招呼一群悖逆的百姓,

他们却任意妄为,

不走正路,

3不断地当面惹我发怒。

他们在园中献祭,

在砖台上烧香,

4坐在坟场里,

宿在隐秘处。

他们吃猪肉,

用不洁之物做汤,

5还对人说,‘站远点,

别挨近我,因为我比你圣洁!’

我被这些人气得鼻孔冒烟,

整天怒火难息。

6看啊,这些都记录在我面前,

我不会再保持缄默,

我要报应他们,

7按他们和他们祖先的罪报应他们。

我必按他们的所作所为报应他们,

因为他们在山上烧香,

在丘陵上亵渎我。

这是耶和华说的。”

8耶和华说:“人发现一串葡萄尚可酿造新酒时,

一定会说,‘不要毁坏它,

里面还有好葡萄。’

同样,因我仆人的缘故,

我也不会把他们全部毁灭。

9“我必使雅各的后裔兴起,

使犹大人兴起,

继承我的群山。

我拣选的子民必拥有那片土地,

我的仆人必在那里安居。

10沙仑必成为牧放羊群的草场,

亚割谷必成为牛群休憩的地方,

这些地方必属于寻求我的人。

11但至于你们这些背弃我、

忘记我的圣山、

摆宴供奉幸运之神、

调酒祭奠命运之神的人,

12我要使你们注定被杀,

丧身刀下。

因为我呼唤你们,你们不回应;

我讲话,你们不聆听。

你们做我视为恶的事,

专行令我不悦的事。”

13所以主耶和华说:

“看啊,我的仆人必有吃有喝,

你们却要饥渴交加;

我的仆人必欢喜,

你们却要受羞辱;

14我的仆人必欢喜快乐,

扬声歌唱,

你们却要伤心欲绝,

嚎啕大哭。

15我的选民必用你们的名字作咒诅,

主耶和华必杀死你们,

给祂的仆人另起名字。

16因此,在地上求福祉的人都必向信实的上帝祈求,

在地上起誓的人都必凭信实的上帝起誓。

因为过去的苦难已经被遗忘,

从我眼前消失了。

新天新地

17“看啊,我要创造新天新地,

过去的一切都要被遗忘,

从记忆中消失。

18你们要因我创造的一切而永远欢喜快乐。

看啊,我要创造一个充满喜乐的耶路撒冷

其中的居民个个欢欣。

19我必因耶路撒冷而欢喜,

因我的子民而快乐。

城里再听不见哭泣和哀号声。

20再没有只活几天便夭折的婴儿,

也没有寿数未尽便死的老人,

因为满了百岁便死的人不过算是青年,

不足百岁便死的人被视为受了咒诅。

21他们要建造房屋,安然居住,

栽种葡萄园,吃园中的果子。

22他们建的房屋再不会被别人居住,

他们种的果实再不会被别人享用。

我的子民必像树木一样长寿,

我拣选的人必长享自己亲手劳碌的成果。

23他们不会徒劳,

他们的孩子也不会遇到灾祸,

因为他们及其子孙是蒙上帝赐福的人。

24他们还没有求告,

我就已经应允;

他们正要祷告,

我就已经垂听。

25豺狼和绵羊必一起吃草,

狮子必像牛一样吃草,

蛇必以尘土为食。

在我的整个圣山上,

它们都不伤人,不害物。

这是耶和华说的。”