Yeremia 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 1:1-19

11:1 Yos 21:18; Yer 32:7-9Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini. 2Neno la Bwana lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, 31:3 2Fal 24:17; Yer 29:2; 52:15; Ezr 5:12; 2Fal 23:34na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.

Wito Wa Yeremia

4Neno la Bwana lilinijia, kusema,

51:5 Yer 25:15-26; Za 139:13-16; Yn 10:36“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

61:6 Kut 3:11; 4:10; 6:12; 1Fal 3:7Nami nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”

7Lakini Bwana akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. 81:8 Mwa 8:1; Kut 3:12; Eze 2:6; Yer 15:20; Hes 22:20; Mwa 26:3; Yer 26:24Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema Bwana.

91:9 Isa 6:7; Kut 4:12Kisha Bwana akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. 101:10 Yer 25:15; 18:7-10; 31:4, 28; 12:17; 24:6Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”

111:11 Yer 24:3; Amo 7:8-9Neno la Bwana likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”

Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”

121:12 Ay 29:2; Yer 44:27Bwana akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”

131:13 Zek 4:2; 5:2; Yer 24:3Neno la Bwana likanijia tena, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”

141:14 Isa 14:31Bwana akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi. 151:15 Yer 9:11; 10:22; 39:3; 4:16Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Bwana.

“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi

katika maingilio ya malango ya Yerusalemu,

watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,

na dhidi ya miji yote ya Yuda.

161:16 Mwa 6:5; Yer 4:12; Kum 28:20; Yer 17:13; Kut 20:3; Yer 44:3-4; 19:4; Hes 25:3Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu

kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,

kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine

na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.

171:17 Kum 31:6; 1Fal 18:46; Eze 2:6; Yer 7:27; 42:4“Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao. 181:18 Isa 50:7Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. 191:19 Mwa 26:3; Isa 43:2; Mit 20:22; Hes 14:9; Mdo 26:17; Za 129:2Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Bwana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 1:1-19

1希勒迦的儿子耶利米便雅悯境内亚拿突城的一位祭司,以下是他的话。 2犹大亚们的儿子约西亚执政第十三年,耶和华的话传给了耶利米3犹大约西亚的儿子约雅敬开始执政,一直到约西亚的另一个儿子西底迦犹大王的第十一年五月,就是耶路撒冷的居民被掳之日,耶和华的话常常传给耶利米

耶利米蒙召

4耶和华对我说:

5“我还没有使你在母腹中成形,就认识你;

你还未出生,我已使你圣洁,

立你做万国的先知。”

6我回答说:“主耶和华啊,我太年轻,不懂得怎样说话。” 7耶和华却说:

“不要说你太年轻,

我派你去谁那里,

你就去谁那里;

我吩咐你说什么,

你就说什么。

8谁也不要怕,

因为我与你同在,

我必拯救你。

这是耶和华说的。”

9然后,耶和华伸手摸我的口,对我说:“看啊,我已把我的话放在你口中。 10今日,我派你到列邦列国去拔掉、拆除、毁灭、推翻、建造和栽植。”

两个异象

11耶和华又对我说:“耶利米,你看见什么?”我说:“我看见一根杏树枝。” 12耶和华说:“不错。我必实现我说过的话。”

13耶和华又对我说:“你看见什么?”我回答说:“我看见一锅煮沸的水,从北方倾倒下来。” 14耶和华说:“不错。因为有灾祸要从北方降临到这地方的一切居民。 15我要召来北方各国,他们要在耶路撒冷的城门自立王位,攻打耶路撒冷周围的城墙和犹大各城邑。这是耶和华说的。 16我要审判他们,因为他们犯罪作恶,背弃我,给别的神明烧香,又跪拜自己制造的神像。 17现在,你要做好准备,去把我吩咐你的话告诉他们。不要惧怕他们,不然我将使你在他们面前充满恐惧。 18看啊,今天我已使你成为坚城、铁柱、铜墙,来对抗整个犹大,对抗犹大的君王、首领、祭司和境内的众民。 19他们必攻击你,但绝不能胜过你,因为我与你同在,我必拯救你。这是耶和华说的。”