Isaya 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 5:1-30

Wimbo Wa Shamba La Mizabibu

15:1 Za 80:8-9; Yn 15:1; Isa 27:2Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,

kuhusu shamba lake la mizabibu:

Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu

kwenye kilima chenye rutuba.

25:2 Kum 32:6; Kut 15:17; Yer 2:21; Mt 21:19; Mk 11:13; Isa 16:8; 27:3; 1Sam 2:9; Ay 24:11; Mt 21:33; Lk 13:6Alililima na kuondoa mawe

na akaliotesha mizabibu bora sana.

Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,

na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.

Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,

lakini lilizaa matunda mabaya tu.

35:3 Mt 21:40“Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,

hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu.

45:4 2Nya 36:15; Mt 23:37; Yer 2:5-7; 2:21; Mk 6:3-4; Yer 24:2; 29:17Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu

kuliko yale niliyofanya?

Nilipotazamia kupata zabibu nzuri,

kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu?

55:5 Za 80:12; Lk 21:24; Yer 12:10; Isa 6:12; 27:10; 22:5; 10:6; 2Nya 36:21Sasa nitawaambia lile nitakalolitendea

shamba langu la mizabibu:

Nitaondoa uzio wake,

nalo litaharibiwa,

nitabomoa ukuta wake,

nalo litakanyagwa.

65:6 Hos 2:12; Ebr 6:8; Mwa 6:13; Isa 6:13; 49:17; 2Sam 23:6; Isa 7:23-24; Law 26:32; Eze 28:24; 2Sam 1:21; Amo 4:7Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,

halitakatiwa matawi wala kulimwa,

nayo michongoma na miiba itamea huko,

nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.”

75:7 Isa 37:30; Eze 9:9; 22:29; Za 80:8; Isa 17:10; 10:2; 29:21; 61:8; Za 12:5Shamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote

ni nyumba ya Israeli,

na watu wa Yuda

ni bustani yake ya kumpendeza.

Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,

alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.

Ole Na Hukumu

85:8 Yer 22:13; Isa 24:16; 6:5; 10:1; Hab 2:9-12; Ay 20:19; Mik 2:2Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba

na kuunganisha mashamba baada ya mashamba

hadi hakuna nafasi iliyobaki,

nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.

95:9 Isa 6:11-12; Mt 23:38; Yer 44:11; Isa 22:14; Mt 23:38Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia:

“Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa,

nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa.

105:10 Law 27:16; Kum 28:38; Zek 8:10; Law 26:26; 27:16Shamba la mizabibu la eka kumi

litatoa bathi5:10 Bathi moja ni sawa na lita 22. moja ya divai,

na homeri5:10 Homeri moja ni sawa na lita 220. ya mbegu zilizopandwa

itatoa efa5:10 Efa moja ni sawa na lita 22. moja tu ya nafaka.”

115:11 1Sam 25:36; Mit 23:29-30Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema

wakikimbilia kunywa vileo,

wale wakawiao sana mpaka usiku,

mpaka wamewaka kwa mvinyo.

125:12 1Sam 12:24; Ay 34:27; Eze 26:13; Amo 6:5-6; Isa 24:8; Ay 21:12; Za 28:5; 68:25Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao,

matari, filimbi na mvinyo,

lakini hawayajali matendo ya Bwana,

wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.

135:13 Isa 49:21; 1:3; 3:3; Mit 10:21; Hos 4:6; Rum 1:28; Ay 22:8Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishoni

kwa sababu ya kukosa ufahamu,

watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaa

na watu wao wengi watakauka kwa kiu.

145:14 Mit 30:16; Hes 16:30; Isa 22:13; 23:7; 24:8Kwa hiyo kaburi5:14 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. limeongeza hamu yake

na kupanua mdomo wake bila kikomo,

ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu,

pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote.

155:15 Isa 2:9-11; 10:33Hivyo mwanadamu atashushwa,

na binadamu kunyenyekezwa,

macho ya wenye majivuno yatanyenyekezwa.

165:16 Isa 61:8; Law 10:3; Eze 36:23; Za 97:6; Isa 33:10; 28:17; 30:18; 29:23Lakini Bwana Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa

kwa ajili ya haki yake,

naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe

kuwa mtakatifu kwa haki yake.

175:17 Sef 2:6, 14; Isa 32:14; 7:25; 17:2Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe,

wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri.

185:18 Isa 59:4-8; 5:8; Amo 5:8; Yer 17:5; 23:14; Hos 11:4Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu

na uovu kama kwa kamba za mkokoteni,

195:19 2Pet 3:3-4; Eze 12:22; Yer 17:15; Isa 30:11-12; 29:23; 1:4; 60:22kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka,

aharakishe kazi yake ili tupate kuiona.

Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike,

tena udhihirike ili tupate kuujua.”

205:20 Ay 24:13; Amo 5:7; Mwa 18:25; 1Fal 22:8; Za 94:21; Isa 5:8; Mt 6:22-23; Lk 11:22, 34-35Ole wao wanaoita ubaya ni wema,

na wema ni ubaya,

wawekao giza badala ya nuru,

na nuru badala ya giza,

wawekao uchungu badala ya utamu,

na utamu badala ya uchungu.

215:21 Mit 3:7; Rum 12:16; Isa 47:10; 1Kor 3:18-20Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,

na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe.

225:22 1Sam 25:36; Mit 23:20; Isa 22:13; Mit 31:4; Yer 7:18Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo,

nao walio hodari katika kuchanganya vileo,

235:23 Kut 23:8; Amo 5:12; Yak 5:6; Eze 22:12; Isa 1:17; 29:21; 59:13-15; Za 94:21wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo,

lakini huwanyima haki wasio na hatia.

245:24 2Fal 19:20; Za 107:11; Ay 18:16; Isa 47:14; Ay 24:24; 40:8; 6:10; Isa 1:31; Nah 1:10; 2Fal 19:30Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi,

na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto,

ndivyo mizizi yao itakavyooza

na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi;

kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote

na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.

255:25 2Fal 22:13; Yer 6:12; 2Fal 9:37; Dan 9:16; Ay 40:11; Kut 19:18; Isa 26:11; 10:17; Ay 40:11; Yer 6:12Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake,

mkono wake umeinuliwa na anawapiga.

Milima inatetemeka,

maiti ni kama takataka kwenye barabara.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

265:26 Za 20:5; Isa 7:18; Zek 10:8; Kum 28:4-9; Isa 13:5; 18:2Yeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali,

anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia.

Tazama wamekuja,

kwa kasi na kwa haraka!

275:27 Yoe 2:7-8; Eze 23:15; Isa 22:21; 40:29-31; 14:31; Ay 12:18Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa,

hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala,

hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni,

hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika.

285:28 Ay 39:23; Za 45:6; 7:12; Eze 26:11; Ay 1:19; Za 25:5; 2Fal 2:1Mishale yao ni mikali,

pinde zao zote zimevutwa,

kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume,

magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.

295:29 Isa 42:22; 49:24-25; 2Fal 17:25; Mik 5:8; Yer 51:38; Zek 11:3; Sef 3:3; Isa 10:6Ngurumo yao ni kama ile ya simba,

wananguruma kama wana simba,

wanakoroma wanapokamata mawindo yao,

na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.

305:30 Yer 4:23-28; Za 93:3; Yoe 2:10; Isa 2:1; 2:11; 50:3; Yer 50:42; Ay 21:30; Lk 21:25; 1Sam 2:9; Za 18:28Katika siku ile watanguruma juu yake

kama ngurumo za bahari.

Kama mtu akiitazama nchi,

ataona giza na dhiki;

hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以赛亚书 5:1-30

葡萄园之歌

1我要为我所爱的歌唱,唱一首有关他葡萄园的歌:

我所爱的在肥美的山冈上有一个葡萄园。

2他松土,清除石头,

栽种了上好的葡萄,

在园中建了一座瞭望塔,

凿了榨酒池。

他期望收获好葡萄,

得到的却是坏葡萄。

3他说,“耶路撒冷犹大的居民啊,

请你们在我和葡萄园之间评评理。

4我不遗余力地料理葡萄园,

希望得到好葡萄,

为什么得到的只是坏葡萄呢?

5“现在,我告诉你们我会怎样处理这葡萄园,

我要除去篱笆,任它被毁坏;

我要拆毁围墙,任它被践踏。

6我不再修剪,不再锄地,

也不再降雨,

任由它荒废,长满荆棘和蒺藜。”

7万军之耶和华的葡萄园就是以色列

祂所喜爱的葡萄树就是犹大人。

祂希望看到公平,

却只看见杀戮;

指望看到公义,

却只听见冤声。

以色列的罪恶

8那些不断建房置田、占光土地、

独居其中的人有祸了!

9我亲耳听到万军之耶和华说:

“许多富丽堂皇的房屋必荒废,无人居住。

10三十亩葡萄园只产二十升酒,

二百公斤种子只产二十公斤粮食。”

11那些从清早到深夜贪杯好酒,

喝到酩酊大醉的人有祸了!

12席上,他们在琴、瑟、鼓、笛声中饮酒作乐,

却毫不理会耶和华的作为。

13所以,我的子民必因无知而被掳。

他们的贵族无饼充饥,

民众无水解渴。

14阴间必食欲膨胀,

张开大口吞噬耶路撒冷的首领、群众和宴乐之人。

15世人遭贬,降为卑下,

狂妄者眼目低垂。

16唯有万军之耶和华因祂的公正而受尊崇,

圣洁的上帝借公义彰显自己的圣洁。

17那时,羊群在那里吃草,

如在自己的草场,

寄居者在富人的荒场上进食。

18那些用虚假作绳子扯来罪恶,

用套绳拉来邪恶的人有祸了!

19他们说:“让上帝快点完成祂的工作,

好让我们看看;

以色列的圣者早点实现祂的计划,

好让我们知道。”

20那些善恶不分、黑白颠倒、

甜苦不辨的人有祸了!

21那些自以为聪明、睿智的人有祸了!

22那些以豪饮称霸、善于调酒的人有祸了!

23他们贪赃枉法,坑害无辜。

24他们的根必朽烂,

花朵如飞尘飘落,

就像火焰吞灭禾秸,烧尽干草,

因为他们厌弃以色列之圣者的训诲,

藐视万军之耶和华的言语。

25耶和华向祂的子民发怒,

伸手击打他们。

山岭震动,

他们横尸街头,犹如粪土。

然而,祂的怒气还没有止息,

祂降罚的手没有收回。

26祂必竖起旗帜召集远方的国家,

吹哨叫来地极的人。

看啊,他们必飞速而来!

27他们无人疲倦,无人踉跄,

无人打盹,无人睡觉,

都腰带紧束,鞋带未断。

28他们的利箭上弦,引弓待发;

他们的马蹄坚如岩石,

车轮快如旋风。

29他们吼叫如狮子,

像猛狮般咆哮着捕食,

将猎物叼走,无人能救。

30那日,他们必向以色列咆哮,

如怒海澎湃。

人若观看大地,

只见黑暗和艰难,

光明被密云遮盖。