112:1 Mwa 41:6; Eze 17:10; 2Fal 17:4; Za 78:67; Hos 4:19; 5:13Efraimu anajilisha upepo;
hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima
na kuzidisha uongo na jeuri.
Anafanya mkataba na Ashuru
na kutuma mafuta ya zeituni Misri.
212:2 Ay 10:212:2 Mik 6:2; Hos 4:9; 9:15; Kut 32:34; Amo 2:4Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,
atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake
na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.
312:3 Mwa 25:26; 32:24-29Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;
kama mwanadamu, alishindana na Mungu.
412:4 Mwa 12:8; 28:12-15; 35:15Alishindana na malaika na kumshinda;
alilia na kuomba upendeleo wake.
Alimkuta huko Betheli
na kuzungumza naye huko:
512:5 Kut 3:15Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,
Bwana ndilo jina lake!
612:6 Mik 6:8; 7:7; Za 106:13; Eze 18:30; Isa 19:22; Yoe 2:12; Yer 22:3Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;
dumisha upendo na haki,
nawe umngojee Mungu wako siku zote.
712:7 Law 19:26; Amo 8:5Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;
hupenda kupunja.
812:8 Za 62:10; Ufu 3:17; Eze 28:5Efraimu hujisifu akisema,
“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.
Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu
uovu wowote au dhambi.”
912:9 Law 23:43; Hos 2:15; Neh 8:17“Mimi ndimi Bwana Mungu wenu
niliyewaleta kutoka Misri;
nitawafanya mkae tena kwenye mahema,
kama vile katika siku
za sikukuu zenu zilizoamriwa.
1012:10 Amu 14:12; Eze 20:49; 2Fal 17:13; Yer 7:25Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi
na kusema mifano kupitia wao.”
1112:11 Amo 4:4; Hos 4:15; 6:8; 8:11Je, Gileadi si mwovu?
Watu wake hawafai kitu!
Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?
Madhabahu zao zitakuwa
kama malundo ya mawe
katika shamba lililolimwa.
1212:12 Mwa 28:5; 29:18Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;
Israeli alitumika ili apate mke,
ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.
1312:13 Kut 14:19-22; Isa 63:11-14; Kut 13:3; Hos 11:1Bwana alimtumia nabii
kumpandisha Israeli kutoka Misri,
kwa njia ya nabii alimtunza.
1412:14 Eze 18:13; Dan 11:18Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;
Bwana wake ataleta juu yake
hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza
kwa ajili ya dharau yake.
1「以法蓮以風為食,
整天追逐東風,
虛謊和暴力日益增多;
他跟亞述結盟,
向埃及進貢橄欖油。」
2耶和華指控猶大;
要按雅各所行的懲罰他,
照雅各所做的報應他。
3雅各在母胎之中曾抓住哥哥的腳跟,
壯年之時曾跟上帝角力。
4他跟天使角力得勝,
向天使哭求福分。
他在伯特利遇見祂,
在那裡與祂說話——
5就是萬軍之上帝耶和華,
耶和華是祂的名。
6所以,你們要歸向你們的上帝,
持守仁愛和公義,常常等候祂。
7以法蓮是個不誠實的商人,
手裡拿著騙人的秤,喜歡壓榨人。
8以法蓮說:「我發財了,
我依靠自己致富。
沒有人能從我的勞碌中找出過錯和罪惡。」
9耶和華說:
「從你們在埃及的時候,
我就是你們的上帝耶和華。
我要使你們再次住在帳篷裡,
就像從前守節期時一樣。
10我曾對先知講話,賜給他們許多異象,
藉他們用比喻警告你們。」
11基列人充滿罪惡,終必滅亡。
他們在吉甲用公牛獻祭,
他們的祭壇像田間犁溝裡的石堆。
12雅各曾逃往亞蘭,
以色列在那裡為娶妻而服侍人,
為得到妻子而替人牧羊。
13耶和華藉著先知帶領以色列離開埃及,
也藉著先知保護他。
14但以法蓮卻極大地觸怒耶和華,
所以他的主要讓他血債血還,
以羞辱還羞辱。