Ezekieli 48 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 48:1-35

Mgawanyo Wa Nchi

148:1 Mwa 30:6; Hes 34:7-9; Eze 47:15-20“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

248:2 Yos 19:24-31“Asheri atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi.

348:3 Yos 19:32-39“Naftali atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi.

448:4 Yos 17:1-11“Manase atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi.

548:5 Yos 16:5-9; 17:7-10, 17“Efraimu atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi.

648:6 Yos 13:15-21“Reubeni atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi.

748:7 Yos 15:1-63“Yuda atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.

848:8 Eze 45:1; 48:21“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa 25,00048:8 Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25. na urefu wake kuanzia mashariki mpaka magharibi utakuwa ule ule wa sehemu moja ya kabila, mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.

948:9 Eze 45:1“Hiyo sehemu maalum mtakayotoa kwa Bwana itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,00048:9 Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5. 1048:10 Eze 45:1-4Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Bwana. 1148:11 2Sam 8:17; Law 8:35; Eze 14:11; 44:15; Yer 23:11; Neh 9:34Hii itakuwa kwa ajili ya makuhani waliowekwa wakfu, Wasadoki, waliokuwa waaminifu katika kunitumikia nao hawakupotoka kama Walawi walivyofanya wakati Waisraeli walipopotoka. 12Itakuwa toleo maalum kwao kutoka sehemu takatifu ya nchi, yaani, sehemu takatifu sana, inayopakana na nchi ya Walawi.

1348:13 Eze 45:5“Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. 1448:14 Law 25:34; 27:10, 28Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana.

1548:15 Kum 20:5; Eze 42:20; 44:23; 45:6“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,00048:15 Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25. na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 1648:16 Ufu 21:16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,48:16 Dhiraa 4,500 ni sawa na kilomita 2.025. upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. 17Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 25048:17 Dhiraa 250 ni sawa na sentimita 112.5. upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi. 1848:18 Eze 21:16Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula. 1948:19 Eze 45:6; Ufu 7:5Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli. 2048:20 Hes 24:5; Isa 33:20; Ufu 21:16Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani, dhiraa 25,000 kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.

2148:21 Eze 45:7; Yos 18:1; Yn 12:32; Rum 15:9-12“Eneo linalobaki pande zote za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu atawalaye. Eneo hili litaenea upande wa mashariki kuanzia kwenye dhiraa 25,000 za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki na kuelekea upande wa magharibi kuanzia kwenye dhiraa 25,000 hadi mpaka wa magharibi. Maeneo yote haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake. 22Kwa hiyo milki ya Walawi na milki ya mji vitakuwa katikati ya eneo lile ambalo ni mali ya mkuu anayetawala. Eneo la mkuu anayetawala litakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini.

2348:23 Yos 18:11-28“Kuhusu makabila yaliyobaki: Benyamini atakuwa na sehemu moja, itakayoanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

2448:24 Mwa 29:33; Yos 19:1-9“Simeoni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Benyamini kuanzia mashariki hadi magharibi.

2548:25 Yos 19:17-23“Isakari atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Simeoni kuanzia mashariki hadi magharibi.

2648:26 Yos 13:24-28“Zabuloni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Isakari kuanzia mashariki hadi magharibi.

2748:27 Yos 13:24-28“Gadi atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Zabuloni kuanzia mashariki hadi magharibi.

2848:28 Mwa 14:7; Hes 34:6, 15; Mwa 15:18; Isa 27:12; Eze 47:19“Mpaka wa kusini wa Gadi utapita kusini kuanzia Tamari hadi maji ya Meriba-Kadeshi, kisha kupitia upande wa Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu.48:28 Bahari Kuu hapa ina maana ya Bahari ya Mediterania.

2948:29 Eze 47:14, 21, 22; 45:1“Hii ndiyo nchi mtakayogawanya kuwa urithi kwa makabila ya Israeli, nazo zitakuwa sehemu zao,” asema Bwana Mwenyezi.

Malango Ya Mji

30“Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea: Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu, 3148:31 Ufu 21:12; Isa 60:18malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.

32“Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Yosefu, lango la Benyamini na lango la Dani.

33“Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.

3448:34 2Nya 4:4; Ufu 21:12-13“Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.

3548:35 Za 72:8; Ufu 21:3; Zek 2:10; Amu 6:24; Isa 12:6; 24:23; Yer 31:17“Urefu wote kuzunguka utakuwa dhiraa 18,000.48:35 Dhiraa 18,000 ni sawa na kilomita 8.1.

“Nalo jina la mji huo kuanzia wakati huo na kuendelea litakuwa:

Bwana yupo hapa.”

Japanese Contemporary Bible

エゼキエル書 48:1-35

48

土地の分割

1以下は、各部族と、その土地のリストである。ダンの所有地は、地中海に面する北西の境界線からヘテロン、レボ・ハマテを経て、さらに南はダマスコと、北はハマテと接する境界線上のハツァル・エナンまでである。ダンの地の東と西はそれぞれ境界線が境となっている。 2アシェルの土地は、ダンの南で、東と西はそれぞれの境界線が境となっている。 3ナフタリの土地は、アシェルの南で、東と西はそれぞれの境界線が境となっている。 4マナセの土地は、ナフタリの南で、同じように、東と西はそれぞれ境界線が境となっている。 5-7さらに南へと、エフライム、ルベン、ユダの土地が続き、その東と西は同じように境界線が境となっている。

8ユダの南は神殿のために取っておかれた土地で、その中央に神殿がある。その東と西の境は、各部族の土地の境と同じである。 9この神殿のための土地は、長さ二万五千キュビト、幅二万キュビトである。 10神殿は、東西二万五千キュビト、南北一万キュビトの土地の中央にある。 11この区域は祭司たちのものである。この祭司たちは、イスラエルの民やレビ部族の残りの者たちが罪を犯したとき、わたしに従って罪を犯さなかったツァドクの子孫である。 12この土地は、分割される土地の中の特別の区域で、最も神聖な土地である。それに隣接して、他のレビ部族の住む区域がある。

13その広さは祭司のための区域と同じで、二つ合わせると、長さ二万五千キュビト、幅二万キュビトになる。 14この特別区の買売や交換は厳禁され、ほかの者に使わせてもいけない。それは主のために聖別された地だからである。

15神殿のための特別区域の南にある、長さ二万五千キュビト、幅五千キュビトの細長い地は、一般用のもので、町を中心にして、家や牧場や農園を造るようにしなさい。 16町は四千五百キュビト平方の正方形とする。 17牧場は約二百五十キュビトの幅で、町の回りを囲むようにする。 18聖なる区域に接したこの地域で、町の外にある残りの地は、東西にそれぞれ一万キュビトで、町の住民のための農園である。 19町で働くイスラエル人なら、どの部族の者でもこの農園で働くことができる。 20聖なる区域と町の所有地とを合わせた、この土地全体は二万五千キュビト平方である。

21-22この区域の両側の、イスラエルの東と西の境までの地は君主のものである。ユダとベニヤミンとの土地にはさまれたこの土地は、聖なる区域と町の所有地との両側にあって、幅はそれぞれ二万五千キュビトである。

23残りの部族に分割される土地は、次のとおり。ベニヤミンの土地は、東の境界線から西の境界線まで、イスラエルの全地を横切っている。 24ベニヤミンの土地の南にはシメオンの土地があり、同じように東と西の境界線の間に広がっている。 25イッサカルの土地が、その南に同じようにある。 26さらに、その南にゼブルンの土地が同じようにある。 27-28それから、ガドの土地がその南にあるが、東と西の境界線は同じでも、南の境界線は、タマルからメリバテ・カデシュの泉、さらにエジプト川に沿って地中海に至っている。 29以上が各部族に割り当てられた土地である。」このように、主が語るのです。

新しい町の門

30-31「町の門には、それぞれイスラエルの各部族の名がつけられている。北側の四千五百キュビトの城壁には三つの門があり、ルベンの門、ユダの門、レビの門と名づけられている。 32東側の四千五百キュビトの城壁にも、ヨセフの門、ベニヤミンの門、ダンの門と名づけられた門がある。 33南側の城壁も同じ長さで、シメオンの門、イッサカルの門、ゼブルンの門と呼ばれる三つの門がある。 34西側の四千五百キュビトの城壁にも、ガドの門、アシェルの門、ナフタリの門と呼ばれる三つの門がある。 35町の周囲は一万八千キュビトあり、町の名は『神の都』と呼ばれる。」