Ezekieli 47 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 47:1-23

Mto Kutoka Hekaluni

147:1 Za 46:4; Ufu 22:1; Yoe 3:18; Isa 55:1Yule mtu akanirudisha mpaka kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki). Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kusini wa Hekalu, kusini mwa madhabahu. 247:2 Eze 40:35Ndipo akanitoa nje kupitia lango la kaskazini na kunizungusha mpaka kwenye lango la nje linaloelekea mashariki, nayo maji yalikuwa yakitiririka kutoka upande wa kusini.

347:3 Eze 40:3; Ufu 11:1Mtu yule alipokwenda upande wa mashariki akiwa na kamba ya kupimia mkononi mwake, akapima dhiraa 1,00047:3 Dhiraa 1,000 ni sawa na mita 450. kisha akanipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kwenye vifundo vya miguu. 4Akapima dhiraa 1,000 nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine 1,000 na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni. 547:5 Isa 11:9; Hab 2:14; Mwa 2:10Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka. 647:6 Ufu 22:2; Isa 41:19Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?”

Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto. 747:7 Eze 47:12; Ufu 22:2; Za 1:3; 92:12Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto.

847:8 Ufu 17:15; Yos 3:16; Isa 41:18; Kum 3:17Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba,47:8 Araba hapa ina maana ya Bonde la Yordani. ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari,47:8 Bahari hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi. 947:9 Isa 12:3; Yn 4:14; 1Kor 15:45; Yn 7:37-38Popote mto huu uendapo kila kiumbe hai kinachoyaparamia hayo maji kitaishi, nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yafikapo huko. Maji hayo yatakuwa hai na kila kitu kitakachoishi kule mto uendako. 1047:10 Isa 19:8; Mt 4:19; Yos 15:62; Eze 26:5; Mt 13:47; Hes 34:6Wavuvi watasimama kando ya bahari, kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu huko patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu47:10 Bahari Kuu hapa ina maana ya Bahari ya Mediterania. 1147:11 Kum 29:23Lakini madimbwi yake na mabwawa yake hayatakuwa na maji yanayofaa kunywa, bali yatabakia kuwa maji ya chumvi. 1247:12 Mwa 2:9; Ufu 22:2; Yer 17:8; Ay 18:6; Eze 36:8Miti ya matunda ya kila aina itaota kwenye kingo zote mbili za mto huu. Majani yake hayatanyauka wala haitaacha kuwa na matunda katika matawi yake. Kila mwezi kutakuwa na matunda, kwa sababu maji yatokayo patakatifu yanaitiririkia. Matunda yake yatakuwa chakula na majani yake yatakuwa dawa.”

Mipaka Mipya Ya Nchi

1347:13 Hes 34:2-12; Yer 3:18; Mwa 48:5-16; 49:26Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Hii ndiyo mipaka ambayo kwayo mtagawanya hiyo nchi kuwa urithi miongoni mwa hayo makabila kumi na mawili ya Israeli, pamoja na mafungu mawili ya Yosefu. 1447:14 Kum 1:8; Mwa 12:7; Eze 36:12Mtagawa kwa usawa miongoni mwao. Kwa sababu niliapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu, nchi hii itakuwa urithi wenu.

1547:15 Eze 48:1; Hes 34:2-8“Huu ndio utakuwa mpaka wa hiyo nchi:

“Upande wa kaskazini utaanzia Bahari Kuu kwa njia ya Hethloni kupitia Lebo-Hamathi hadi maingilio ya Sedadi. 1647:16 2Sam 8:8; Hes 13:21; Yer 49:23; Amo 6:2Berotha na Sibraimu (ambao uko kwenye mpaka kati ya Dameski na Hamathi), hadi kufikia Haser-Hatikoni, ambao uko katika mpaka wa Haurani. 1747:17 Hes 34:9; Eze 48:1Hivyo mpaka utaendelea kuanzia Baharini hadi Hasar-Enoni, ukiambaa na mpaka wa kaskazini wa Dameski, pamoja na mpaka wa Hamathi upande wa kaskazini. Huu utakuwa ndio mpaka wa kaskazini.

1847:18 Eze 27:18Upande wa mashariki mpaka utapita kati ya Haurani na Dameski, kuambaa Yordani na kati ya Gileadi na nchi ya Israeli, hadi bahari ya mashariki47:18 Bahari ya mashariki hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. na kufika Tamari. Huu utakuwa ndio mpaka wa mashariki.

1947:19 Mwa 15:18; Kum 32:51; Isa 27:12; Eze 48:28Upande wa kusini utaanzia Tamari hadi kufikia maji ya Meriba-Kadeshi, kisha utaambaa na Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu. Huu utakuwa ndio mpaka wa kusini.

2047:20 Hes 13:21; 34:6; Eze 48:1Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa ndio mpaka wa magharibi.

2147:21 Kum 24:19; Efe 2:19-22; Rum 10:12; Law 24:22; Mal 3:5; Efe 3:6; Isa 56:6-7“Mtagawanya nchi hii miongoni mwenu kufuatana na makabila ya Israeli. 2247:22 Mdo 2:5; Efe 2:19-22; Rum 10:12; Efe 3:6; Ufu 7:9-10; Gal 3:28; Kol 3:11Mtaigawanya kuwa urithi kwa ajili yenu na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwenu na ambao wana watoto. Wao watakuwa kwenu kama wenyeji wazawa wa Israeli, pamoja na ninyi watagawiwa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli. 2347:23 Kum 10:19Katika kabila lolote mgeni atakapoishi hapo ndipo mtakapompatia urithi wake,” asema Bwana Mwenyezi.

Japanese Contemporary Bible

エゼキエル書 47:1-23

47

神殿から流れる川

1それから、その人は私を神殿の入口に連れ戻しました。見ると、神殿の下から東に向かって、水が流れ出ているのです。水は祭壇の右側、すなわち南側を通って流れていました。 2私は北の門を通って塀の外へ連れて行かれ、東の門へと回らされました。見ると、水は東の門の南端を流れていました。

3その人は流れに沿って測りながら東に進み、一千キュビト行ったとき、その流れを渡るように私に命じました。水はくるぶしまでありました。 4さらに一千キュビト行くと、また、渡るように命じられました。今度は、水はひざまでありました。 5それから一千キュビト行くと、水の深さは腰までになりました。さらに一千キュビト先へ行くと、もう泳がなければ渡れないほどの川となっていました。深くて、とても歩いて渡ることはできなかったのです。 6その人は、今見たことをよく脳裏に刻み込んでおくようにと言って、私をその川の岸に沿って連れ帰りました。 7すると驚いたことに、川の両岸にたくさんの木が茂っているではありませんか。

8その人はこう言いました。「この川は東に流れて、砂漠地帯とヨルダン渓谷を通って死海に注いでいる。こうして死海の塩分の多い水を浄化し、新鮮な水に変えるのだ。 9この川の水に触れるものはすべて生き生きとする。魚が住める水に変えられるので、死海にも魚がいっぱいになる。この水が流れ込む所はどこでも、すべてのものが生かされる。 10南はエン・ゲディから北はエン・エグライムに至るまで、死海の沿岸で漁師が漁をするようになる。岸には一面に網が干されるようになる。魚の種類も、地中海の魚と同じくらい豊富になる。 11だが、沼地や湿地は相変わらず塩水のまま残される。 12川岸にはあらゆる種類の果樹が茂り、その葉は枯れず、落ちることもなく、いつも実がなっている。毎月、必ず新しい実がなる。神殿から流れ出る水で潤されているからだ。その実は食物に、葉は薬になる。」

イスラエルの境界

13神である主はこう語ります。「イスラエルの十二の部族に土地を分割するときは、次のようにしなさい。ヨセフ(エフライムとマナセ)の部族には二区分を与えよ。 14他の部族には、それぞれ平等に一区分が与えられる。わたしはあなたがたの先祖に、土地を与えると約束した。今、その土地を受け継ぐのだ。

15北の境界線は、地中海からヘテロンに、さらにレボ・ハマテからツェダデに、 16ダマスコとハマテの境にあるベロタとシブライムを経て、ハウランの境にあるハツェル・ハティコンに至る。 17つまり地中海から、北はハマテと、南はダマスコと接しているハツァル・エナンまでである。 18東の境界線は、ハツァル・エナンからハウラン山へと南下し、そこで西に曲がってガリラヤ湖の南岸から、イスラエルとギルアデとを分けるヨルダン川に沿って死海に下り、さらにタマルに至る。

19南の境界線は、タマルから西に向かってメリバテ・カデシュの泉を通り、エジプト川(ワディ・エル・アリシュ)に沿って地中海に至る。

20西側は地中海が境界線で、南の境界線から北の境界線が始まる所までである。

21これらの境界線の内側を、イスラエルの部族に分割しなければならない。 22その土地をあなたがたと、あなたがたの中に住んでいる外国人の相続地として割り当てるのだ。イスラエルの地で生まれた子どもはみな、たとえ親が外国人でも、イスラエルの市民権が与えられ、あなたがたの子どもと同じ権利を与えられる。 23このような移住者全員に、現在住んでいる部族の間で土地を与えなければならない。