2 Wakorintho 6 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wakorintho 6:1-18

16:1 1Kor 3:9; 2Kor 5:20; 1Kor 15; 2Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 26:2 Isa 49; 8; Za 69:13; Isa 55:6Kwa maana asema:

“Wakati wangu uliokubalika nilikusikia,

siku ya wokovu nilikusaidia.”

Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.

Taabu Za Paulo

36:3 Mt 5:29; Rum 14:13-20; 1Kor 8:9-13; 9:13; 10:32Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama. 46:4 2Kor 4:2; 1Kor 4:1Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida; 56:5 Mdo 16:23; 2Kor 11:23-25; 1Kor 4:11katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga; 66:6 1Kor 2:4; Rum 12:5; 1Tim 1:5; 1The 1:5katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli; 76:7 2Kor 4:2-7; Rum 13:12; 2Kor 10:4; Efe 6:10-18katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; 86:8 1Kor 4:10-13; Mt 27:63katika utukufu na katika kudharauliwa; katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli; 96:9 Rum 8:36; 2Kor 1:8-10; 4:10-11tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi; 106:10 Mt 5:12; 2Kor 7; 4; Flp 2:17; 4:4; Kol 1:24; 1The 1:6; 2Kor 8:9; Mdo 3:6; Rum 8:32tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.

116:11 2Kor 7:3; Za 119:32Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa. 126:12 2Nya 12:15Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu. 136:13 1The 2:11; 2Kor 7:2Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa.

Msifungiwe Nira Pamoja Na Wasioamini

146:14 Mwa 24:3; Kum 22:10; 1Kor 5:9-10; Efe 5:7-11Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 156:15 1Kor 10:21; Mdo 5:14; 1Kor 6; 6Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari?6:15 Beliari hapa ina maana ya uovu, kutokumcha Mungu. Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 166:16 1Kor 10:21; 3:16; Mt 16:16; Law 26:12; Yer 32:38; Eze 37:27; Ufu 21; 3Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

176:17 Ufu 18; 4; Isa 51:11; Eze 20:34-41“Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,

mkatengwe nao,

asema Bwana.

Msiguse kitu chochote kilicho najisi,

nami nitawakaribisha.”

186:18 Kut 4:22; 2Sam 7:14; 1Nya 17:13; Isa 43:6; Rum 8:14; 2Sam 7:8“Mimi nitakuwa Baba kwenu,

nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu,

asema Bwana Mwenyezi.”

King James Version

2 Corinthians 6:1-18

1We then, as workers together with him, beseech you also that ye receive not the grace of God in vain. 2(For he saith, I have heard thee in a time accepted, and in the day of salvation have I succoured thee: behold, now is the accepted time; behold, now is the day of salvation.) 3Giving no offence in any thing, that the ministry be not blamed: 4But in all things approving ourselves as the ministers of God, in much patience, in afflictions, in necessities, in distresses, 5In stripes, in imprisonments, in tumults, in labours, in watchings, in fastings; 6By pureness, by knowledge, by longsuffering, by kindness, by the Holy Ghost, by love unfeigned, 7By the word of truth, by the power of God, by the armour of righteousness on the right hand and on the left, 8By honour and dishonour, by evil report and good report: as deceivers, and yet true; 9As unknown, and yet well known; as dying, and, behold, we live; as chastened, and not killed; 10As sorrowful, yet alway rejoicing; as poor, yet making many rich; as having nothing, and yet possessing all things.

11O ye Corinthians, our mouth is open unto you, our heart is enlarged. 12Ye are not straitened in us, but ye are straitened in your own bowels. 13Now for a recompence in the same, (I speak as unto my children,) be ye also enlarged. 14Be ye not unequally yoked together with unbelievers: for what fellowship hath righteousness with unrighteousness? and what communion hath light with darkness? 15And what concord hath Christ with Belial? or what part hath he that believeth with an infidel? 16And what agreement hath the temple of God with idols? for ye are the temple of the living God; as God hath said, I will dwell in them, and walk in them; and I will be their God, and they shall be my people. 17Wherefore come out from among them, and be ye separate, saith the Lord, and touch not the unclean thing; and I will receive you, 18And will be a Father unto you, and ye shall be my sons and daughters, saith the Lord Almighty.