2 Samweli 15 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 15:1-37

Mipango Ya Hila Ya Absalomu

115:1 2Sam 12:11; 1Sam 8:11; 1Fal 1:5; Mit 11:2; 16:18Baada ya muda, Absalomu akajipatia magari ya vita na farasi pamoja na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake. 215:2 Mwa 23:10; 2Sam 19:8; Mit 1:16Akawa anaamka asubuhi na mapema na kusimama kando ya barabara inayoelekea kwenye lango la mji. Wakati wowote alipokuja mtu yeyote mwenye mashtaka yanayohitaji kuletwa mbele ya mfalme kwa maamuzi, Absalomu naye angemwita na kumuuliza, “Wewe unatoka mji upi?” Naye angejibu, “Mtumishi wako anatoka katika mojawapo ya makabila ya Israeli.” 315:3 Mit 12:2Kisha Absalomu angemwambia, “Tazama, malalamiko yako ni ya haki na sawasawa, lakini hakuna mwakilishi wa mfalme wa kukusikiliza.” 415:4 Rum 16:18; Amu 9:29Absalomu aliongeza, “Laiti tu ningeteuliwa kuwa mwamuzi katika nchi. Ndipo kila mmoja mwenye mashtaka au shauri angekuja kwangu nami ningeona kwamba anapata haki.”

515:5 Za 12:2Pia, wakati mtu yeyote alipomkaribia ili kusujudu mbele yake, Absalomu alinyoosha mkono wake na kumshika pia kumbusu. 615:6 2Sam 3:3; Mwa 28:20; 2Sam 13:37-38; Rum 16:18Absalomu akaendelea na tabia hii mbele ya Waisraeli wote waliomjia mfalme kumwomba awape haki; kwa hiyo Absalomu akaiba mioyo ya watu wa Israeli.

715:7 2Sam 2:1Mnamo mwisho wa mwaka wa nne, Absalomu akamwambia mfalme, “Naomba unipe ruhusa niende Hebroni nikatimize nadhiri niliyomwekea Bwana. 815:8 1Fal 1:34, 39; 2Fal 9:13; 1Sam 16:2; Mwa 28:20; 1Sam 1:11; Za 56:12; 2Sam 13:38Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu Bwana huko Hebroni.’ ”

9Mfalme akamwambia, “Enenda kwa amani.” Hivyo akaenda Hebroni.

1015:10 1Fal 1:34, 39; 2Fal 9:13Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ” 1115:11 1Sam 9:13; 16:3-5; Mwa 20:5; Mit 14:15; Mt 10:16; Rum 16:18-19Watu mia mbili kutoka Yerusalemu walikuwa wamefuatana na Absalomu. Walikuwa wamealikwa kama wageni nao walikwenda kwa nia njema, pasipo kujua lolote. 1215:12 2Sam 16:15, 23; 17:14; 23:34; 1Nya 27:33; Ay 19:14; Za 41:9; 55:13; Yer 9:4; Yos 15:51; Za 3:1; Mik 7:5-6Wakati Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli, Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.

Kukimbia Kwa Daudi

1315:13 Amu 9:3Mjumbe akaja na kumwambia Daudi, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”

1415:14 1Fal 2:26; Za 132:1; 3; 2Sam 16:9Ndipo Daudi akawaambia maafisa wake wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Njooni! Ni lazima tukimbie, la sivyo hakuna hata mmoja wetu atakayeokoka kutoka mkononi mwa Absalomu. Ni lazima tuondoke kwa haraka, la sivyo atakuja mbio na kutupata, atatuangamiza na kuupiga mji kwa upanga.”

15Maafisa wa mfalme wakamjibu, “Watumishi wako tu tayari kufanya lolote mfalme bwana wetu analochagua.”

1615:16 2Sam 16:21-22; 20:3; 12:11Mfalme akatoka, pamoja na watu wa nyumbani mwake wakimfuata; lakini akawaacha masuria kumi ili kuangalia jumba la kifalme. 17Hivyo mfalme akaondoka, pamoja na watu wote wakimfuata, wakatua mahali mbali kiasi. 1815:18 1Sam 30:14; 2Sam 20:7, 23; 1Fal 1:34, 44; 1Nya 18:17; 2Sam 8:18Watu wake wote wakatembea, wakampita wakiwa wamefuatana na Wakerethi na Wapelethi wote; pia Wagiti wote mia sita waliokuwa wamefuatana naye kutoka Gathi wakapita mbele ya mfalme.

1915:19 2Sam 18:2; Mwa 31:15Mfalme akamwambia Itai, Mgiti, “Kwa nini ufuatane na sisi? Rudi ukakae pamoja na Mfalme Absalomu. Wewe ni mgeni, mkimbizi kutoka nchini mwako. 2015:20 1Sam 22:2; 2:6; 23:13Ulikuja jana tu. Nami leo nikufanye utangetange pamoja nasi, wakati sijui niendako? Rudi, nawe ukawachukue watu wa kwenu. Wema na uaminifu na viwe pamoja nawe.”

2115:21 Rut 1:16-17; Mit 17:17; 1Sam 20:3; 2Fal 2:2-6Lakini Itai akamjibu mfalme, “Hakika kama Bwana aishivyo na kama mfalme bwana wangu aishivyo, popote mfalme bwana wangu atakapokuwa, ikiwa ni kuishi au kufa, hapo ndipo mtumishi wako atakapokuwa.”

22Daudi akamwambia Itai, “Songa mbele, endelea.” Kwa hiyo Itai, Mgiti, akaendelea pamoja na watu wake wote, pia jamaa zote waliokuwa pamoja naye.

2315:23 1Sam 11:4; Ay 2:12; 1Fal 2:37; 2Fal 23:12; 2Nya 15:16; 29:16; 30:14; Yer 31:40; Yn 18:1; 2Sam 16:2; Mt 3:1-3Watu wote wa nje ya mji wakalia kwa sauti wakati watu wote walipokuwa wakipita. Mfalme naye akavuka Bonde la Kidroni, nao watu wote wakaelekea jangwani.

2415:24 2Sam 8:17; 19:11; Hes 4:18; 10:33; 1Fal 2:26; 1Sam 22:20Sadoki pia alikuwako, kadhalika Walawi wote waliokuwa pamoja naye walikuwa wamechukua Sanduku la Agano la Mungu. Wakaweka chini Sanduku la Mungu, naye Abiathari akatoa dhabihu mpaka watu wote walipokuwa wameondoka mjini.

2515:25 Kut 15:13; Law 15:31; Za 43:3; 46:4; 84:1; 132:7; 2Sam 6:17Kisha mfalme akamwambia Sadoki, “Rudisha Sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitapata kibali mbele za Bwana, atanirudisha, nami nitaliona Sanduku hili tena pamoja na Maskani yake. 2615:26 Amu 10:15; 2Sam 22:20; 1Fal 10:9; Hes 14:8; 2Nya 9:8; Isa 62:4; 1Sam 3:18Lakini kama yeye atasema, ‘Mimi sipendezwi nawe,’ basi mimi niko tayari; yeye na anifanye chochote aonacho chema kwake.”

2715:27 1Sam 9:9; 2Sam 17:17; 1Fal 1:42; 2Sam 24:11Pia mfalme alimwambia kuhani Sadoki, “Je, wewe si mwonaji? Rudi mjini kwa amani pamoja na mwanao Ahimaasi na Yonathani mwana wa Abiathari. Wewe na Abiathari wachukueni wana wenu wawili. 2815:28 2Sam 17:16Nitasubiri kwenye vivuko katika jangwa mpaka neno litakapotoka kwenu kuniarifu.” 29Kwa hiyo Sadoki na Abiathari wakarudisha Sanduku la Mungu mpaka Yerusalemu na kukaa huko.

3015:30 Hes 25:6; Za 30:5; Es 6:12; Isa 20:2-4; Zek 14:4; Mt 21:1; Lk 19:20; Mdo 1:12; Yer 14:3; Za 126:6; Mt 5:4; Rum 12:15Bali Daudi akaendelea, akapanda Mlima wa Mizeituni, akaenda huku analia, akiwa amefunika kichwa chake na bila viatu miguuni. Watu wote waliokuwa pamoja naye nao wakafunika vichwa vyao, wakawa wanapanda mlima huku wanalia. 3115:31 2Sam 16:23; 17:14, 23; Za 3:1; 55:12Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”

3215:32 2Sam 16:16; 17:5; 1Fal 4:16; Yos 16:2; 7:6; 2Sam 1:2Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwariki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake. 3315:33 2Sam 19:35Daudi akamwambia, “Kama ukienda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu. 3415:34 2Sam 16:19; 17:14; Mit 11:14Lakini ikiwa utarudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga shauri la Ahithofeli. 3515:35 2Sam 17:15-16Je, makuhani Sadoki na Abiathari hawatakuwa pamoja nawe? Waambie lolote utakalosikia katika jumba la mfalme. 3615:36 2Sam 18:19; 17:17; 1Fal 1:42Wana wao wawili, Ahimaasi mwana wa Sadoki na Yonathani mwana wa Abiathari, wako pamoja nao huko. Watume kwangu na lolote utakalosikia.”

3715:37 1Nya 27:33; 2Sam 16:15-17; Mit 17:17Kwa hiyo Hushai, rafiki wa Daudi, akafika Yerusalemu wakati Absalomu alipokuwa anaingia mjini.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记下 15:1-37

押沙龙谋反

1后来,押沙龙为自己备了车马,又派五十个人在他前面开道。 2他常常清早起来,站在城门的通道旁边。每当有人来找王审理争讼时,押沙龙便问他是从哪一座城来的,那人就会报上自己所属的支派。 3押沙龙会对他说:“你的申诉合情合理,可惜王没有派人来听你申诉。” 4他接着会说:“要是我被立为国中的审判官就好了!那样,任何人有申诉都可以来找我,我一定会为他主持公道。” 5每当有人要向他叩拜,他都伸手扶他,亲吻他。 6押沙龙这样对待每一个来向王申诉的以色列人,赢得了民心。

7过了四年,押沙龙对王说:“请让我到希伯仑去还我向耶和华许下的愿吧。 8仆人住在亚兰基述时曾许愿,如果耶和华带领我回到耶路撒冷,我必在希伯仑敬拜祂。” 9王说:“你平安地去吧!”押沙龙就去了希伯仑10他派密使通知以色列各支派一听见号角的响声,便喊:“押沙龙希伯仑做王了!” 11有二百人应邀随同押沙龙一起从耶路撒冷希伯仑,他们对内情一无所知。 12押沙龙献祭的时候,还派人去把大卫的谋士亚希多弗从他的故乡基罗请来。反叛的势力大增,拥护押沙龙的民众越来越多。

大卫逃离耶路撒冷

13有人来禀告大卫:“以色列的民心都归向押沙龙了。” 14大卫便对在耶路撒冷跟随他的臣仆说:“我们赶快逃命吧!否则,我们都难逃押沙龙的追捕。我们要马上离开!免得他赶到残害我们,屠杀全城。” 15臣仆对王说:“臣等谨遵我主我王的决定。” 16于是王就带着全家逃命,只留下十个妃嫔看守宫殿。

17大卫王带着众民离开耶路撒冷,走到最后的那座房子时,停了下来。 18跟随他的人都走到前面去了,包括基利提人、比利提人以及从迦特来跟随他的六百人。 19王问迦特以太说:“你为什么要跟我们一起逃难呢?回去留在新王那里吧!你是流亡到这里的外族人。 20你刚来不久,我怎么可以叫你跟我们一同四处飘流呢?我甚至不知道往何处去。你还是和你的弟兄回去吧,愿耶和华以慈爱和信实待你!” 21以太却答道:“我凭永活的耶和华和我主我王的性命起誓,不管我王去哪里,仆人都要誓死追随到底!” 22大卫便对以太说:“那就继续前行吧!”于是,迦特以太带着他的人及所有的家眷继续前行。 23众人离开时,百姓都放声大哭。王带着所有的人过了汲沦溪,向旷野走去。

24祭司撒督亚比亚他和抬上帝约柜的利未人都来了,他们把约柜放下,让城里出来的人先走过去。 25王对撒督说:“你把上帝的约柜运回城去吧。倘若耶和华恩待我,祂必使我重返家园,重见约柜和会幕; 26但如果我使祂不悦,我也甘愿听凭祂的处置。 27你是个有先见之明的人,安心带着你的儿子亚希玛斯亚比亚他的儿子约拿单回城吧。 28我会在旷野渡口那里等你们的消息。” 29于是,撒督亚比亚他便把上帝的约柜抬回耶路撒冷,留了下来。

30大卫蒙着头,赤着脚登上橄榄山,边走边哭,他的随从也蒙着头,哭着走上山。 31有人告诉大卫亚希多弗也叛变,投奔了押沙龙大卫就祷告说:“耶和华啊,求你使亚希多弗的谋算都变得愚不可及。” 32大卫来到山顶敬拜上帝的地方,看见亚基户筛撕破了衣服,头蒙灰尘前来迎接他。 33大卫对他说:“你跟我一同逃命,只会给我带来不便。 34你还是回到城中,告诉押沙龙你愿意做他的臣仆,就像以前做我的臣仆一样,这样你就可以帮我破坏亚希多弗的计谋。 35祭司撒督亚比亚他都在那里,你在宫内听到什么消息就告诉他们。 36撒督的儿子亚希玛斯亚比亚他的儿子约拿单也在那里,你听到什么消息,可以派他们传信给我。” 37于是,大卫的朋友户筛便回到城里。那时,押沙龙也进了耶路撒冷