1 Samweli 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 1:1-28

Kuzaliwa Kwa Samweli

11:1 Mwa 18:25; 1Sam 9:5; Yos 17:17-18; 21:20-22; 1Nya 6:27-34; Rut 1:2Kulikuwepo na mtu mmoja kutoka Rama, Msufi kutoka nchi ya vilima vya Efraimu, ambaye jina lake aliitwa Elikana mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu. 21:2 Mwa 4:19; Kum 21:15-17Alikuwa na wake wawili, mmoja aliitwa Hana na mwingine Penina. Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na mtoto.

31:3 Kut 23:14; 1Sam 2:19; 20:6; Lk 2:41; Kum 12:5-7; 1Sam 2:31; 14:3; Yos 18:1; Amu 18:31; Za 78:60; Yer 7:12-14Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote huko Shilo, ambapo Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa makuhani wa Bwana. 41:4 Law 7:15-18; Kum 12:17-18; Mwa 29:34Kila mara ilipofika siku ya Elikana kutoa dhabihu, aliwapa mafungu Penina mkewe na wanawe wote pamoja na binti zake. 51:5 Mwa 37:3; 11:30; 29:31Lakini alimpa Hana fungu maradufu kwa sababu alimpenda, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. 61:6 Mwa 16:4-5Kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake alikuwa anamchokoza ili kumuudhi. 71:7 2Sam 12:17; Za 102:4; Kut 23:14; Kum 16:16; Kut 23:14Hili liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda katika nyumba ya Bwana, mke mwenzake alikuwa akimkasirisha mpaka analia na kushindwa kula. 81:8 Rut 4:15Elikana mumewe akawa anamwambia, “Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je, mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?”

91:9 1Sam 3:3Siku moja walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alisimama. Wakati huo kuhani Eli alikuwa ameketi kwenye kiti pembeni mwa mwimo wa mlango wa Hekalu la Bwana. 101:10 Ay 3:20; 7:11; 10:1; 21:25; 23:2; 27:2; Isa 38:15; Yer 20:18Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 111:11 Amu 11:30; 13:7; 13:5; Lk 1:15; Mwa 17:1; 8:1; Za 24:10; 46:7; Isa 1:9; Hes 6:1-21; 21:2; 30:3-8; Mhu 5:4; Mwa 29:32; Kut 4:31Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.”

12Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake. 13Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa 14naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.”

151:15 2Fal 4:27; Za 42:4; 62:8; Mao 2:19Hana akajibu, “Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Bwana. 161:16 Za 55:2; 2Kor 6:15Usimdhanie mtumishi wako kuwa mwanamke mwovu; nimekuwa nikiomba hapa katika wingi wa uchungu mkuu na huzuni.”

171:17 Hes 6:26; 1Sam 20:42; 2Fal 5:19; Mdo 15:33; Mwa 25:21; Za 20:3-5; Mwa 33:15; Yn 16:24Eli akamjibu, “Nenda kwa amani, naye Mungu wa Israeli na akujalie kile ulichomwomba.”

181:18 Mwa 18:3; Rut 2:13; Rum 15:13; Ufu 2:13; Mhu 9:7Hana akasema, “Mtumishi wako na apate kibali machoni pako.” Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.

191:19 Yos 18:25; Mwa 8; 1; 29:31Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za Bwana na kisha wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye Bwana akamkumbuka. 201:20 Mwa 17:19; 29:32; 30:6; Kut 2:10; Mt 1:21; 1Sam 7:5; 12:23; 1Nya 6:27; Yer 15:1; Ebr 11:32Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa kuwa nilimwomba kwa Bwana.”

Hana Anamweka Samweli Wakfu

211:21 Mwa 28:20; Hes 30:2; Kum 12:11Wakati huyo mtu Elikana alipanda pamoja na jamaa yake yote kutoa dhabihu ya mwaka kwa Bwana na kutimiza nadhiri yake, 221:22 Lk 2:22; Kut 13:2; 1Sam 2:11; 3:1Hana hakwenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za Bwana, naye ataishi huko wakati wote.”

231:23 Mwa 25:21; 21:8; Hes 30:7; 2Sam 7:25Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, Bwana na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.

241:24 Hes 15:8-10Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga1:24 Efa moja ya unga ni sawa na kilo 22. na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo. 25Walipokwisha kumchinja yule fahali, wakamleta mtoto kwa Eli, 26naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana. 271:27 1Sam 2:20; Za 66:19-20; Mit 7:7Niliomba mtoto huyu, naye Bwana amenijalia kile nilichomwomba. 281:28 Amu 13:7; Mwa 24:26, 52Hivyo sasa ninamtoa kwa Bwana. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Bwana.” Naye akamwabudu Bwana huko.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

撒母耳记上 1:1-28

撒母耳的出生

1有一个以法莲人名叫以利加拿,住在以法莲山区的拉玛·琐非城。他是苏弗的玄孙、托户的曾孙、以利户的孙子、耶罗罕的儿子。 2他有两个妻子,一个叫哈娜,一个叫毗尼娜毗尼娜有儿有女,哈娜却无儿无女。

3以利加拿每年都从家乡到示罗去敬拜万军之耶和华,献上祭物。当时以利的两个儿子何弗尼非尼哈在那里做耶和华的祭司。 4每当献完祭后,以利加拿就会把祭肉分给毗尼娜和她的儿女。 5但他会给哈娜双份祭肉,因为他爱哈娜,虽然耶和华使她不能生育。 6毗尼娜见她不能生育,便常常羞辱她、气她。 7每年来到耶和华的殿时,毗尼娜总是惹她伤心哭泣,以致她吃不下饭。 8她的丈夫以利加拿对她说:“哈娜,你为什么哭?为什么不吃饭?为什么心里难过?有我不是比有十个儿子更好吗?”

9一天,他们在示罗吃完饭后,哈娜起来祷告。当时,祭司以利正坐在耶和华殿门口的座位上。 10哈娜心中愁苦,一边祷告一边伤心地哭泣。 11她向上帝许愿说:“万军之耶和华啊,如果你眷顾婢女的痛苦,不忘记婢女,赐给婢女一个儿子,我必让他终生事奉你,永不剃他的头1:11 参见民数记6章。。” 12哈娜在耶和华面前祷告,以利注视着她的嘴唇。 13哈娜在心中默祷,只动嘴唇,不出声音,以利以为她喝醉了, 14便对她说:“你要醉到什么时候呢?醒醒酒吧!” 15哈娜答道:“我主啊,我没有喝醉,我淡酒和烈酒都没有喝。我是心里非常愁苦,在耶和华面前倾诉心事。 16请不要以为我是堕落的女人,我心中非常悲伤痛苦,所以一直在祷告。” 17以利说:“你安心地回去吧,愿以色列的上帝答应你的祈求。” 18哈娜说:“谢谢你恩待婢女。”于是,她就去吃饭,不再愁容满面了。

19第二天,以利加拿一家清早起来敬拜耶和华,然后回到自己的家乡拉玛以利加拿哈娜同房,耶和华顾念哈娜20使她怀孕。她后来生了一个儿子,给孩子取名叫撒母耳,因为她说:“他是我向耶和华求来的。”

21第二年,以利加拿带全家人前往示罗,向耶和华献年祭并还所许的愿。 22哈娜没有跟他们同去,她告诉丈夫说:“孩子断奶以后,我会把他带去献给耶和华,让他永远住在那里。” 23以利加拿说:“就依你的意思吧。愿耶和华成就祂的应许。”于是,她就留在家中哺养孩子,直到孩子断奶。 24孩子断奶以后,她就把他带到示罗耶和华的殿,并带去三头公牛、十公斤面粉和一袋酒。 25他们宰了一头公牛后,就把孩子带到以利面前。 26哈娜说:“我主啊,我敢在你面前起誓,我就是那一次站在你这里向耶和华祈求的妇人。 27我求耶和华赐给我一个孩子,祂应允了我的祈求。 28现在,我将他献给耶和华,让他终身事奉耶和华。”

他便在那里敬拜耶和华。