1 Samweli 9 – NEN & BPH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 9:1-27

Samweli Anamtia Sauli Mafuta

19:1 Yos 18:11-20; Rut 2:1; 1Sam 14:51; 1Nya 8:33; 9:39; Es 2:5; Mdo 13:21Kulikuwako Mbenyamini mmoja, mtu maarufu, ambaye aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia wa Benyamini. 29:2 Mwa 39:6; 1Sam 10:23-24Alikuwa na mwana aliyeitwa Sauli, kijana anayevutia sana, hakuwepo aliyelingana naye miongoni mwa Waisraeli, alikuwa mrefu kuliko wengine wote.

39:3 1Sam 10:14-16Basi punda wa Kishi baba yake Sauli walipotea, naye Kishi akamwambia mwanawe Sauli, “Mchukue mmoja wa watumishi mwende pamoja naye kuwatafuta punda.” 49:4 Yos 24:33; 2Fal 4:42; 1Sam 10:2Hivyo akapita katika nchi ya vilima ya Efraimu na katika eneo la Shalisha, lakini hawakuwapata. Wakaendelea katika sehemu ya Shaalimu, lakini punda hawakuwepo huko. Kisha wakapita katika nchi ya Benyamini, lakini hawakuwapata.

59:5 1Sam 1:1; 10:1Walipofika sehemu ya Sufu, Sauli akamwambia mtumishi aliyekuwa pamoja naye, “Njoo, sisi na turudi, au baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda na kuanza kufadhaika kutuhusu sisi.”

69:6 Kum 33:1; Amu 13:6; 1Sam 3:19; 1Fal 13:1; 2Fal 6:6; 1Tim 6:11; 1Sam 3:19; Isa 44:26; Mt 24:35Lakini mtumishi akajibu, “Tazama, katika mji huu yupo mtu wa Mungu, anayeheshimiwa sana na kila kitu asemacho hutokea kweli. Sasa na twende huko. Huenda atatuambia twende njia ipi.”

79:7 Mwa 32:20; 1Fal 13:7; 14:3; 2Fal 4:42; 5:5, 15; Yer 40:5; Amu 6:18; 13:17Sauli akamwambia mtumishi wake, “Kama tukienda, tutampa nini huyo mtu? Chakula kimekwisha kwenye mifuko yetu. Hatuna zawadi ya kumpelekea huyo mtu wa Mungu. Je tuna nini?”

8Mtumishi akamjibu Sauli tena, akasema, “Tazama, nina fedha robo shekeli.9:8 Robo shekeli ni sawa na gramu 3. Hiyo nitampa huyo mtu wa Mungu ili aweze kutuambia twende kwa njia ipi.” 99:9 Mwa 25:22; 2Sam 15:27; 24:11; 17:13; 1Nya 9:22; 21:9; 26:28; 29:29; 2Nya 19:2; Isa 29:10; 30:10; Amo 7:12; Kut 28:30; Hes 27:21; Amu 1:1; 20:18-28; 2Sam 24:11; 2Fal 17:13(Zamani katika Israeli, kama mtu alikwenda kuuliza neno kwa Mungu, angalisema, “Njoo na twende kwa mwonaji,” kwa sababu nabii wa sasa alikuwa akiitwa mwonaji.)

10Sauli akamwambia mtumishi wake, “Vyema, njoo na twende.” Basi wakaenda mjini alipokuwepo huyo mtu wa Mungu.

119:11 Mwa 24:11-13; Kut 2:16Walipokuwa wakipanda mlima kwenda mjini, wakakutana na baadhi ya wasichana wanakuja kuchota maji, nao wakawauliza, “Je, mwonaji yuko?”

129:12 Hes 28:11-15; 1Sam 7:17; Law 26:30; 1Fal 3:2Wakajibu, “Yuko, yu mbele yenu amewatangulia, sasa fanyeni haraka, ndiyo tu amekuja mjini kwetu leo, kwa kuwa watu wana dhabihu huko mahali pa juu. 139:13 Mt 14:19; 1Kor 10:16; 1Tim 4:3-5Mara tu mwingiapo mjini, mtamkuta kabla hajapanda kwenda mahali pa juu kula. Watu hawataanza kula mpaka atakapofika kwa sababu ni lazima kwanza yeye abariki dhabihu, ndipo wale walioalikwa watakapokula. Pandeni sasa, mtamkuta kwa wakati huu.”

14Wakapanda mjini, nao walipokuwa wakiingia mjini, tazama, Samweli alikuwa akija kuelekea walikokwenda mahali pa juu.

159:15 1Sam 24:11; Za 25:14; Mk 11:2-4; Mdo 13:11Basi siku moja kabla Sauli hajaja, Bwana alikuwa amemfunulia Samweli jambo hili: 169:16 Kut 30:25; 1Sam 2:35; 12:3; 15:1; 26:9; 2Fal 11:12; Za 2:2; 2Sam 7:8; 1Fal 8; 16; 1Nya 5:2; Kut 3:8; 1Sam 23:4; 2Sam 3:18; Mwa 16:11; Za 102:1“Kesho wakati kama huu nitakupelekea mtu kutoka nchi ya Benyamini. Umtie mafuta awe kiongozi juu ya watu wangu Israeli, ndiye atakayewakomboa watu wangu na mkono wa Wafilisti. Nimewaangalia watu wangu, kwa kuwa kilio chao kimenifikia.”

179:17 1Sam 16:12; Hos 13:11Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, “Huyu ndiye mtu niliyekuambia habari zake, kwamba yeye atawatawala watu wangu.”

18Sauli akamkaribia Samweli langoni na kumuuliza, “Tafadhali, je, waweza kuniambia mahali nyumba ya mwonaji ilipo?”

19Samweli akamjibu Sauli, “Mimi ndiye mwonaji, panda utangulie mbele yangu mpaka mahali pa juu, kwa kuwa leo itakupasa kula pamoja nami na asubuhi nitakuruhusu uende na nitakuambia yale yote yaliyo moyoni mwako. 209:20 1Sam 12:13; Ezr 6:8; Isa 60:4-9; Dan 2:44; Hag 2:7; Mal 3:1Kuhusu wale punda uliowapoteza siku tatu zilizopita, usifadhaike kwa habari yao; wamepatikana. Ni kwa nani ambaye shauku yote ya Israeli imeelekea, kama si kwako na jamaa yote ya baba yako?”

219:21 Za 68:27; Kut 3:11; Mt 2:6; 1Kor 15:9; Amu 6:15; 20:35, 46; 1Sam 18:18; 15:17Sauli akajibu, “Je, mimi si Mbenyamini, kutoka kabila dogo kuliko yote ya Israeli, nao ukoo wangu si ndio mdogo kuliko koo zote za kabila la Benyamini? Kwa nini uniambie jambo la namna hiyo?”

22Kisha Samweli akamleta Sauli na mtumishi wake ndani ukumbini na kuwaketisha mahali pa heshima zaidi miongoni mwa wale waliokuwa wamealikwa; jumla yao walikuwa kama watu thelathini. 23Samweli akamwambia mpishi, “Leta ile sehemu ya nyama niliyokupa, ile niliyokuambia iweke kando.”

249:24 Law 7:24; Hes 18:18; Eze 24:4; Mdo 10:9Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.

259:25 Kum 22:8; Yos 2:8; Mt 24:17; Lk 5:19; Mdo 10:9Baada ya kushuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, Samweli alizungumza na Sauli juu ya dari ya nyumba yake. 26Walipoamka mapema alfajiri, Samweli akamwita Sauli darini, akamwambia, “Jiandae, nami nitakuaga uende zako.” Sauli alipokuwa tayari yeye na Samweli wakatoka nje pamoja. 27Hata walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu.” Naye mtumishi akafanya hivyo. “Lakini subiri hapa kwa kitambo kidogo, ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu.”

Bibelen på hverdagsdansk

1. Samuelsbog 9:1-27

Saul og Samuel mødes

1Der var en rig og anset mand af Benjamins stamme, som hed Kish. Kish var søn af Abiel, som var søn af Zeror, som var søn af Bekorat, som var søn af Afia. 2Kish havde en søn, der hed Saul. Han var den flotteste fyr i hele Israel, og han var et hoved højere end nogen anden i landet.

3En dag var nogle af Kish’ æsler løbet væk. Derfor sagde han til Saul: „Tag en tjener med dig og gå ud og led efter dem.” 4Saul og hans tjener gennemsøgte Efraims højland, Shalisha-egnen, Shalim-egnen og hele Benjamins land uden at finde æslerne. 5Da de til sidst nåede Zuf-området, sagde Saul til tjeneren: „Lad os gå hjem. Nu er min far sikkert mere bekymret for os end for æslerne.”

6Men tjeneren svarede: „Ved du hvad? I den by dér bor der en Guds profet, som folk har stor respekt for, fordi alt, hvad han siger, sker. Lad os opsøge ham. Måske han kan fortælle os, hvor vi kan finde æslerne.”

7„Men vi har ingen penge med, så vi kan betale ham,” indvendte Saul. „Vi har ingen verdens ting, ikke engang et stykke brød.”

8„Jo,” svarede tjeneren. „Jeg har et lille stykke sølv, en kvart shekel. Den vil jeg give ham, så han kan sige os, hvad vi skal gøre.” 9-11„Godt,” sagde Saul. „Lad os så bare prøve.”

Så begav de sig op ad bakken mod byen, hvor profeten holdt til. Undervejs mødte de nogle unge piger, som var på vej ned for at hente vand, og de spurgte dem: „Er seeren hjemme?” (På den tid kaldte man endnu profeter for „seere”. „Lad os gå hen og spørge seeren,” sagde man, når man ville spørge Gud til råds).

12-13Pigerne svarede: „Jo, han er kommet til byen i dag, for der skal ofres et dyr på offerhøjen. Hvis I følger vejen lige frem og går ind i byen, vil I træffe ham der. Han går snart op til offerhøjen, for det er ham, der skal velsigne slagtofferet, og folk har ikke lov at spise af slagtofferet, før han kommer.”

14Så skyndte de sig op til byen, og netop som de kom til byporten, kom Samuel gående hen imod dem på vej til offerhøjen.

15Dagen før havde Herren sagt til Samuel: 16„I morgen ved denne tid sender jeg en mand fra Benjamins land til dig. Ham skal du salve til konge over mit folk. Han skal frelse folket fra filistrenes herredømme, for jeg har hørt folkets klageråb og har besluttet at hjælpe dem.”

17Da Samuel fik øje på Saul, sagde Herren til ham: „Det er den mand, jeg fortalte dig om. Han skal regere over mit folk.”

18I det samme henvendte Saul sig til Samuel dér i byporten og spurgte: „Kan du sige mig, hvor seeren bor?”

19„Det er mig, der er seeren,” svarede Samuel. „Gå foran mig op til offerhøjen. Så kan vi spise sammen, og i morgen tidlig skal jeg fortælle dig, hvad du ønsker at vide, og sende dig af sted. 20Du skal ikke bekymre dig om æslerne, der løb bort for tre dage siden. De er i god behold. Men hvem er det, hele Israels håb står til, om ikke det er til dig og din slægt?”

21„Hvordan kan du sige sådan noget,” indvendte Saul. „Jeg er jo fra Benjamins stamme, den mindste i hele Israel. Og min slægt er den mest ubetydelige i hele stammen!”

22Men Samuel førte Saul og hans tjener ind i gildesalen og gav dem hæderspladsen blandt de 30 indbudte gæster, 23og han sagde til kokken: „Kom med det fine stykke kød, som er forbeholdt hædersgæsten.” 24Kokken løftede kødet op og lagde det foran Saul. „Spis! Det er til dig,” sagde Samuel. „Jeg havde lagt det stykke til side til dig, så du ved denne lejlighed kunne spise det sammen med de øvrige gæster.”

Så spiste Saul sammen med Samuel. 25Derefter gik de ned fra offerhøjen. Da de var kommet tilbage til byen, blev der redt op til Saul på tagterrassen. 26-27Ved daggry næste morgen råbte Samuel op til Saul: „Stå op! Jeg vil følge dig på vej.” Så stod Saul op, og Samuel gik med dem et stykke hen ad vejen. Da de var nået til udkanten af byen, sagde Samuel til Saul: „Sig til tjeneren, at han skal gå i forvejen, men bliv du her lidt endnu. Herren har nemlig givet mig et særligt budskab til dig.”