1 Samweli 21 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 21:1-15

Daudi Huko Nobu

121:1 1Sam 22:9; Neh 11:32; Isa 10:32; 1Sam 16:1Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamuuliza, “Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu yeyote?”

221:2 Mwa 27:20-24; 1Sam 19:11; 22:22; 1Fal 13:18; Za 119:29; 141:3; Mit 29:25; Gal 2:12, 13; Kol 3:9Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi yako wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia tukutane mahali fulani. 3Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata.”

421:4 Law 24:8-9; Mt 12:4; Kut 19:15; Law 15:18; 24:5; Zek 7:3Lakini kuhani akamjibu Daudi, “Sina mkate wowote wa kawaida kwa sasa. Hata hivyo, ipo hapa mikate iliyowekwa wakfu, iwapo watu wamejitenga na wanawake.”

521:5 Kum 23:9-11; Yos 3:5; 2Sam 11:11; 1Tim 4:4; 1The 4:4; Law 8:26Daudi akajibu, “Hakika tumejitenga na wanawake kwa siku hizi chache kama kawaida ya ninapotoka kwenda kwenye shughuli. Navyo vyombo vya wale vijana huwa ni vitakatifu hata kwenye safari ya kawaida, si zaidi sana leo vyombo vyao vitakuwa ni vitakatifu?” 621:6 Kut 25:30; 1Sam 22:10; Mt 12:3-4; Mk 2:25-28; Lk 6:1-5; Law 24:8Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwepo mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonyesho iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Bwana na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.

721:7 1Sam 22:9; 14:47; Za 52Basi siku hiyo palikuwepo na mmoja wa watumishi wa Sauli, aliyezuiliwa mbele za Bwana; alikuwa Doegi Mwedomu, kiongozi wa wachunga wanyama wa Sauli.

8Daudi akamuuliza Ahimeleki, “Je, unao mkuki au upanga hapa? Sikuleta upanga wala silaha nyingine yoyote, kwa sababu shughuli ya mfalme ilikuwa ya haraka.”

921:9 1Sam 17:51; 17:2, 4Kuhani akajibu, “Upanga wa Goliathi Mfilisti, ambaye ulimuua katika Bonde la Ela, upo hapa, umefungiwa katika kitambaa nyuma ya kisibau. Kama unauhitaji, uchukue, hakuna upanga mwingine hapa ila huo tu.”

Daudi akasema, “Hakuna upanga mwingine kama huo. Nipatie huo.”

Daudi Huko Gathi

1021:10 1Sam 25:13; 27:2-3; 18:7Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 1121:11 1Sam 18:7; 29:5; Za 50Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:

“ ‘Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake’?”

12Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 1321:13 Za 34Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.

14Akishi akawaambia watumishi wake, “Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu? 15Je, mimi nimepungukiwa na wenda wazimu kiasi kwamba mmeniletea mtu huyo hapa aendelee kufanya hivi mbele yangu? Je, ilikuwa ni lazima mtu huyo aje nyumbani kwangu?”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

撒母耳記上 21:1-15

大衛逃亡

1大衛來到挪伯的祭司亞希米勒那裡。亞希米勒戰戰兢兢地出來迎接他,問道:「你為什麼獨自一人,沒有隨從呢?」 2大衛答道:「王差遣我來辦一件事,他吩咐我不可把事情洩露給任何人。我已經吩咐部下在某處跟我會合。 3現在你這裡有什麼吃的嗎?請給我五個餅,或任何吃的東西。」 4祭司答道:「我們沒有普通的餅,只有聖餅21·4 聖餅」指分別出來獻給耶和華的餅。,如果你的部下沒有親近過女色,就可以吃。」 5大衛答道:「當然沒有親近過女色。每逢我們出來辦事,即使是平常的任務,我的部下總是保持聖潔,何況這次是特別的任務。」 6於是,祭司把聖餅給他,因為那裡沒有別的餅,只有從耶和華的會幕裡更換下來的供餅。 7那天,掃羅的司牧長以東多益碰巧在耶和華的會幕。 8大衛亞希米勒:「你這裡有沒有刀槍?因為王的事緊急,倉促間我連兵器也沒有帶。」 9祭司答道:「你在以拉谷殺的非利士歌利亞的刀在這裡,用布包著放在以弗得後面。如果你要就拿去吧,這裡沒有別的刀了。」大衛答道:「這刀再好不過了,把它給我吧。」

10那日,大衛為了躲避掃羅,逃往迦特亞吉那裡。 11亞吉的臣僕對亞吉說:「這個大衛不是以色列的王嗎?民眾跳舞歌唱『掃羅殺死千千,大衛殺死萬萬』,歌頌的不是他嗎?」 12大衛聽到這些話,擔心迦特亞吉會加害於他, 13就在他們面前裝作瘋子,在城門上胡亂塗畫,任由唾沫沿著鬍子流下來。 14亞吉對臣僕說:「你們看,這是個瘋子,為什麼把他帶到我這裡來? 15我這裡缺少瘋子嗎?你們怎麼可以把這個傢伙帶到我家裡,在我面前瘋瘋癲癲呢?」