1 Nyakati 27 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 27:1-34

Vikosi Vya Jeshi

1Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.

227:2 2Sam 23:8; 1Nya 11:11Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. 327:3 Mwa 38:29Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.

427:4 2Sam 23:9-20Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

527:5 1Fal 4:5Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. 627:6 2Sam 23:20-23Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.

727:7 2Sam 2:18; 1Nya 11:26-28; 2Sam 23:24Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

8Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

927:9 2Sam 23:26; 1Nya 11:28Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

10Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

1127:11 2Sam 21; 18; 1Nya 11:29Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

1227:12 2Sam 23:27; 1Nya 11:30-31Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

1327:13 2Sam 23:28; 1Nya 11:36Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

1427:14 2Sam 23:30; 1Nya 11:31Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

1527:15 2Sam 23:29; Yos 15:17; Amu 3:9Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

Maafisa Wa Makabila

16Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:

Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;

kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;

1727:17 1Nya 26:30; 2Sam 8:17; 1Nya 12:28kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;

kwa Aroni: Sadoki;

1827:18 1Sam 16:6kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;

kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;

19kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;

kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;

20kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;

kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;

21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;

kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;

22kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.

Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.

2327:23 2Sam 24:1; 1Nya 21:2-5; Mwa 12:2; 15:5; Kut 32:13; Ebr 11:12Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 2427:24 2Sam 24:15; 1Nya 21:7Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.

Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme

25Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.

Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.

26Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.

2727:27 Wim 8:11Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.

Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.

2827:28 1Fal 10:27; 2Nya 1:15Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.

Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.

29Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.

Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.

30Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.

Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.

3127:31 1Nya 5:10Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.

Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.

3227:32 2Sam 21:21Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.

3327:33 2Sam 15:12, 37Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.

Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 3427:34 1Sam 22:20; 2Sam 2:13; 1Nya 11:6Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.

Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志上 27:1-34

以色列的军队

1以色列人的族长、千夫长、百夫长及其他官长都分定班次,每班两万四千人,每年按月轮流服侍王。

2撒巴第业的儿子雅朔班负责第一班,在一月当值,他班内有两万四千人。 3他是法勒斯的子孙,统管一月当值的所有将领。 4亚哈希朵代负责二月的班次,他的副官是密基罗,他班内有两万四千人。 5祭司耶何耶大的儿子比拿雅负责第三班,在三月当值,他班内有两万四千人。 6比拿雅是当时的三十位勇士之一,也是三十位勇士之首。他儿子暗米萨拔在他班内做统领。 7约押的兄弟亚撒黑负责第四班,在四月当值,他班内有两万四千人,他儿子西巴第雅后来接替了他。 8伊斯拉珊合负责第五班,在五月当值,他班内有两万四千人。 9提哥亚益吉的儿子以拉负责第六班,在六月当值,他班内有两万四千人。 10以法莲的子孙比伦希利斯负责第七班,在七月当值,他班内有两万四千人。 11谢拉族的户沙西比该负责第八班,在八月当值,他班内有两万四千人。 12便雅悯的子孙亚拿突亚比以谢负责第九班,在九月当值,他班内有两万四千人。 13谢拉族的尼陀法玛哈莱负责第十班,在十月当值,他班内有两万四千人。 14以法莲的子孙比拉顿比拿雅负责第十一班,在十一月当值,他班内有两万四千人。 15俄陀聂族的尼陀法黑玳负责第十二班,在十二月当值,他班内有两万四千人。

以色列各支派的官长

16以下是以色列各支派的首领:吕便支派的首领是细基利的儿子以利以谢西缅支派的首领是玛迦的儿子示法提雅17利未支派的首领是基姆利的儿子哈沙比雅亚伦子孙的首领是撒督18犹大支派的首领是大卫的哥哥以利户以萨迦支派的首领是米迦勒的儿子暗利19西布伦支派的首领是俄巴第雅的儿子伊施玛雅拿弗他利支派的首领是亚斯列的儿子耶利摩20以法莲支派的首领是阿撒细雅的儿子何细亚玛拿西半个支派的首领是毗大雅的儿子约珥21基列玛拿西另半个支派的首领是撒迦利亚的儿子易多便雅悯支派的首领是押尼珥的儿子雅西业22支派的首领是耶罗罕的儿子亚萨列。以上这些人是以色列各支派的首领。 23大卫没有统计二十岁以下的以色列人,因为耶和华曾经应许要使以色列的人数像天上的星那样多。 24洗鲁雅的儿子约押开始统计人数,但没有完成,因为耶和华因此事而向以色列人发烈怒,因此统计的数目没有收录在大卫王记上。

王室产业的主管

25亚叠的儿子押斯马威管理王室的库房。乌西雅的儿子约拿单管理城邑、村庄和堡垒的库房。 26基绿的儿子以斯利管理耕田种地的人。 27拉玛示每管理葡萄园。实弗米撒巴底管理葡萄园的酒窖。 28基第利巴勒·哈南管理丘陵的橄榄树和无花果树。约阿施管理油仓。 29沙仑施提莱管理沙仑的牛群。亚第莱的儿子沙法管理山谷中的牛群。 30以实玛利阿比勒管理骆驼群。米仑耶希底亚管理驴群。 31夏甲雅悉管理羊群。以上这些人都是替大卫王管理产业的。

32大卫的叔叔约拿单很精明,任谋士和书记。哈摩尼的儿子耶歇做众王子的老师。 33亚希多弗也是王的谋士。亚基户筛是王的朋友。 34后来,比拿雅的儿子耶何耶大亚比亚他接替亚希多弗做谋士。约押在王的军队中做元帅。