路加福音 3 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

路加福音 3:1-38

施洗者約翰的傳道

1凱撒提庇留執政第十五年,本丟·彼拉多猶太總督,希律加利利的分封王,他的弟弟腓力以土利亞特拉可尼兩地的分封王,呂撒聶亞比利尼的分封王, 2亞那該亞法當大祭司。當時,撒迦利亞的兒子約翰住在曠野,上帝向他說話。 3他就到約旦河附近宣講悔改的洗禮,使人的罪得到赦免。 4這正應驗了以賽亞先知書上的話:「在曠野有人大聲呼喊,

『預備主的道,

修直祂的路。

5一切山谷將被填滿,

大山小丘將被削平,

彎曲的道路要被修直,

崎嶇的路徑要被鋪平。

6世人都要看見上帝的救恩。』」

7約翰對前來接受他洗禮的人群說:「你們這些毒蛇的後代!誰指示你們逃避那將臨的烈怒呢? 8你們要結出與悔改相稱的果子。不要心裡說,『我們是亞伯拉罕的子孫。』我告訴你們,上帝可以從這些石頭中興起亞伯拉罕的子孫。 9現在斧頭已經放在樹根上了,不結好果子的樹都要被砍下丟在火裡。」

10眾人問道:「那麼,我們該怎麼辦呢?」

11約翰回答說:「有兩件衣服的,應當分一件給沒有的;食物充裕的,應當分些給饑餓的。」

12有些稅吏也來受洗,並問約翰:「老師,我們該怎麼辦呢?」

13約翰說:「除了規定的稅以外,一分錢也不可多收。」

14有些軍人問:「我們該怎麼辦呢?」約翰說:「不可敲詐勒索,自己有糧餉就當知足。」

15當時的百姓正期待著基督的來臨,大家心裡都在猜想,也許約翰就是基督。 16約翰對眾人說:「我是用水給你們施洗,但有一位能力比我更大的快來了,我就是給祂解鞋帶也不配。祂要用聖靈和火給你們施洗。 17祂手裡拿著簸箕,要清理祂的麥場,把麥子收進倉庫,用不滅的火燒盡糠秕。」 18約翰向眾人傳福音,講了許多勸勉的話。

19分封王希律娶了自己弟弟的妻子希羅底,又做了許多惡事,因而受到約翰的指責, 20可是他卻惡上加惡,將約翰關進監牢裡。

耶穌受洗

21眾人都受了洗,耶穌也接受了洗禮。祂正在禱告的時候,天開了, 22聖靈像鴿子一樣降在祂身上,又有聲音從天上傳來:「你是我的愛子,我甚喜悅你。」

耶穌的家譜

23耶穌開始傳道的時候,年紀約三十歲,照人的看法,

祂是約瑟的兒子,

約瑟希里的兒子,

24希里瑪塔的兒子,

瑪塔利未的兒子,

利未麥基的兒子,

麥基雅拿的兒子,

雅拿約瑟的兒子,

25約瑟瑪他提亞的兒子,

瑪他提亞亞摩斯的兒子,

亞摩斯拿鴻的兒子,

拿鴻以斯利的兒子,

以斯利拿該的兒子,

26拿該瑪押的兒子,

瑪押瑪他提亞的兒子,

瑪他提亞西美的兒子,

西美約瑟的兒子,

約瑟猶大的兒子,

猶大約亞拿的兒子,

27約亞拿利撒的兒子,

利撒所羅巴伯的兒子,

所羅巴伯撒拉鐵的兒子,

撒拉鐵尼利的兒子,

尼利麥基的兒子,

28麥基亞底的兒子,

亞底哥桑的兒子,

哥桑以摩當的兒子,

以摩當的兒子,

約細的兒子,

29約細以利以謝的兒子,

以利以謝約令的兒子,

約令瑪塔的兒子,

瑪塔利未的兒子,

30利未西緬的兒子,

西緬猶大的兒子,

猶大約瑟的兒子,

約瑟約南的兒子,

約南以利亞敬的兒子,

31以利亞敬是米利亞的兒子,

米利亞邁南的兒子,

邁南瑪達他的兒子,

瑪達他拿單的兒子,

拿單大衛的兒子,

32大衛耶西的兒子,

耶西俄備得的兒子,

俄備得波阿斯的兒子,

波阿斯撒門的兒子,

撒門拿順的兒子,

33拿順亞米拿達的兒子,

亞米拿達的兒子,

希斯崙的兒子,

希斯崙法勒斯的兒子,

法勒斯猶大的兒子,

34猶大雅各的兒子,

雅各以撒的兒子,

以撒亞伯拉罕的兒子,

亞伯拉罕他拉的兒子,

他拉拿鹤的兒子,

35拿鹤西鹿的兒子,

西鹿拉吳的兒子,

拉吳法勒的兒子,

法勒希伯的兒子,

希伯沙拉的兒子,

36沙拉該南的兒子,

該南亞法撒的兒子,

亞法撒的兒子,

挪亞的兒子,

挪亞拉麥的兒子,

37拉麥瑪土撒拉的兒子,

瑪土撒拉以諾的兒子,

以諾雅列的兒子,

雅列瑪勒列的兒子,

瑪勒列蓋南的兒子,

蓋南以挪士的兒子,

38以挪士塞特的兒子,

塞特亞當的兒子,

亞當是上帝的兒子。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 3:1-38

Yohana Mbatizaji Aanza Kuhubiri

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Yohana 1:19-28)

13:1 Mt 27:2Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, 23:2 Yn 18:13; Mdo 4:6; Mt 3:1nao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko jangwani. 33:3 Mk 3:16; Mal 1:4Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 43:4 Isa 40:3-5; Mt 3:3; Mk 1:3; Yn 1:23Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Sauti ya mtu aliaye nyikani,

‘Itengenezeni njia ya Bwana,

yanyoosheni mapito yake.

5Kila bonde litajazwa,

kila mlima na kilima vitashushwa.

Njia zilizopinda zitanyooshwa,

na zilizoparuza zitasawazishwa.

63:6 Za 98:2; Lk 2:30Nao watu wote watauona

wokovu wa Mungu.’ ”

73:7 Mt 12:34; 23:33; Rum 1:18Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 83:8 Isa 51:7; Gal 3:7Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya. 93:9 Mt 3:10Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

103:10 Mdo 2:37; 16:30Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”

113:11 Isa 58:7; Eze 18:7Yohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”

123:12 Lk 7:29Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

133:13 Lk 19:8Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

143:14 Law 19:11Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”

Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

153:15 Mt 3:1; Yn 1:19-20; Mdo 13:25Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.3:15 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. 163:16 Mk 1:4; Yn 1:26, 33; Mdo 11:16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.3:16 Tafsiri nyingine zinasema ndani ya maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 173:17 Isa 30:24; Mt 13:30; 25:41Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” 18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

193:19 Mt 14:1Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, 203:20 Mt 14:3-4Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani.

Kubatizwa Kwa Bwana Yesu

(Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11)

213:21 Mt 14:23; Mk 1:35Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 223:22 Isa 42:1; Yn 1:32-33; Mt 3:17Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Ukoo Wa Bwana Yesu

(Mathayo 1:1-17)

233:23 Mt 4:17; Lk 1:27Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu,

Yosefu alikuwa mwana wa Eli,

24Eli alikuwa mwana wa Mathati,

Mathati alikuwa mwana wa Lawi,

Lawi alikuwa mwana wa Melki,

Melki alikuwa mwana wa Yanai,

Yanai alikuwa mwana wa Yosefu,

25Yosefu alikuwa mwana wa Matathia,

Matathia alikuwa mwana wa Amosi,

Amosi alikuwa mwana wa Nahumu,

Nahumu alikuwa mwana wa Esli,

Esli alikuwa mwana wa Nagai,

26Nagai alikuwa mwana wa Maathi,

Maathi alikuwa mwana wa Matathia,

Matathia alikuwa mwana wa Semeini,

Semeini alikuwa mwana wa Yoseki,

Yoseki alikuwa mwana wa Yoda,

273:27 Mt 1:12; 1Nya 3:17Yoda alikuwa mwana wa Yoanani,

Yoanani alikuwa mwana wa Resa,

Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli,

Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli,

Shealtieli alikuwa mwana wa Neri,

28Neri alikuwa mwana wa Melki,

Melki alikuwa mwana wa Adi,

Adi alikuwa mwana wa Kosamu,

Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu,

Elmadamu alikuwa mwana wa Eri,

29Eri alikuwa mwana wa Yoshua,

Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri,

Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu,

Yorimu alikuwa mwana wa Mathati,

Mathati alikuwa mwana wa Lawi,

30Lawi alikuwa mwana wa Simeoni,

Simeoni alikuwa mwana wa Yuda,

Yuda alikuwa mwana wa Yosefu,

Yosefu alikuwa mwana wa Yonamu,

Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu,

Eliakimu alikuwa mwana wa Melea,

313:31 2Sam 5:14; 1Nya 3:5Melea alikuwa mwana wa Mena,

Mena alikuwa mwana wa Matatha,

Matatha alikuwa mwana wa Nathani,

Nathani alikuwa mwana wa Daudi,

323:32 Rut 4:22; 1Nya 2:10Daudi alikuwa mwana wa Yese,

Yese alikuwa mwana wa Obedi,

Obedi alikuwa mwana wa Boazi,

Boazi alikuwa mwana wa Salmoni,

Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni,

333:33 Rut 4:18-22; 1Nya 2:10Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu,

Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu,

Aramu alikuwa mwana wa Hesroni,

Hesroni alikuwa mwana wa Peresi,

Peresi alikuwa mwana wa Yuda,

343:34 Mwa 11:24-26Yuda alikuwa mwana wa Yakobo,

Yakobo alikuwa mwana wa Isaki,

Isaki alikuwa mwana wa Abrahamu,

Abrahamu alikuwa mwana wa Tera,

Tera alikuwa mwana wa Nahori,

35Nahori alikuwa mwana wa Serugi,

Serugi alikuwa mwana wa Reu,

Reu alikuwa mwana wa Pelegi,

Pelegi alikuwa mwana wa Eberi,

Eberi alikuwa mwana wa Sala,

363:36 Mwa 5:28-32; 11:12Sala alikuwa mwana wa Kenani,

Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi,

Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu,

Shemu alikuwa mwana wa Noa,

Noa alikuwa mwana wa Lameki,

373:37 Mwa 5:12-25Lameki alikuwa mwana wa Methusela,

Methusela alikuwa mwana wa Enoki,

Enoki alikuwa mwana wa Yaredi,

Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli,

Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani,

383:38 Mwa 5:19Kenani alikuwa mwana wa Enoshi,

Enoshi alikuwa mwana wa Sethi,

Sethi alikuwa mwana wa Adamu,

Adamu alikuwa mwana wa Mungu.