歷代志下 11 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 11:1-23

耶和華禁止他們交戰

1羅波安回到耶路撒冷,從猶大便雅憫支派召集了十八萬精兵,要攻打以色列,收復全國。 2然而,耶和華上帝對祂的僕人示瑪雅說: 3「你去告訴所羅門的兒子猶大羅波安和所有住在猶大便雅憫以色列人, 4耶和華這樣說,『你們不要上去與弟兄交戰,都回家吧,因為這事出於我。』」眾人聽從了耶和華的話,沒有去攻打耶羅波安,各自回家去了。

羅波安加強防禦

5羅波安住在耶路撒冷,他在猶大修築城池以作防禦。 6他修築的城池有伯利恆以坦提哥亞7伯·夙梭哥亞杜蘭8迦特瑪利沙西弗9亞多萊音拉吉亞西加10瑣拉亞雅崙希伯崙,這些都是猶大便雅憫的堅城。 11他又在各城池加強防禦,派將領駐守,供給食物、油和酒。 12他在城內儲備盾牌和矛槍,使城池非常堅固。猶大便雅憫都歸屬他。

祭司和利未人投奔猶大

13以色列全境的祭司和利未人都從四面八方來投奔羅波安14利未人撇下他們的草場和產業,來到猶大耶路撒冷,因為耶羅波安和他的眾子不准他們做祭司事奉耶和華。 15耶羅波安卻為邱壇、公山羊像和他造的牛犢像設立他自己的祭司。 16以色列各支派中那些誠心尋求以色列的上帝耶和華的人,都跟隨利未人到耶路撒冷獻祭給他們祖先的上帝耶和華。 17他們使猶大國堅固,他們效忠所羅門的兒子羅波安三年之久,並在此期間遵行大衛所羅門的道。

羅波安的家室

18羅波安娶了大衛的兒子耶利摩的女兒瑪哈拉為妻,她母親亞比孩耶西的兒子以利押的女兒。 19瑪哈拉為他生了耶烏施示瑪利雅撒罕三個兒子。 20後來,他又娶了押沙龍的女兒瑪迦11·20 押沙龍的女兒瑪迦」或譯「押沙龍的孫女瑪迦」。,生了亞比雅亞太細撒示羅密21羅波安共有十八個妻子、六十個妾、二十八個兒子、六十個女兒。眾妻妾中瑪迦最得寵愛, 22羅波安就立她所生的兒子亞比雅為太子,以便讓他繼承王位。 23羅波安精明地把其他王子派駐到猶大便雅憫境內的各堅城,給他們充足的供應和許多妻妾。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 11:1-23

Utabiri Wa Shamaya

(1 Wafalme 12:21-24)

111:1 1Fal 12:21Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni.

211:2 1Sam 2:27; 1Fal 12:22-24; 2Nya 12:15; Kum 33:1; 2Nya 8:14; 1Tim 6:11Lakini neno hili la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu: 3“Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda, na Israeli wote walioko Yuda na Benyamini, 411:4 2Nya 28:8-11; 28:8-11‘Hili ndilo asemalo Bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Bwana na wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.

Yeroboamu Ajengea Yuda Ngome

5Rehoboamu akaishi Yerusalemu akajenga miji yenye ngome katika Yuda: 611:6 Mwa 35:19; Amu 15:8; 1Sam 17:12; 2Nya 20:20; 2Sam 14:2; Neh 3:5; Yer 3:5; 6:1; Amo 1:1Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa, 7Beth-Suri, Soko, Adulamu, 8Gathi, Maresha, Zifu, 9Adoraimu, Lakishi, Azeka, 10Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ndiyo iliyokuwa miji iliyojengewa ngome katika Yuda na Benyamini. 11Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na ghala za mahitaji ya vyakula, mafuta ya zeituni na divai. 12Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.

13Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake. 1411:14 Hes 35:2-5; 1Nya 6:81; 2Nya 13:9; 1Fal 12:28-33Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Bwana. 1511:15 1Fal 12:28-31; 13:33; Law 17:7; 2Nya 13:8; Kum 32:15-17; Hos 13:2; 1Kor 10:20; Ufu 16:14; 1Fal 12:28Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza. 1611:16 2Nya 15:9; Za 69:32; 2Nya 30:11Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Bwana dhabihu, Mungu wa baba zao. 1711:17 2Nya 12:1; Mt 13:18; Hos 6:4Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu.

Jamaa Ya Rehoboamu

18Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese. 1911:19 1Fal 15:2Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu. 2011:20 1Fal 15:2; 2Nya 12:16Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi. 2111:21 Kum 15:17Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini.

2211:22 Kum 21:15-17Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme. 2311:23 Kum 17:17; 1Fal 11:3Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi.