歷代志下 12 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 12:1-16

埃及侵犯猶大

1羅波安王位穩定、國勢強盛後,就離棄耶和華的律法,以色列人也都隨從他。 2羅波安王執政第五年,埃及示撒上來攻打耶路撒冷,因為猶大君民對耶和華不忠。 3示撒率領一千二百輛戰車、六萬騎兵及無數的路比人、蘇基人和古實人。 4他攻陷了猶大的堅城,直逼耶路撒冷

5那時,猶大各首領因為戰事都聚集在耶路撒冷示瑪雅先知去見羅波安和眾首領,對他們說:「耶和華說,『你們背棄了我,所以我也要離棄你們,把你們交在示撒手中。』」 6王與以色列的眾首領聽了,就謙卑下來說:「耶和華是公義的。」 7耶和華見他們謙卑下來,就對示瑪雅說:「既然他們謙卑下來,我就不滅絕他們,給他們留一條生路。我也不會藉示撒耶路撒冷傾倒我的憤怒。 8然而,他們必做示撒的僕人,好讓他們體驗事奉我和服侍世上的君王的不同。」

9埃及示撒帶兵攻陷了耶路撒冷,把耶和華殿裡和王宮裡的財寶及所羅門造的金盾牌擄掠一空。 10羅波安王就造了銅盾牌代替金盾牌,交給看守宮門的護衛長看管。 11每次王進耶和華的殿,護衛兵就帶上盾牌,用完後放回護衛房。 12王謙卑下來後,耶和華便不再向他發怒,沒有將他完全毀滅。況且,在猶大還有一些善事。

羅波安逝世

13羅波安王在耶路撒冷鞏固了自己的勢力,繼續做王。他四十一歲登基,在耶路撒冷執政十七年。耶和華從以色列眾支派中選擇耶路撒冷作為立祂名的城。羅波安的母親叫拿瑪,是亞捫人。 14羅波安行為邪惡,因為他不專心尋求耶和華。

15他執政期間的事件自始至終都記在示瑪雅先知和易多先見的史記上。羅波安耶羅波安之間常有爭戰。 16羅波安與祖先同眠後,葬在大衛城。他兒子亞比雅繼位。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 12:1-16

Shishaki Ashambulia Yerusalemu

(1 Wafalme 14:25-28)

112:1 2Nya 11:17; Kum 8:14; 1Fal 14:22-24Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria ya Bwana Mungu. 212:2 1Nya 5:25; 1Fal 11:40; 14:24-25Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Bwana, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu. 312:3 Mwa 10:6; Amo 9:7; 2Nya 16:8Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi12:3 Yaani watu kutoka sehemu ya Naili ya juu. yaliyokuja pamoja naye kutoka Misri. 412:4 2Nya 11:10Akateka miji ya Yuda yenye ngome akaendelea mpaka Yerusalemu.

512:5 2Nya 11:1; Kum 28:15; 2Nya 15:1-2Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.’ ”

612:6 Law 26:40-42; Ezr 9:15; Yak 4:10; Kut 9:27; 10:3; 2Nya 33:12; 34:27; Za 78:34Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Bwana Mungu ni mwenye haki.”

712:7 1Fal 21:29; Za 78:38Bwana Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Bwana likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kwa kupitia Shishaki. 812:8 Kum 28:48; Isa 26:13Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.”

912:9 2Nya 9:16; 1Fal 14:25Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza. 1012:10 2Sam 8:18; 23:23; 1Nya 11:25Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme. 11Kila wakati mfalme alipokwenda katika Hekalu la Bwana walinzi walikwenda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.

1212:12 1Fal 14:13; 2Nya 19:3; Mwa 18:24Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Bwana ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.

1312:13 2Nya 6:6; 13:7; Kum 12:5; 1Fal 14:21; Za 48:1-3Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao Bwana alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, alikuwa Mwamoni. 1412:14 Mt 7:7; Mdo 9:11Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta Bwana Mungu.

1512:15 2Nya 9:29; 13:22Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu. 1612:16 2Nya 11:20Rehoboamu akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akawa mfalme baada yake.