马太福音 17 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 17:1-27

登山变象

1六天后,耶稣带着彼得雅各雅各的兄弟约翰暗暗地登上一座高山。 2耶稣在他们面前改变了形象,面貌如太阳一样发光,衣服洁白如光。 3忽然,摩西以利亚一起出现,跟耶稣谈话。 4彼得对耶稣说:“主啊,我们在这里好极了。如果你愿意,我就在这里搭三座帐篷,一座给你,一座给摩西,一座给以利亚。”

5他正在说话的时候,一朵灿烂的云彩笼罩他们。云中传出声音:“这是我的爱子,我甚喜悦祂,你们要听从祂。”

6门徒听见这声音,便俯伏在地,非常惧怕。 7耶稣就过来摸他们,说:“起来吧,别害怕。” 8他们抬起头来,看见只剩下耶稣一个人。

9下山时,耶稣叮嘱他们:“人子还没有从死里复活以前,不要把刚才看见的告诉别人。”

10门徒问耶稣:“律法教师为什么说以利亚必须先来?”

11耶稣回答说:“以利亚的确要来,他将复兴一切。 12但我告诉你们,以利亚已经来了,人们却不认识他,甚至还任意对待他。人子同样也会在他们手下受苦。” 13门徒这才明白耶稣所说的是指施洗者约翰

治好被鬼附身的孩子

14他们回到山下众人聚集的地方。有一个人过来跪在耶稣跟前,说: 15“主啊!救救我的儿子吧!他患了癫痫症,痛苦极了,曾经几次跌进火中,掉进水里。 16我带他去见你的门徒,但他们却不能治好他。”

17耶稣说:“唉!这世代又不信又败坏的人啊,我要跟你们在一起待多久?我要容忍你们多久呢?把他带来吧。” 18耶稣斥责附在孩子身上的鬼,鬼就离开了那孩子,从此他就好了。

19事后,门徒私下问耶稣:“我们为什么赶不走那鬼呢?”

20耶稣说:“你们的信心太小了。我实在告诉你们,你们若有像芥菜种那样大的信心,就算叫这座山从这里移到那里,它也会移开,你们将没有办不到的事。 21至于这一类的鬼,你们必须祷告和禁食才能把它赶走。”

耶稣第二次预言受害和复活

22他们聚集在加利利的时候,耶稣对他们说:“人子将要被出卖,交在人手里。 23他们将杀害祂,第三天祂将复活。”门徒听了,十分忧愁。

从鱼口得税钱

24他们来到迦百农,有几个收圣殿税的来问彼得:“你们的老师不纳圣殿税吗?”

25彼得说“纳!”他进了屋,还没开口,耶稣便问他:“西门,你有何看法?世上的君王向谁征收赋税?向自己的儿子呢,还是向外人呢?”

26彼得答道:“向外人。”

耶稣说:“所以儿子不用纳税。 27但为了避免得罪这些人,你就去湖边钓鱼,把钓上来的第一条鱼的嘴打开,里面有一个钱币,拿它去缴你我的税好了。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 17:1-27

Yesu Abadilika Sura Mlimani

(Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)

117:1 Mk 9:2; Lk 9:28; Mt 4:21Siku sita baada ya jambo hili, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapeleka juu ya mlima mrefu peke yao. 217:2 2Pet 1:16-18Wakiwa huko, Yesu alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukangʼaa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho. 3Ghafula wakawatokea mbele yao Mose na Eliya, wakizungumza na Yesu.

4Ndipo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.”

517:5 Mt 3:17; 2Pet 1:17; Mdo 3:22-23Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”

617:6 2Pet 1:18Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. 717:7 Mt 14:27Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” 8Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine yeyote isipokuwa Yesu.

917:9 Mk 8:30; Mt 8:20; 16:21; Mk 8:30; Mt 8:20; 16:21Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”

1017:10 Mt 11:14; Mal 4:5Wale wanafunzi wakamuuliza, “Kwa nini basi walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?”

1117:11 Mal 4:5-6; Lk 1:16-17Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. 1217:12 Mt 11:14; 14:3, 10; 16:21Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao.” 1317:13 Lk 1:17Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yohana Mbatizaji.

Yesu Amponya Kijana Mwenye Pepo

(Marko 9:14-29; Luka 9:37-43)

1417:14 Mk 9:14-20Walipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Yesu na kupiga magoti mbele yake, akasema, 1517:15 Mt 4:24“Bwana, mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au kwenye maji. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.”

1717:17 Kum 32:5; Yn 14:9Yesu akajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana hapa kwangu.” 18Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona saa ile ile.

1917:19 Mt 10:1Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu wakiwa peke yao, wakamuuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa?”

2017:20 Mt 21:21; Mk 11:23; Lk 17:6; 1Kor 13:2Akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Ninawaambia kweli, mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale,’ nao utaondoka. Wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwenu. [ 21Lakini hali kama hii haitoki ila kwa kuomba na kufunga.]”

2217:22 Mt 8:20Siku moja walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. 2317:23 Mdo 2:23; 3:13; Mt 16:21Nao watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika sana.

Yesu Na Petro Watoa Kodi Ya Hekalu

2417:24 Kut 30:13Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu17:24 Kodi ya Hekalu ilikuwa didrachmas, yaani drakma mbili, ambazo ni sawa na nusu shekeli. wakamjia Petro na kumuuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?”

2517:25 Mt 12:17-21; Rum 13:7Petro akajibu, “Ndiyo, yeye hulipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?”

26Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Yesu akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa. 2717:27 Yn 6:61Lakini ili tusije tukawaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemvua. Fungua kinywa chake nawe utakuta humo fedha, ichukue ukalipe kodi yako na yangu.”