马太福音 16 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 16:1-28

求神迹

1有几个法利赛人和撒都该人来试探耶稣,要求祂显个天上的神迹给他们看。

2耶稣回答说:“傍晚的时候,你们看见天边出现红霞,就说明天一定是晴天; 3早晨的时候,你们看见天色又红又暗,就说今天必有风雨。你们懂得分辨天色,却不能分辨时代的征兆。 4一个邪恶淫乱的世代想看神迹,可是除了约拿的神迹以外,再没有神迹给他们看。”于是耶稣离开他们走了。

防备法利赛人和撒都该人的酵

5门徒渡到湖对岸,忘记带饼了。 6耶稣对他们说:“你们要小心提防法利赛人和撒都该人的酵。”

7门徒彼此议论说:“这是因为我们没有带饼吧。”

8耶稣知道他们的心思,就说:“你们的信心太小了!为什么议论没有带饼的事呢? 9你们还不明白吗?你们不记得那五个饼让五千人吃饱,又装满多少篮子吗? 10也不记得那七个饼给四千人吃饱,又装满多少筐子吗? 11我说你们要提防法利赛人和撒都该人的酵,指的不是饼,你们怎么不明白呢?”

12门徒这才恍然大悟,知道耶稣不是叫他们当心什么面酵,而是要提防法利赛人和撒都该人的教导。

彼得宣告耶稣是基督

13到了凯撒利亚·腓立比境内,耶稣问门徒:“人们说人子是谁?”

14门徒回答说:“有人说是施洗者约翰,有人说是以利亚,也有人说是耶利米,或其他某位先知。”

15耶稣问:“那么,你们说我是谁?”

16西门·彼得回答说:“你是基督,是永活上帝的儿子!”

17耶稣对他说:“约拿的儿子西门啊,你是有福的!因为这件事不是属血肉的人告诉你的,而是我天上的父启示你的。 18我告诉你,你是彼得16:18 彼得”希腊文是“磐石”的意思。,我要在这磐石上建立我的教会,阴间的势力16:18 势力”希腊文是“门”。不能胜过它。 19我要把天国的钥匙交给你。凡你在地上捆绑的,在天上也要捆绑;凡你在地上释放的,在天上也要释放。”

20当下,耶稣叮嘱门徒不可告诉别人祂就是基督。

耶稣预言自己的受害和复活

21从此以后,耶稣开始清楚地指示门徒,祂必须去耶路撒冷,受长老、祭司长和律法教师许多的迫害,并且被处死,但第三天必从死里复活。 22彼得把耶稣拉到一边,劝阻祂说:“主啊,千万不可!这件事绝不会发生在你身上!”

23耶稣立刻转过身来责备彼得说:“撒旦,退到我后面去!你是我的绊脚石,因为你不考虑上帝的意思,只考虑人的意思。”

24于是耶稣对门徒说:“如果有人要跟从我,就应当舍己,背起他的十字架跟从我。 25因为想救自己生命的,必失去生命;但为了我而失去生命的,必得到生命。 26人若赚得全世界,却丧失自己的生命,又有什么益处呢?人还能拿什么换回自己的生命呢?

27“因为人子要在祂父的荣耀中与众天使一起降临,那时,祂将按照各人的行为报应各人。 28我实在告诉你们,有些站在这里的人会在有生之年看见人子降临在祂的国度里。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 16:1-28

Mafarisayo Wadai Ishara

(Marko 8:11-13; Luka 12:54-56)

116:1 Mdo 4:1; Mt 12:38Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu na kumjaribu kwa kumwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

216:2 Lk 12:54-56Yesu akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’ 316:3 Lk 12:54-56Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati. 416:4 Mt 12:39Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.

Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo

(Marko 8:14-21)

516:5 Mk 8:14Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. 616:6 Lk 12:1Yesu akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

7Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.”

816:8 Mt 6:30Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? 916:9 Mt 14:17-21Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 1016:10 Mt 15:34-38Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 11Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 1216:12 Yn 6:27; Mdo 4:1Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ni Mwana Wa Mungu

(Marko 8:27-30; Luka 9:18-21)

1316:13 Mk 8:27; Lk 9:18Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?”

1416:14 Mt 3:1; 14:2; Mk 6:15; Yn 1:21; Mt 14:2; Lk 9:7, 8, 9Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.”

15Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

1616:16 Yer 10:10; Yn 11:27Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo,16:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu aliye hai.”

1716:17 Gal 1:16; Efe 6:12Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona,16:17 Bar-Yona ni neno la Kiaramu, maana yake ni Mwana wa Yona. kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. 1816:18 Yn 1:42; Efe 2:20Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. 1916:19 Isa 22:22; Ufu 3:7; Mt 18:18; Yn 20:23Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.” 2016:20 Mt 8:30 Kisha akawakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.

Yesu Anatabiri Juu Ya Kifo Chake

(Marko 8:31–9:1; Luka 9:22-27)

2116:21 Za 22:6; Yn 19:3; Hos 6:2; 1Kor 15:3-4; Lk 18:31-33; 9:22Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.

22Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea akisema, “Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!”

2316:23 Mt 4:10Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

2416:24 Mt 10:38-39; Lk 14:27Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 2516:25 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. 2616:26 Za 49; Mt 4:8Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 2716:27 Mt 8:20; 1Kor 1:7; Ufu 22:7; 2Nya 6:23; 2Kor 5:10Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 2816:28 Mk 9:1; Lk 9:27; Mt 10:23Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake.”