Zaburi 130
Kuomba Msaada
Wimbo wa kwenda juu.
1130:1 Ay 30:19Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2130:2 Za 27:7; 28:2, 6; 31:22; 86:6; 140:6; 2Nya 6:40Ee Bwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
3130:3 1Sam 6:20; Ezr 9:15; Hes 1:6; Za 143:2; Ufu 6:17; Yn 8:7, 9; Rum 3:20Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4130:4 Kut 34:7; Efe 1:7; 2Sam 24:14; Yer 17:5-6; 31:34; 1Fal 8:40; 2The 1:6; Za 37:2; Ebr 12:28Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
5130:5 Isa 8:17; 26:8; 30:18; 49:23; Za 5:3; 119:74; 27:14Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6130:6 Za 63:6; 2Sam 23:4Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7130:7 1Nya 21:13; Za 25:5; 71:14; 111:9; Rum 3:24; Isa 55:7Ee Israeli, mtumaini Bwana,
maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8130:8 Lk 1:68; Kut 34:7; Mt 1:21Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka dhambi zao zote.