约伯记 1 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约伯记 1:1-22

约伯的敬虔

1乌斯有一个人名叫约伯,他纯全正直,敬畏上帝,远离罪恶。 2他有七子三女、 3七千只羊、三千只骆驼、五百对牛、五百头母驴及许多仆婢。他在东方人中最富有。 4约伯的儿子们经常轮流在自己家里设宴,派人邀请他们的三个姊妹来一起吃喝。 5宴会的日子结束后,约伯便派人召来他的儿女,为他们行洁净礼。他清早起来,为他们每个人献上燔祭,因为他想:“也许我的孩子们犯了罪,心中亵渎了上帝。”约伯常常这样做。

撒旦控告约伯

6有一天,众天使1:6 众天使”希伯来文是“上帝的众子”,2:138:7同。来朝见耶和华,撒旦也在他们当中。 7耶和华问撒旦:“你从哪里来?”撒旦答道:“我在地上到处游走。” 8耶和华问撒旦:“你注意到我的仆人约伯了吗?世上没有人像他那样纯全正直,敬畏我,远离罪恶。” 9撒旦说:“约伯敬畏你难道无缘无故吗? 10你岂不是像篱笆一样四面保护他及其全家和一切产业吗?你使他事事蒙福,牛羊遍地。 11倘若你伸手毁坏他拥有的一切,他必当面亵渎你。” 12耶和华对撒旦说:“好吧,他的一切都在你手中,但不可伤害他。”撒旦便从耶和华面前退去。

约伯失去所有

13有一天,约伯的儿女正在长兄家吃喝, 14有报信的人来对约伯说:“牛正在耕田、驴正在旁边吃草的时候, 15示巴人忽然来袭,抢走了牲口,用刀杀了你的仆人,只有我一人逃脱来向你报信。” 16话音未落,又有人来报信说:“上帝的火从天而降,烧死了羊群和牧人,只有我一人逃脱来向你报信。” 17话音未落,又有人来报信说:“迦勒底人分三队来袭,抢走了骆驼,用刀杀了你的仆人,只有我一人逃脱来向你报信。” 18话音未落,又有人来报信说:“你的儿女正在长兄家吃喝的时候, 19忽然从旷野刮来一阵狂风,摧毁了房子四角,房子倒塌,压死了屋里所有的人,只有我一人逃脱来向你报信。”

20约伯站起来,撕裂外袍,剃掉头发,俯伏在地上敬拜, 21说:“我从母腹赤身而来,也必赤身而去。赏赐的是耶和华,收回的也是耶和华。耶和华的名当受称颂!” 22约伯遭此不幸,仍没有犯罪,也没有埋怨上帝。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 1:1-22

Sehemu Ya Kwanza: Habari Za Awali

(Ayubu 1–2)

Ayubu Na Jamaa Yake

11:1 Mwa 22:21; Yak 5:11; Eze 14:14, 20; Mit 8:13; Mwa 10:23; 6:9; 22:12; Ay 23:7, 10; 2:3; Za 11:7; 107:42; Mit 21:29; Mik 7:2; Kum 4:6; 1The 5:22Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu. 21:2 Za 127:3; Rut 4:15; Ay 1:13, 18; 42:13; Za 144:12Alikuwa na wana saba na binti watatu, 31:3 Ay 29:25; Mwa 13:2; 12:16; Ay 1:8; Mwa 25:6; Ay 42:10; Za 103:10naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.

41:4 Ay 1:13, 18Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. 51:5 Mwa 8:20; Ay 42:8; 1Fal 21:10-13; Za 74:10; Neh 12:30; Ay 8:4; Za 10:3Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

Jaribu La Kwanza La Ayubu

61:6 1Fal 22:19; Ay 38:7; 2:1; Dan 7:10; Mwa 6:2; 2Sam 24:1; 2Nya 18:21; Za 109:6; Lk 22:31Siku moja wana wa Mungu1:6 Wana wa Mungu hapa ina maana malaika au viumbe vya mbinguni. walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani1:6 Shetani hapa ina maana ya mshtaki wa watakatifu. naye akaja pamoja nao. 71:7 Mwa 3:1; 1Pet 5:8; Mt 12:43Bwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

81:8 Ay 42:7-8; Kut 20:20; Yos 1:7; Za 25:16; 26:12; 112:1; 128:4Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

91:9 1Tim 6:5Shetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? 101:10 Za 34:7; 128:1-2; Ay 8:7; 1Sam 25:16; Ay 2:4; 29:6; 42:12, 17Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima. 111:11 Ay 19:21; Law 24:11; Ufu 12:9-10; Lk 22:31; Isa 3:8; 65:3; Ay 2:5Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

121:12 Ay 2:6; 1Kor 10:13Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”

Ndipo Shetani akatoka mbele za Bwana.

131:13 Ay 1:2, 4; Mhu 9:12; Lk 12:19, 20Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 141:14 Mwa 36:24akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao, 151:15 Mwa 10:7; Ay 6:19; 9:26Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

161:16 1Fal 18:38; 2Fal 1:12; Ay 20:26; Mwa 18:17; Law 10:2; Hes 11:1-3Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

171:17 Mwa 11:28-31; Ay 9:24Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”

181:18 Ay 1:2, 4Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 191:19 Isa 21:1; Mk 7:25; Za 11:6; Isa 5:28; Yer 4:11; 13:24; 18:17; Eze 17:10; Hos 13:15ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

201:20 Mwa 37:29; Mk 14:63; Isa 3:24; 15:2; 22:12; Yer 7:29; 16:6; Eze 27:31; 29:18; Mik 1:16; 1Pet 5:6Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu 211:21 Mhu 5:15; Rut 1:21; Amu 10:15; Efe 5:20; Mwa 45:5; 1Tim 6:7; 1Sam 2:7; Mhu 7:14; Yak 5:11; Amo 3:6; Efe 5:20; Mwa 45:5na kusema:

“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,

nami nitaondoka uchi,1:21 Au: nitarudi huko uchi.

Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa,

jina la Bwana litukuzwe.”

221:22 Mit 10:19; Rum 9:20; Ay 2:10; Za 39:1; Isa 53:7Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.