以赛亚书 33 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以赛亚书 33:1-24

主必拯救锡安

1你们这些毁灭别人、自己还未被毁灭的人有祸了!

等你们毁灭完了,就毁灭你们。

你们这些欺诈别人、自己还未被欺诈的人有祸了!

等你们欺诈完了,就欺诈你们。

2耶和华啊,求你施恩给我们,

我们等候你。

求你每天早晨都作我们的力量,

在艰难的时候拯救我们。

3你大喊一声,列邦都奔逃;

你一站起来,列国都溃散。

4他们的战利品必被拿走,

就像谷物被蝗虫吃掉一样;

人们像蝗虫一样扑向他们的战利品。

5耶和华受尊崇,

因为祂住在高天之上,

祂必使锡安充满公平和公义。

6祂必成为你一生的保障,

使你得到丰盛的救恩、智慧和知识。

敬畏耶和华是你最大的宝藏。

7看啊,他们的勇士在街上哀号,

求和的使者悲痛哭泣。

8大路荒凉,行人绝迹。

条约被废,城邑被弃,

人民遭藐视。

9地上一片荒凉,

黎巴嫩的树木枯干,

沙仑好像旷野,

巴珊迦密的树叶凋零。

10耶和华说:

“我现在要施展大能,

我必受尊崇。

11你们所谋的像糠秕,

所行的如碎秸,毫无价值。

你们的气息会像火一样烧灭你们自己。

12列邦必被烧成灰烬,

好像割下的荆棘被火焚烧。”

13远方的人啊,

要听一听我的作为。

近处的人啊,

要承认我的大能。

14锡安的罪人恐惧,

不敬虔的人颤抖。

他们说:“我们谁能住在烈火中呢?

谁能住在永不止息的火焰里呢?”

15秉公行义、说话正直、

憎恶不义之财、不受贿赂、

掩耳不听害人之谋、

闭眼不看邪恶之事的人,

16才可以住在高处。

他们的堡垒是坚固的磐石,

他们必不会绝粮断水。

17你们必目睹君王的荣美,

看到辽阔的土地,

18你们必想起以往可怕的情景,

说:“登记人口的在哪里?

收贡银的在哪里?

数城楼的在哪里?”

19你们再也看不见那些残暴之徒了,

他们的言语奇怪、陌生、

无法听懂。

20你们看锡安——我们守节期的城!

你们必看见耶路撒冷成为安宁之地,

像一个永不挪移的帐篷,

橛子永不拔出,

绳索也不会断。

21在那里,威严的耶和华必与我们同在。

那里必如巨川大河流经之地,

敌人的大小船只都无法穿过。

22因为耶和华是我们的审判官,

是我们的立法者,

是我们的君王,

是我们的拯救者。

23敌人的帆索松开,

桅杆晃动不稳,

风帆无法扬起。

那时,大量的战利品将被瓜分,

甚至瘸子都分得一份。

24耶路撒冷必没有居民说:

“我生病了”,

城中百姓的罪恶必得到赦免。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 33:1-24

Taabu Na Msaada

133:1 Hab 2:8; Yer 30:16; Eze 39:10; 2Fal 19:21; Isa 31:8; 21:2; Mt 7:2Ole wako wewe, ee mharabu,

wewe ambaye hukuharibiwa!

Ole wako, ee msaliti,

wewe ambaye hukusalitiwa!

Utakapokwisha kuharibu,

utaharibiwa;

utakapokwisha kusaliti,

utasalitiwa.

233:2 Za 13:5; Isa 59:16; 25:9; 5:30; Ezr 9:8; Mwa 43:29; Isa 40:10Ee Bwana, uturehemu,

tunakutamani.

Uwe nguvu yetu kila asubuhi

na wokovu wetu wakati wa taabu.

333:3 Za 12:5; Hes 10:35; Za 46:6; 68:33; Isa 59:16-18Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia;

unapoinuka, mataifa hutawanyika.

433:4 Hes 14:3; 2Fal 7:16; Isa 17:5; Yoe 3:13Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,

kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.

533:5 Za 97:9; Isa 5:16; 28:6; Ay 16:19; Isa 9:7; 1:26Bwana ametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,

ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

633:6 Isa 12:2; Mt 6:33; Mit 1:7; Mwa 39:3; Ay 22:25; 1Sam 11:2-3Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,

ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;

kumcha Bwana ni ufunguo wa hazina hii.

733:7 Isa 10:34; 2Fal 18:37Angalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani,

wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

833:8 Amu 5:6; Isa 30:21; 60:15; Zek 7:14; 2Fal 18:14Njia kuu zimeachwa,

hakuna wasafiri barabarani.

Mkataba umevunjika,

mashahidi wake wamedharauliwa,33:8 Au: miji yake imedharauliwa.

hakuna yeyote anayeheshimiwa.

933:9 Isa 3:26; 2Fal 19:23; Isa 24:4; 3:26; Yer 22:6; Kum 32:35-43; Mik 7:14Ardhi inaomboleza33:9 Au: Ardhi inakauka. na kuchakaa,

Lebanoni imeaibika na kunyauka,

Sharoni ni kama Araba,

nayo Bashani na Karmeli

wanapukutisha majani yao.

1033:10 Isa 33:3; 2:21; 5:16“Sasa nitainuka,” asema Bwana.

“Sasa nitatukuzwa;

sasa nitainuliwa juu.

1133:11 Za 7:14; Yak 1:5; Isa 26:18; 59:4Mlichukua mimba ya makapi,

mkazaa mabua,

pumzi yenu ni moto uwateketezao.

1233:12 Amo 2:1; Isa 5:6; 10:17; 27:11Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,

kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”

1333:13 Za 48:10; Isa 48:16; 49:1Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;

ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu!

1433:14 Isa 32:11; Zek 13:9; Ebr 12:29; Isa 30:30; 1:28-31Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,

kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:

“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?

Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

1533:15 Za 15:2; 119:37; Isa 58:8; Za 24:4; Eze 22:13; Mit 15:27Yeye aendaye kwa uadilifu

na kusema lililo haki,

yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma

na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,

yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,

na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

1633:16 Isa 25:4; Za 18:1-2; Isa 65:13; Kum 32:13; Isa 48:21; 49:10huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,

ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.

Atapewa mkate wake,

na maji yake hayatakoma.

1733:17 Isa 6:5; 4:2; 26:10Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake

na kuiona nchi inayoenea mbali.

1833:18 1Kor 1:20; Isa 17:14; 2:15Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:

“Yuko wapi yule afisa mkuu?

Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?

Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”

1933:19 Mwa 11:7; Yer 5:15; Isa 28:11Hutawaona tena wale watu wenye kiburi,

wale watu wenye usemi wa mafumbo,

wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.

2033:20 Isa 32:18; Za 46:5; 125:1-2; Mwa 26:22; Isa 41:18; 48:18Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;

macho yenu yatauona Yerusalemu,

mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa,

nguzo zake hazitangʼolewa kamwe,

wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.

2133:21 Kut 17:6; Nah 3:8; Zek 2:5; Isa 10:34Huko Bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu.

Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.

Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,

wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

2233:22 Yak 4:12; Mt 21:5; Isa 11:4; Za 89:18; Isa 2:3Kwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu,

Bwana ndiye mtoa sheria wetu,

Bwana ni mfalme wetu,

yeye ndiye atakayetuokoa.

2333:23 2Fal 7:8-16Kamba zenu za merikebu zimelegea:

Mlingoti haukusimama imara,

nalo tanga halikukunjuliwa.

Wingi wa mateka yatagawanywa,

hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.

2433:24 Hes 23:21; Rum 11:27; 1Yn 1:7-9; Isa 30:26; 2Nya 6:21; Yer 31:34; 33:18Hakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;

nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.