Daily Manna for Wednesday, May 25, 2022

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Yeremia 17:5-8

17:5 Za 108:12; Isa 30:1-3; 2:22; 2Kor 1:9Hili ndilo asemalo Bwana:

“Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu,

ategemeaye mwenye mwili

kwa ajili ya nguvu zake,

ambaye moyo wake

umemwacha Bwana.

17:6 Kum 29:23; Za 107:34; Ay 20:17; 20:17; 30:3; 39:6; Yer 48:9Atakuwa kama kichaka cha jangwani;

hataona mafanikio yatakapokuja.

Ataishi katika sehemu zisizo na maji,

katika nchi ya chumvi ambapo

hakuna yeyote aishiye humo.

17:7 Mit 16:20; Za 146:5; 34:8; 40:4; Yer 39:18“Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika Bwana,

ambaye matumaini yake ni katika Bwana.

17:8 Yer 14:1-6; Eze 47:12; Ay 14:9; Za 92:12-14; Eze 19:10Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.

Hauogopi wakati wa joto ujapo;

majani yake ni mabichi daima.

Hauna hofu katika mwaka wa ukame

na hautaacha kuzaa matunda.”