Daily Manna for Monday, May 23, 2022

Daily Manna is a daily Bible devotional service provided by Biblica. The Scripture is provided in many forms and is new every day. It is a great way to receive the encouragement and hope found in the Word of God.

Verse of the Day

Zaburi 91:1-6

Zaburi 91

91:1 Kut 33:2; Isa 49:2; Mao 4:20; Za 63:7Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

91:2 Za 9:9; 91:9; 2Sam 22:2, 3Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

91:3 Za 124:7; Mit 6:5; 1Fal 8:37Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

91:4 Za 61:4; 17:8; 35:2; Rum 2:12; Kum 32:10; Isa 27:3; 31:5; Zek 12:8Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mbawa zake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

91:5 Ay 5:21; 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

wala maradhi ya kuambukiza

yanayonyemelea gizani,

wala tauni iharibuyo adhuhuri.