Neno: Bibilia Takatifu

Matayo 10

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili

1Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. 10 Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.

11 “Mkiingia katika mji au kijiji cho chote, mtafuteni mtu mwaminifu mkae kwake mpaka mtakapoondoka. 12 Kila nyumba mtakay oingia, toeni salamu. 13 Kama watu wa nyumba hiyo wanastahili, amani yenu na ikae kwao; na kama hawastahili, amani yenu itawaru dia ninyi. 14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”

Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu. 21 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanae auawe. Watoto nao wataasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka. 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwa maana nawaambieni hakika, hamtamaliza kuipitia miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajafika.

24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25 Inatosha ikiwa mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamethubutu kum wita bwana mwenye nyumba Beelzebuli, je, si watawasema vibaya zaidi jamaa ya mwenye nyumba?”

Anayestahili Kuogopwa

27 Ninalo waambia gizani, ninyi litamkeni mwangani: na lile mnalosikia likinong’onwa, litangazeni mkiwa mmesimama kwenye paa la nyumba. 28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehena. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 32 Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Lakini ye yote atakayenikana mbele ya watu, mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”

Gharama Ya Kumfuata Yesu

34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita. 35 Kwa maana nimekuja kuleta kutokuele wana kati ya mtu na baba yake, na kati ya binti na mama yake, na kati ya mkwe na mama mkwe wake. 36 Na maadui wakubwa wa mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake. 37 Ye yote anayempenda baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Na ye yote ampendaye mwanae au binti yake kuliko anavyoni penda mimi, hastahili kuwa wangu. 38 Na ye yote asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 39 Ata kayeng’ang’ania nafsi yake ataipoteza lakini aipotezae nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.”

Watakaopokea Tuzo

40 “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye ali yenituma. 41 Mtu anayemkaribisha nabii kwa kuwa ni nabii, atapo kea tuzo ya nabii; na mtu anayemkaribisha mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea tuzo ya mwenye haki. 42 Na mtu ata kayetoa japo kikombe cha maji kwa mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, basi ninawaambieni hakika, hatakosa tuzo yake.”

New International Version - UK

Matthew 10

Jesus sends out the Twelve

1Jesus called his twelve disciples to him and gave them authority to drive out impure spirits and to heal every disease and illness.

These are the names of the twelve apostles: first, Simon (who is called Peter) and his brother Andrew; James son of Zebedee, and his brother John; Philip and Bartholomew; Thomas and Matthew the tax collector; James son of Alphaeus, and Thaddaeus; Simon the Zealot and Judas Iscariot, who betrayed him.

These twelve Jesus sent out with the following instructions: ‘Do not go among the Gentiles or enter any town of the Samaritans. Go rather to the lost sheep of Israel. As you go, proclaim this message: “The kingdom of heaven has come near.” Heal those who are ill, raise the dead, cleanse those who have leprosy,[a] drive out demons. Freely you have received; freely give.

‘Do not get any gold or silver or copper to take with you in your belts – 10 no bag for the journey or extra shirt or sandals or a staff, for the worker is worth his keep. 11 Whatever town or village you enter, search there for some worthy person and stay at their house until you leave. 12 As you enter the home, give it your greeting. 13 If the home is deserving, let your peace rest on it; if it is not, let your peace return to you. 14 If anyone will not welcome you or listen to your words, leave that home or town and shake the dust off your feet. 15 Truly I tell you, it will be more bearable for Sodom and Gomorrah on the day of judgment than for that town.

16 ‘I am sending you out like sheep among wolves. Therefore be as shrewd as snakes and as innocent as doves. 17 Be on your guard; you will be handed over to the local councils and be flogged in the synagogues. 18 On my account you will be brought before governors and kings as witnesses to them and to the Gentiles. 19 But when they arrest you, do not worry about what to say or how to say it. At that time you will be given what to say, 20 for it will not be you speaking, but the Spirit of your Father speaking through you.

21 ‘Brother will betray brother to death, and a father his child; children will rebel against their parents and have them put to death. 22 You will be hated by everyone because of me, but the one who stands firm to the end will be saved. 23 When you are persecuted in one place, flee to another. Truly I tell you, you will not finish going through the towns of Israel before the Son of Man comes.

24 ‘The student is not above the teacher, nor a servant above his master. 25 It is enough for students to be like their teachers, and servants like their masters. If the head of the house has been called Beelzebul, how much more the members of his household!

26 ‘So do not be afraid of them, for there is nothing concealed that will not be disclosed, or hidden that will not be made known. 27 What I tell you in the dark, speak in the daylight; what is whispered in your ear, proclaim from the roofs. 28 Do not be afraid of those who kill the body but cannot kill the soul. Rather, be afraid of the One who can destroy both soul and body in hell. 29 Are not two sparrows sold for a penny? Yet not one of them will fall to the ground outside your Father’s care.[b] 30 And even the very hairs of your head are all numbered. 31 So don’t be afraid; you are worth more than many sparrows.

32 ‘Whoever acknowledges me before others, I will also acknowledge before my Father in heaven. 33 But whoever disowns me before others, I will disown before my Father in heaven.

34 ‘Do not suppose that I have come to bring peace to the earth. I did not come to bring peace, but a sword. 35 For I have come to turn

‘“a man against his father,
    a daughter against her mother,
a daughter-in-law against her mother-in-law –
36     a man’s enemies will be the members of his own household.”[c]

37 ‘Anyone who loves their father or mother more than me is not worthy of me; anyone who loves their son or daughter more than me is not worthy of me. 38 Whoever does not take up their cross and follow me is not worthy of me. 39 Whoever finds their life will lose it, and whoever loses their life for my sake will find it.

40 ‘Anyone who welcomes you welcomes me, and anyone who welcomes me welcomes the one who sent me. 41 Whoever welcomes a prophet as a prophet will receive a prophet’s reward, and whoever welcomes a righteous person as a righteous person will receive a righteous person’s reward. 42 And if anyone gives even a cup of cold water to one of these little ones who is my disciple, truly I tell you, that person will certainly not lose their reward.’

Notas al pie

  1. Matthew 10:8 The Greek word traditionally translated leprosy was used for various diseases affecting the skin.
  2. Matthew 10:29 Or will; or knowledge
  3. Matthew 10:36 Micah 7:6