Zekaria 12 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zekaria 12:1-14

Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa

112:1 Mwa 1:8; Za 102:25; 104:2; Yer 51:15; Ebr 1:10; Isa 57:16; Ebr 12:9Hili ni neno la Bwana kuhusu Israeli. Bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: 212:2 Za 78:5; 60:3; Isa 51:23; Zek 14:14“Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia. 312:3 Isa 28:16; 29:8; 66:18; Zek 14:2; Dan 2:34-35; Mt 21:44Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. 412:4 Za 76:6; Zek 10:5Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asema Bwana. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa. 512:5 Eze 30:24Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’

612:6 Isa 10:17-18; Zek 11:1; 14:10; Oba 1:18“Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.

712:7 Yer 30:18; Amo 9:11Bwana atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. 812:8 Za 91:4; 82:6; Yoe 3:10, 16; Zek 9:15; Mik 7:8Katika siku hiyo, Bwana atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Bwana akiwatangulia. 912:9 Isa 29:7; Zek 1:21; 14:2-3; 1Kor 1:27-31Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.

Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki

1012:10 Eze 37:9; 39:29; Isa 44:3; Yoe 2:28-29; Za 22:16; Yn 19:34-37; Amu 11:34; Mwa 21:16; Yer 31:19; Yoe 2:28; Lk 2:35; Ufu 1:7“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema12:10 Au: Roho wa neema. na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 1112:11 Yer 50:4; 2Fal 23:29; Mdo 2:37; 2Nya 35:24Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. 1212:12 Mt 24:30; Ufu 1:7Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao, 13ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, 1412:14 Zek 7:3na koo zote zilizobaki na wake zao.

New International Version – UK

Zechariah 12:1-14

Jerusalem’s enemies to be destroyed

1A prophecy: the word of the Lord concerning Israel.

The Lord, who stretches out the heavens, who lays the foundation of the earth, and who forms the human spirit within a person, declares: 2‘I am going to make Jerusalem a cup that sends all the surrounding peoples reeling. Judah will be besieged as well as Jerusalem. 3On that day, when all the nations of the earth are gathered against her, I will make Jerusalem an immovable rock for all the nations. All who try to move it will injure themselves. 4On that day I will strike every horse with panic and its rider with madness,’ declares the Lord. ‘I will keep a watchful eye over Judah, but I will blind all the horses of the nations. 5Then the clans of Judah will say in their hearts, “The people of Jerusalem are strong, because the Lord Almighty is their God.”

6‘On that day I will make the clans of Judah like a brazier in a woodpile, like a flaming torch among sheaves. They will consume all the surrounding peoples right and left, but Jerusalem will remain intact in her place.

7‘The Lord will save the dwellings of Judah first, so that the honour of the house of David and of Jerusalem’s inhabitants may not be greater than that of Judah. 8On that day the Lord will shield those who live in Jerusalem, so that the feeblest among them will be like David, and the house of David will be like God, like the angel of the Lord going before them. 9On that day I will set out to destroy all the nations that attack Jerusalem.

Mourning for the one they pierced

10‘And I will pour out on the house of David and the inhabitants of Jerusalem a spirit12:10 Or the Spirit of grace and supplication. They will look on12:10 Or to me, the one they have pierced, and they will mourn for him as one mourns for an only child, and grieve bitterly for him as one grieves for a firstborn son. 11On that day the weeping in Jerusalem will be as great as the weeping of Hadad Rimmon in the plain of Megiddo. 12The land will mourn, each clan by itself, with their wives by themselves: the clan of the house of David and their wives, the clan of the house of Nathan and their wives, 13the clan of the house of Levi and their wives, the clan of Shimei and their wives, 14and all the rest of the clans and their wives.