Zaburi 128
Thawabu Ya Kumtii Bwana
Wimbo wa kwenda juu.
1128:1 Za 103:11; 119:1-3Heri ni wale wote wamchao Bwana,
waendao katika njia zake.
2128:2 Za 58:11; 109:11; Isa 3:10; Mwa 39:3; Mit 10:22Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3128:3 Mwa 49:22; Ay 29:5; Mit 5:15; Eze 19:10; Za 52:8; 144:12Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4128:4 Za 1:1; 112:1Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Bwana.
5128:5 Za 122:9; 134:3Bwana na akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6128:6 Mwa 50:23; 48:11; Za 125:5nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.
الْمَزْمُورُ الْمِئَةُ وَالثَّامِنُ وَالْعِشْرُونَ
تَرْنِيمَةُ الْمَصَاعِدِ
1طُوبَاكَ يَا مَنْ تَتَّقِي الرَّبَّ وَتَسْلُكُ فِي طُرُقِهِ. 2لأَنَّكَ تَأْكُلُ مِنْ تَعَبِ يَدَيْكَ وَتَتَمَتَّعُ بِالسَّعَادَةِ وَالْخَيْرِ. 3تَكُونُ امْرَأَتُكَ كَكَرْمَةٍ مُثْمِرَةٍ فِي جَوَانِبِ بَيْتِكَ، وَأَبْنَاؤُكَ كَأَغْرَاسِ الزَّيْتُونِ حَوْلَ مَائِدَتِكَ. 4هَكَذَا يُبَارَكُ الرَّجُلُ الَّذِي يَتَّقِي الرَّبَّ. 5يُبَارِكُكَ الرَّبُّ مِنْ صِهْيَوْنَ، حَتَّى تَشْهَدَ خَيْرَ أُورُشَلِيمَ كُلَّ أَيَّامِ حَيَاتِكَ، 6وَتَعِيشَ لِتَرَى أَحْفَادَكَ. وَلْيَكُنْ لِشَعْبِ إِسْرَائِيلَ سَلامٌ.