Yoshua 13 – NEN & NIRV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yoshua 13:1-33

Sehemu Za Kanaani Ambazo Hazijatwaliwa

113:1 Mwa 24:1; Yos 14:10; 23:1-3; 1Fal 1:1Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, Bwana akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa.

213:2 Mwa 10:14; Amu 3:31; Yos 12:5“Nchi iliyosalia ni hii: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: 313:3 1Nya 13:5; Isa 23:3; Yer 2:18; Yos 15:11; 19:43; Amu 1:18; 1Sam 5:10; 7:14; Amu 3:3; 16:5, 18; 1Sam 6:4, 17; Isa 14:29; Eze 25:15; Yos 11:22; Amo 3:9; Amu 14:19; 2Sam 1:20; Kum 2:23; 13:4; Yos 12:18; Mwa 14:7; 15:16kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani (maeneo yale matano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi); 4kuanzia kusini, nchi yote ya Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na eneo la Waamori, 513:5 1Fal 5:18; Za 83:7; Eze 27:9; Yos 11:17; Kum 3:8; Hes 13:21; 34:8; Amu 3:3eneo la Wagebali;13:5 Yaani eneo la Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Lebanoni yote kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi.

613:6 Yos 11:8; Za 80:8; Hes 33:54; 34:13; Amu 2:12; Yos 14:1, 2“Na kuhusu wakaaji wote katika maeneo ya milima, kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza watoke mbele ya Waisraeli. Hakikisha umegawa nchi hii kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuagiza, 713:7 Yos 11:23; Za 78:55sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Mwa Yordani

813:8 Yos 12:6; 18:7; Hes 32:33; Kum 3:12; Yos 12:6; 18:7Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa Bwana alivyowagawia.

913:9 Hes 32:34; Kum 2:36; Amu 11:26; 2Sam 24:5; Yer 48:8, 21; Hes 21:30; 32:3; Isa 15:2Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, likijumlisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni, 1013:10 Yos 12:2; Hes 21:24nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamoni. 1113:11 Yos 12:2-5Vilevile ilijumlisha Gileadi, eneo la Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote ikienea hadi Saleka: 1213:12 Kum 1:4; Yos 12:4; Mwa 14:5; Kum 3:5, 11; Hes 21:24yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao. 1313:13 Yos 12:5; Kum 3:12-15Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii.

1413:14 Kum 18:1-2; Yos 14:2; Hes 18:20; Kum 10:9Lakini kwa kabila la Lawi, Mose hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa Bwana, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.

15Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo:

1613:16 Yos 12:2; 1Sam 30:28; Hes 21:30; Isa 15:2; Kum 3:12Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba 1713:17 Hes 32:3; 22:41; 1Nya 5:8; Yer 48:23; Eze 25:9hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, 1813:18 Hes 21:23; Kum 2:26; Yos 21:37; Yer 48:21Yahasa, Kedemothi, Mefaathi, 1913:19 Hes 32:37; 32:3Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, 2013:20 Kum 3:29Beth-Peori, materemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi: 2113:21 Mwa 25:2; Hes 25:15; 31:8; Kum 3:10; Hes 21:24; 31:8miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni. Mose alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile. 2213:22 Hes 22:5; Mwa 30:27; Hes 23:23; 2Pet 2:15; Ufu 2:14Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemuua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa mchawi. 2313:23 1Nya 5:7Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii na vijiji vyake ndiyo iliyokuwa urithi wa Wareubeni ukoo kwa ukoo.

24Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:

2513:25 Hes 21:32; Yos 21:39; 12:2; Kum 3:11; Amu 11:13; 2Sam 11:1; 12:26Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni iliyoenea hadi Aroeri, karibu na Raba; 2613:26 Hes 21:25; Yer 49:3; Mwa 32:2; Yos 10:3na kuanzia Heshboni mpaka Ramath-Mispa na Betonimu, na kutoka Mahanaimu hadi eneo la Debiri; 2713:27 Hes 32:3; Mwa 33:17; Amu 12:1; Za 48:2; Hes 34:11; 1Fal 7:46; Kum 3:17; Yos 11:2; Mt 14:34; Lk 5:1na katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki mwa Mto Yordani, eneo inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi13:27 Yaani Bahari ya Galilaya.). 2813:28 Mwa 46:16; Hes 32:3; Eze 48:27Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Gadi ukoo kwa ukoo.

29Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo:

3013:30 Mwa 32:2; Hes 21:33; Yos 12:4; Hes 32:41Eneo lililoenea kuanzia Mahanaimu, na kujumlisha Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini, 3113:31 Hes 21:33; Mwa 50:23; Yos 17:5nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.

3213:32 Hes 26:3; 22:1Huu ndio urithi alioupeana Mose wakati alipokuwa katika tambarare za Moabu, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko. 3313:33 Hes 26:62; 18:20; Yos 18; 7; Eze 44:28Lakini kwa kabila la Walawi, Mose hakuwapa urithi; Bwana Mungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

New International Reader’s Version

Joshua 13:1-33

The Land That Remained to Be Taken Over

1Joshua was now very old. The Lord said to him, “You are very old. And there are still very large areas of land that have not yet been taken over.

2“Here is the land that remains to be taken over.

“It includes all the areas of Philistia and Geshur. 3Those areas begin at the Shihor River in the eastern part of Egypt. They go to the territory of Ekron in the north. All that land is considered Canaanite even though it is controlled by five Philistine rulers. They rule over Gaza, Ashdod, Ashkelon, Gath and Ekron.

The Avvites 4live south of them.

The rest of the land of Canaan that remains to be taken over reaches from Arah all the way to Aphek. Arah belongs to the people of Sidon. The land that remains to be taken reaches the border of Amorite territory.

5It includes the area of Byblos.

It also includes all of Lebanon to the east. It reaches from Baal Gad below Mount Hermon all the way to Lebo Hamath.

6“I myself will drive out all the people who live in the mountain areas. Those areas reach from Lebanon to Misrephoth Maim. They include the area where all the people of Sidon live. I myself will drive out those people to make room for the Israelites. Make sure you set that land apart for Israel. Give it to them as their share, just as I have directed you. 7Divide it up among the nine tribes and half of the tribe of Manasseh. Give each tribe its share.”

Land for the Tribes East of the Jordan River

8The other half of Manasseh’s tribe had already received the share of land Moses had given them. Their share was east of the Jordan River. The tribes of Reuben and Gad had already received their share too. Moses, the servant of the Lord, had given it to them.

9That land starts at Aroer on the rim of the Arnon River valley. It includes the town in the middle of the valley. It includes the high plains of Medeba all the way to Dibon. 10It also includes all the towns of Sihon, the king of the Amorites. He had ruled in Heshbon. That area reaches to the border of Ammon.

11It also includes Gilead. It includes the territory of Geshur and Maakah. It includes Mount Hermon and the whole land of Bashan all the way to Salekah. 12So it includes the entire kingdom of Og in Bashan. Og had ruled in Ashtaroth and Edrei. He was the last of the Rephaites. Moses had won the battle over Sihon and Og. He had taken over their land. 13But the Israelites didn’t drive out the people of Geshur and Maakah. So they continue to live among the Israelites to this day.

14Moses hadn’t given any share of the land to the tribe of Levi. That’s because the food offerings are their share. Those offerings are presented to the Lord, the God of Israel. Moses gave the Levites what he had promised them.

15Here is what Moses had given to the tribe of Reuben, according to its family groups.

16Their territory starts at Aroer on the rim of the Arnon River valley. It includes the town in the middle of the valley. It includes all of the high plains near Medeba. 17It includes Heshbon and all its towns on those plains. Those towns include Dibon, Bamoth Baal, Beth Baal Meon, 18Jahaz, Kedemoth and Mephaath. 19They include Kiriathaim, Sibmah and Zereth Shahar on the hill in the valley. 20They also include Beth Peor, Beth Jeshimoth and the slopes of Pisgah. 21All those towns are on the high plains. The territory includes the whole kingdom of Sihon, the king of the Amorites. He had ruled in Heshbon. Moses had won the battle over him and over the chiefs of Midian. Those chiefs were Evi, Rekem, Zur, Hur and Reba. They were princes who helped Sihon fight against Israel. They lived in that country. 22The Israelites killed many of them in battle. They also killed Balaam with their swords. He was the son of Beor. Balaam had used evil magic to find out what was going to happen.

23The border of the tribe of Reuben was the bank of the Jordan River. All those towns and their villages were given to the tribe of Reuben as their very own. Each family group received its share.

24Here is what Moses had given to the tribe of Gad, according to its family groups.

25Their territory includes Jazer and all the towns of Gilead. It includes half of the country of Ammon all the way to Aroer, which was near Rabbah. 26Their territory reaches from Heshbon to Ramath Mizpah and Betonim. It reaches from Mahanaim to the territory of Debir. 27In the valley their land includes Beth Haram, Beth Nimrah, Sukkoth and Zaphon. It also includes the rest of the kingdom of Sihon. He was the king of Heshbon. His kingdom included the east side of the Jordan River. It reached up to the south end of the Sea of Galilee.

28All those towns and their villages were given to the tribe of Gad as their very own. Each family group received its share.

29Here is what Moses had given to half of the tribe of Manasseh, according to its family groups. It’s what Moses had given to half of Manasseh’s family line.

30Their territory starts at Mahanaim. It includes the whole land of Bashan. That was the entire kingdom of Og, the king of Bashan. Manasseh’s territory includes all the 60 towns of Jair in Bashan. 31It includes half of the land of Gilead. It also includes Ashtaroth and Edrei. They were the royal cities of Og in Bashan.

That land was given to half of the family line of Makir. He was the son of Manasseh. Each family group received its share.

32Those were the shares of land Moses had given the eastern tribes when he was in the plains of Moab. The plains are across the Jordan River east of Jericho. 33But Moses hadn’t given any share to the tribe of Levi. The Lord, the God of Israel, is their share. Moses gave the Levites what he had promised them.