Yohana 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 8:1-59

Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini

18:1 Mt 21:1Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni. 28:2 Mt 26:55Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha. 3Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. 4Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 58:5 Kum 22:22; Ay 31:11Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” 68:6 Mt 22:15-18; 12:10Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki.

Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. 78:7 Kum 17:7; Eze 16:40; Rum 2:1, 22Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” 8Akainama tena na kuandika ardhini.

98:9 Rum 2:22Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. 10Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”

118:11 Yn 3:17; 5:14Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.”

Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]

Yesu Nuru Ya Ulimwengu

128:12 Yn 6:35; 12:35; Mit 4:18; Mt 5:14Kisha Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”

138:13 Yn 5:31Mafarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.”

148:14 Yn 13:3; 16:28; 7:28; 9:29Yesu akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli kwa sababu najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. 158:15 Yn 7:24; 3:17Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu, mimi simhukumu mtu yeyote. 168:16 Yn 5:30Lakini hata kama nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma. 17Imeandikwa katika Sheria yenu kwamba, ushahidi wa watu wawili ni thabiti. 188:18 Yn 5:37Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.”

198:19 Yn 16:3; 14:7; 1Yn 2:23Ndipo wakamuuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?”

Yesu akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hammfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.” 208:20 Mt 26:18, 55; Mk 12:41; Yn 7:30Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia.

Yesu Atabiri Kifo Chake Mwenyewe

218:21 Eze 3:18; Yn 7:34; 13:33Yesu akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi ninyi hamwezi kuja.”

228:22 Yn 7:35Ndipo wale Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Je, hii ndiyo sababu amesema, ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kuja’?”

238:23 Yn 3:31; 17:14Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini, mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. 248:24 Yn 4:26; 13:19Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu, kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”

258:25 Yn 8:14Wakamuuliza, “Wewe ni nani?”

Naye Yesu akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo. 268:26 Yn 7:28; 3:32; 15:15Nina mambo mengi ya kusema juu yenu na mengi ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kweli, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.”

27Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni. 288:28 Yn 3:14; 5:19Kisha Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua juu Mwana wa Adamu, ndipo mtakapojua kuwa, ‘Mimi ndiye yule niliyesema na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu bali ninasema yale tu ambayo Baba yangu amenifundisha. 298:29 Yn 16:32; Isa 50:5; Yn 4:34Yeye aliyenituma yu pamoja nami, hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.’ ” 308:30 Yn 7:31Wengi waliomsikia Yesu akisema maneno haya wakamwamini.

Wanafunzi Wa Kweli

318:31 Yn 15:7; 2Yn 9Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. 328:32 Gal 5:1, 13; Yak 2:12Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

338:33 Mk 3:9; Lk 3:8Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Abrahamu, nasi hatujawa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”

348:34 Rum 6:16; 2Pet 2:19Yesu akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 358:35 Gal 4:30Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. 368:36 Rum 8:2; Gal 5:1Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. 378:37 Yn 7:19; 8:40Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Abrahamu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu. 388:38 Yn 5:19, 30; 14:10, 24Ninasema yale niliyoyaona mbele za Baba yangu, nanyi inawapa kufanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.”

Yesu Na Abrahamu

398:39 Lk 3:8; Gal 3:7Wakajibu, “Baba yetu ni Abrahamu.”

Yesu akawaambia, “Kama mngekuwa wazao wa Abrahamu mngefanya mambo yale aliyofanya Abrahamu. 408:40 Yn 8:37; 8:26Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu, Abrahamu hakufanya jambo la namna hii. 418:41 Isa 63:16; 64:8; Mal 1:6Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.”

Wakamjibu, “Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee.”

428:42 1Yn 5:1; Yn 16:27; 7:28; 3:17Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. 438:43 Yn 7:17Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. 448:44 1Yn 3:8; 2Nya 18:21; Za 12:2Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. 458:45 Yn 18:37Lakini kwa sababu nimewaambia kweli hamkuniamini! 468:46 2Kor 5:21; 1Pet 2:22Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? 478:47 Yn 18:37; 1Yn 4:6Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”

Maelezo Ya Yesu Kuhusu Yeye Mwenyewe

488:48 Mt 10:5; Mk 3:22; Yn 7:20Wayahudi wakamjibu Yesu, “Je, hatuko sahihi tunaposema ya kwamba wewe ni Msamaria na ya kwamba una pepo mchafu?”

49Yesu akawajibu, “Mimi sina pepo mchafu, bali ninamheshimu Baba yangu, nanyi mnanidharau. 508:50 Yn 7:20; 8:54; 10:20Lakini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi. 518:51 Yn 11:26Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.”

528:52 Zek 1:5; Ebr 11:13Ndipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Abrahamu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema ‘Mtu akitii neno langu hatakufa milele.’ 538:53 Yn 4:12Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa na manabii ambao nao pia walikufa? Hivi wewe unajifanya kuwa nani?”

548:54 Yn 16:14; 17:1-5Yesu akawajibu, “Kama nikijitukuza utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi. 558:55 Yn 7:28-29; 15:10Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake. 568:56 Mwa 18:18; Mt 13:17; Ebr 11:13Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.”

57Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, wewe wasema umemwona Abrahamu?”

588:58 Yn 1:2; 17:5, 24; Kut 3:14; 6:3Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’ ” 598:59 1Sam 30:6; Yn 11:8; 12:36Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Yesu akajificha, naye akatoka Hekaluni.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

約翰福音 8:1-59

淫婦獲赦

1眾人都回家去了,耶穌卻上了橄欖山。 2第二天清晨,祂又回到聖殿。百姓聚集在祂那裡,祂就坐下來教導他們。 3這時候,律法教師和法利賽人帶來一個通姦時被捉的女人,讓她站在眾人面前, 4然後問耶穌:「老師,這個女人是在通姦時被捉到的。 5摩西的律法,我們要用石頭把她打死,你說該怎麼處置她呢?」

6他們這樣問是要使耶穌落在他們的圈套裡,可以有藉口控告祂。耶穌卻只是彎著腰用指頭在地上寫字。 7他們不斷地追問耶穌,於是祂直起腰來,對他們說:「你們中間誰沒有罪,誰就先拿石頭打她吧。」 8說完,又彎下腰在地上寫字。

9他們聽了這句話,就從老到少一個一個地走了,只剩下耶穌和那個女人在那裡。 10耶穌直起腰來,說:「婦人,他們到哪裡去了?沒有人定你的罪嗎?」

11她說:「主啊,沒有。」

耶穌說:「我也不定你的罪。回去吧,從今以後不要再犯罪了。」

世界的光

12耶穌又對眾人說:「我是世界的光,凡跟從我的,必不會走在黑暗裡,必要得到生命的光。」

13法利賽人對祂說:「你自己為自己做見證,你的見證不真實。」

14耶穌說:「即便我自己為自己做見證,我的見證仍是真實的,因為我知道自己從哪裡來、要到哪裡去,你們卻不知道我從哪裡來、要到哪裡去。 15你們只憑外表判斷別人,我卻不判斷人。 16就算我判斷人,我的判斷也是正確的,因為我不是獨自一人,還有差我來的父與我同在。 17你們的律法不是說兩個人做見證就有效嗎? 18我是自己為自己做見證,差我來的父也為我做見證。」

19他們問:「你的父在哪裡?」

耶穌回答說:「你們不認識我,也不認識我的父。如果你們認識我,也會認識我的父。」 20耶穌在聖殿的庫房這樣教導人,但沒有人抓祂,因為祂的時候還沒有到。

警告不信的人

21耶穌又對他們說:「我要走了,你們會尋找我,你們將死在自己的罪中。我去的地方,你們不能去。」

22猶太人說:「祂說祂去的地方我們不能去,難道祂想自殺嗎?」

23耶穌對他們說:「你們是從下面來的,我是從上面來的。你們屬於這世界,我不屬於這世界。 24所以我說你們將死在自己的罪中,你們如果不相信我就是8·24 耶稣用「我就是」這個詞提醒聽衆祂就是出埃及記3·14節提到的那位自有永有的上帝,8·28同。那一位,一定會死在自己的罪中。」

25他們問:「你到底是誰?」

耶穌回答說:「我不是早就告訴你們了嗎? 26關於你們,我有許多要說、要審判的,但差我來的那位是真實的,我把從祂那裡聽到的告訴世人。」 27他們不明白耶穌是指著父說的。

28於是耶穌說:「你們舉起人子以後,必知道我就是那一位,並且知道我沒有一件事是憑自己做的,我所說的都是父教導我的。 29差我來的那位跟我在一起,祂沒有撇下我,讓我孤單一人,因為我做的都是祂所喜悅的。」 30許多人因為這番話而信了耶穌。

真正的自由

31耶穌對信祂的猶太人說:「你們若持守我的道,就真是我的門徒了。 32你們必認識真理,真理必叫你們得到自由。」

33他們說:「我們是亞伯拉罕的子孫,從來沒有做過奴隸,你為什麼說我們可以得到自由呢?」

34耶穌說:「我實實在在地告訴你們,所有犯罪的人都是罪的奴隸。 35奴隸不能永遠留在主人的家裡,只有兒子才可以。 36所以,如果上帝的兒子釋放了你們,你們就真正自由了!

耶穌和亞伯拉罕

37「我知道你們是亞伯拉罕的子孫,但你們卻想殺我,因為你們心裡容不下我的道。 38我所說的,是我從父那裡看到的,你們卻照著你們父8·38 猶太文化中,「父」可指生身的父,亦可泛指祖先。的話去做。」

39他們說:「我們的父就是亞伯拉罕!」

耶穌說:「你們如果真是亞伯拉罕的子孫,一定會做他所做的事。 40我把從上帝那裡聽到的真理告訴你們,你們反要殺我,亞伯拉罕絕不做這樣的事。 41你們是在作你們父所做的事。」

他們說:「我們不是從淫亂生的!我們只有一位父,就是上帝。」

42耶穌說:「如果上帝是你們的父,你們一定會愛我,因為我來自上帝。如今我在這裡,我不是憑自己來的,而是上帝差我來的, 43你們為什麼不明白我的話呢?因為你們聽不進去我的道。 44你們是出於你們的父魔鬼,你們樂意順著牠的私慾行。魔鬼從起初就是個殺人兇手,從不站在真理這一邊,因為牠心裡根本沒有真理。撒謊是牠的本性,因為牠是撒謊者,又是撒謊者的始祖。 45所以,我講真理的時候,你們不信我。 46你們誰能指證我有罪呢?我既然把真理告訴了你們,你們為什麼還不信我呢? 47出於上帝的人聽上帝的話,你們不聽上帝的話,因為你們不是出於上帝。」

48猶太人對祂說:「我們說你是撒瑪利亞8·48 撒瑪利亞人血統不純,常被猶太人藐視,並當作罵人的話。,被鬼附身了,難道不對嗎?」

49耶穌說:「我沒有被鬼附身。我尊敬我的父,你們卻侮辱我。 50我不為自己尋求榮耀,但有一位會為我尋求,祂也會斷定誰是誰非。 51我實實在在地告訴你們,人如果遵行我的道,必永遠不死。」

52那些猶太人說:「現在我們的確知道你是被鬼附身了!亞伯拉罕和眾先知都死了,你還說人如果遵行你的道,必永遠不死。 53難道你比我們的祖先亞伯拉罕還大嗎?他死了,先知們也死了,你以為你是誰?」

54耶穌說:「如果我為自己爭取榮耀,那榮耀算不了什麼。但使我得榮耀的是我的父,你們也稱祂為你們的上帝。 55你們不認識祂,我卻認識祂。如果我說我不認識祂,那我就像你們一樣是說謊的。然而,我認識祂,並且遵行祂的道。 56你們的祖先亞伯拉罕曾經歡歡喜喜地盼望看到我來的日子。他看見了,就歡喜快樂。」

57猶太人說:「你還不到五十歲,怎麼會見過亞伯拉罕呢?」

58耶穌說:「我實實在在地告訴你們,亞伯拉罕還沒有出生,我就已經存在了8·58 我就已經存在了」希臘文是「我是」,參見8·24注。。」 59於是,他們就拿起石頭要打祂,耶穌卻避開他們,離開了聖殿。