Yohana 20 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 20:1-31

Kufufuka Kwa Yesu

(Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-8; Luka 24:1-12)

120:1 Lk 8:2; Yn 19:25; Mt 27:60, 66Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio. 220:2 Yn 13:23Hivyo akaja akikimbia kwa Simoni Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, na kusema, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na hatujui walikomweka!”

320:3 Lk 24:12Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara kuelekea kaburini. 4Wote wawili walikuwa wanakimbia, lakini yule mwanafunzi mwingine akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini. 520:5 Yn 20:11; 19:40Alipofika, akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani mle ndani, lakini hakuingia. 6Ndipo Simoni Petro akaja, akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini 720:7 Yn 11:44na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa mahali pa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda. 820:8 Yn 20:4Kisha yule mwanafunzi aliyetangulia kufika kaburini naye akaingia ndani, akaona, akaamini, 920:9 Mt 22:29; Yn 2:22; Lk 24:26; Mdo 2:24(kwa kuwa mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa kutoka Maandiko kwamba ilikuwa lazima Yesu afufuke kutoka kwa wafu).

10Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.

Yesu Anamtokea Maria Magdalene

(Mathayo 28:9-10; Marko 16:9-11)

1120:11 Yn 20:5Lakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini, 1220:12 Mk 16:5; Mdo 10:30naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni.

1320:13 Yn 20:2, 15Wakamuuliza Maria, “Mwanamke, mbona unalia?”

Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.” 1420:14 Mt 28:9; Mk 16:9; Lk 24:16; Yn 21:14Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Yesu amesimama, lakini hakumtambua.

1520:15 Yn 20:13Yesu akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?”

Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.”

1620:16 Yn 5:2; Mt 23:7Yesu akamwita, “Maria!”

Ndipo Maria akamgeukia Yesu na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (maana yake Mwalimu).

1720:17 Mt 28:10; Yn 7:33; Mt 28:10Yesu akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ”

1820:18 Yn 20:1; Lk 24:10, 22, 23Kwa hiyo Maria Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Yesu, akisema, “Nimemwona Bwana!” Naye akawaambia kwamba Yesu alikuwa amemweleza mambo hayo yote.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49)

19Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi. Naye Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!” 2020:20 Lk 24:36-39, 40; Yn 19:34; 16:20, 22; Lk 24:39, 40; Yn 19:34; 16:20Baada ya kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana.

2120:21 Yn 20:19; 3:17; Mt 28:19; Yn 17:18Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.” 2220:22 Mdo 19:2; Gal 3:2; Yn 7:39; Mdo 2:38; 8:15; 17; 19:2; Gal 3:2Naye alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 2320:23 Mt 16:19; 18:18Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa, na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa.”

Yesu Anamtokea Tomaso

2420:24 Yn 11:16Lakini Tomaso, aliyeitwa Didimasi, yaani Pacha, mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Yesu alipokuja. 2520:25 Mk 16:11Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana.”

Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.”

2620:26 Yn 14:27; 20:21Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Yesu akaja milango ikiwa imefungwa na kusimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 2720:27 Yn 20:25; Lk 24:40Kisha akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.”

2820:28 Yn 1:1; 20:29; 3:15; 1Pet 1:8Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”

2920:29 Yn 3:15; 1Pet 1:8Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”

Kusudi La Kitabu Hiki

3020:30 Yn 21:25; 2:11; 21:25; Mt 4; 3; 25:46Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. 3120:31 Yn 3:15; 19:35; Mt 4:3; 25:46Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo,20:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

约翰福音 20:1-31

耶稣复活

1周日清晨,天还未亮,抹大拉玛丽亚就来到坟墓前,发现封住墓口的石头已经挪开了。 2她赶快跑去告诉西门·彼得和耶稣所爱的那个门徒,说:“有人把主从坟墓里搬走了,不知放到哪里去了。”

3彼得和那个门徒听了就出去,往坟墓那边跑。 4两个人一起跑,但那个门徒比彼得跑得快,所以先到了坟墓。 5他并没有进去,只是探头往里看,看见细麻布还在那里。 6西门·彼得随后也来了,他进到里边,看到细麻布放在那里, 7耶稣的裹头巾则卷着放在另一处,没有和细麻布放在一起。 8先到的那个门徒也进来了,看见这种情形,就信了。 9因为他们还不明白圣经上有关耶稣必要从死里复活的话。 10然后,他们各自回家去了。

11玛丽亚却站在坟墓外面哭泣,边哭边往坟墓里面看, 12看见两个穿着白衣的天使分别坐在原来安放耶稣遗体的头脚两端。

13天使对她说:“妇人,你为什么哭呢?”

她说:“有人把我的主搬走了,不知道放在什么地方。” 14说完,她转过身来,看见耶稣站在那里,但她不知道那就是耶稣。

15耶稣问她:“妇人,你为什么哭?你在找谁?”

玛丽亚还以为祂是园丁,就说:“先生,如果是你把祂搬走了,请告诉我放在哪里了,我好搬回来。”

16耶稣说:“玛丽亚。”

玛丽亚立即转过头来用希伯来话对祂说:“拉波尼!”拉波尼的意思是老师。

17耶稣说:“不要拉着我,我还没有升到父那里。你先去找我的众弟兄,告诉他们我要升天去见我的父,也是你们的父;去见我的上帝,也是你们的上帝。”

18抹大拉玛丽亚就去向门徒报讯,说:“我看见主了!”又把主对她说的话告诉门徒。

向门徒显现

19当天晚上,即周日晚上,门徒因为害怕犹太人,把房门都关上了。忽然,耶稣来了,站在他们当中,对他们说:“愿你们平安!” 20说完,让他们看祂的手和肋旁。门徒看见主,十分欢喜。

21耶稣又说:“愿你们平安!父怎样差遣我,我也照样差遣你们。” 22然后祂向他们吹了一口气,说:“你们领受圣灵吧! 23你们赦免谁的罪,谁的罪就得到赦免;你们不赦免谁的罪,谁的罪就得不到赦免。”

向多马显现

24耶稣显现的时候,十二个门徒中绰号“双胞胎”的多马不在场。 25其他门徒告诉他:“我们看见主了!”可是多马说:“除非我亲眼看见祂手上的钉痕,用手摸到祂手上的钉痕和祂的肋旁,否则我决不信。”

26过了八天,门徒又聚在一起,多马也在,门都关着。突然耶稣来了,站在他们当中说:“愿你们平安!” 27然后对多马说:“把你的指头放在我手上摸摸看,伸出手来摸摸我的肋旁。不要怀疑,要信!”

28多马回答说:“我的主,我的上帝!”

29耶稣说:“你看见我才信,那些没有看见就信的人有福了。”

30耶稣在门徒面前还行了许多神迹,只是没有记在这本书里。 31而记载这些事的目的是为了使你们相信耶稣就是基督,是上帝的儿子,并且使你们这些信祂的人可以靠祂的名得到生命。