Yohana 12 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 12:1-50

Maria Ampaka Yesu Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)

112:1 Yn 11:55; Mt 21:17Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 212:2 Lk 10:38-42Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 312:3 Yn 11:12Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja12:3 Painti moja ni kama nusu lita. yenye manukato ya nardo12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

412:4 Mt 10:4Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 30012:5 Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300. na fedha hizo wakapewa maskini?” 612:6 Yn 13:29Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

712:7 Yn 19:40Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 812:8 Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Shauri La Kumuua Lazaro

912:9 Yn 11:43, 44Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua. 1012:10 Lk 16:31Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 1112:11 Yn 11:45; 12:18kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini.

Kuingia Kwa Yesu Yerusalemu Kwa Ushindi

(Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40)

1212:12 Mt 21:8; Mk 11:8; Lk 19:35, 36Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 1312:13 Za 118:25-26; Yn 1:49Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,

“Hosana!”12:13 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”

1412:14 Mt 21:7Yesu akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,

1512:15 Zek 9:9“Usiogope, Ewe binti Sayuni;

tazama, Mfalme wako anakuja,

amepanda mwana-punda!”

1612:16 Lk 18:34; Yn 7:39Wanafunzi wake Yesu mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

1712:17 Yn 11:42Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu, waliendelea kushuhudia. 1812:18 Yn 12:11; 19:37Ni kwa sababu pia walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu ndiyo maana umati wa watu ukaenda kumlaki. 1912:19 Yn 11:47, 48Hivyo Mafarisayo walipoona hayo wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”

Yesu Anatabiri Kifo Chake

2012:20 Yn 7:35; Mdo 11:20Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wamekwenda kuabudu wakati wa Sikukuu. 2112:21 Mt 11:21; Yn 1:44Hawa wakamjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Yesu.

2312:23 Yn 13:32; 17:1Yesu akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. 2412:24 1Kor 15:36Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi. 2512:25 Mk 8:35; Lk 14:26Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. 2612:26 Flp 1:23Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.

2712:27 Mt 26:38, 39; Lk 12:50; Yn 13:21; Lk 22:53; Yn 18:37“Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii.’ Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu. 2812:28 Mt 3:17Baba, litukuze jina lako.”

Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.” 2912:29 Lk 22:43Ule umati wa watu uliokuwa mahali pale uliisikia nao ukasema, “Hiyo ni sauti ya radi,” wengine wakasema, “Malaika ameongea naye.”

3012:30 Kut 19:9Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. 3112:31 Yn 16; 11; Efe 2:2; 1Yn 5:19Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. 3212:32 Isa 11:10; Yn 3:14; 6:44Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 3312:33 Yn 18:32; 21:19Yesu aliyasema haya akionyesha ni kifo gani atakachokufa.

3412:34 Za 110:4; Isa 9:7; Mt 8:20; Yn 3:14Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Sheria kwamba ‘Kristo12:34 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”

3512:35 Yn 1:9; 8:12; 9:5; Yer 13:16; Efe 5:8; 1Yn 2:11Ndipo Yesu akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakokwenda. 3612:36 Lk 16:8; Efe 5:8; 1The 5:5; 1Yn 2:9, 10, 11; Yn 8:59; 11:54Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka, akajificha wasimwone.

Wayahudi Waendelea Kutokuamini

3712:37 Yn 2:11Hata baada ya Yesu kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. 3812:38 Isa 53:1; Rum 10:16Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema:

“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu,

na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?”

3912:39 Isa 6:9, 10; Mt 13:14, 15Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:

4012:40 Isa 6:10; Mt 13:13, 15“Amewafanya vipofu,

na kuifanya mioyo yao kuwa migumu,

ili wasiweze kuona kwa macho yao,

wala kuelewa kwa mioyo yao,

wasije wakageuka nami nikawaponya.”

4112:41 Isa 6:1-4; Lk 24:27Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Yesu na kunena habari zake.

4212:42 Yn 7:48; 9:22Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi. 4312:43 Yn 5:44; Rum 2:29Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani

4412:44 Mt 10:40; Yn 5:24Yesu akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali yeye aliyenituma. 4512:45 Yn 14:9Yeyote anionaye mimi, amemwona yeye aliyenituma. 4612:46 Yn 3:19; 8:12Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kwamba kila mtu aniaminiye asibaki gizani.

4712:47 Yn 3:17“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. 4812:48 Yn 5:45Yuko amhukumuye yeye anikataaye mimi na kutokuyapokea maneno yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. 4912:49 Yn 14:31Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. 5012:50 Yn 8:26, 28Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”

King James Version

John 12:1-50

1Then Jesus six days before the passover came to Bethany, where Lazarus was which had been dead, whom he raised from the dead. 2There they made him a supper; and Martha served: but Lazarus was one of them that sat at the table with him. 3Then took Mary a pound of ointment of spikenard, very costly, and anointed the feet of Jesus, and wiped his feet with her hair: and the house was filled with the odour of the ointment. 4Then saith one of his disciples, Judas Iscariot, Simon’s son, which should betray him, 5Why was not this ointment sold for three hundred pence, and given to the poor? 6This he said, not that he cared for the poor; but because he was a thief, and had the bag, and bare what was put therein. 7Then said Jesus, Let her alone: against the day of my burying hath she kept this. 8For the poor always ye have with you; but me ye have not always. 9Much people of the Jews therefore knew that he was there: and they came not for Jesus’ sake only, but that they might see Lazarus also, whom he had raised from the dead.

10¶ But the chief priests consulted that they might put Lazarus also to death; 11Because that by reason of him many of the Jews went away, and believed on Jesus.

12¶ On the next day much people that were come to the feast, when they heard that Jesus was coming to Jerusalem, 13Took branches of palm trees, and went forth to meet him, and cried, Hosanna: Blessed is the King of Israel that cometh in the name of the Lord. 14And Jesus, when he had found a young ass, sat thereon; as it is written, 15Fear not, daughter of Sion: behold, thy King cometh, sitting on an ass’s colt. 16These things understood not his disciples at the first: but when Jesus was glorified, then remembered they that these things were written of him, and that they had done these things unto him. 17The people therefore that was with him when he called Lazarus out of his grave, and raised him from the dead, bare record. 18For this cause the people also met him, for that they heard that he had done this miracle. 19The Pharisees therefore said among themselves, Perceive ye how ye prevail nothing? behold, the world is gone after him.

20¶ And there were certain Greeks among them that came up to worship at the feast: 21The same came therefore to Philip, which was of Bethsaida of Galilee, and desired him, saying, Sir, we would see Jesus. 22Philip cometh and telleth Andrew: and again Andrew and Philip tell Jesus.

23¶ And Jesus answered them, saying, The hour is come, that the Son of man should be glorified. 24Verily, verily, I say unto you, Except a corn of wheat fall into the ground and die, it abideth alone: but if it die, it bringeth forth much fruit. 25He that loveth his life shall lose it; and he that hateth his life in this world shall keep it unto life eternal. 26If any man serve me, let him follow me; and where I am, there shall also my servant be: if any man serve me, him will my Father honour. 27Now is my soul troubled; and what shall I say? Father, save me from this hour: but for this cause came I unto this hour. 28Father, glorify thy name. Then came there a voice from heaven, saying, I have both glorified it, and will glorify it again. 29The people therefore, that stood by, and heard it, said that it thundered: others said, An angel spake to him. 30Jesus answered and said, This voice came not because of me, but for your sakes. 31Now is the judgment of this world: now shall the prince of this world be cast out. 32And I, if I be lifted up from the earth, will draw all men unto me. 33This he said, signifying what death he should die. 34The people answered him, We have heard out of the law that Christ abideth for ever: and how sayest thou, The Son of man must be lifted up? who is this Son of man? 35Then Jesus said unto them, Yet a little while is the light with you. Walk while ye have the light, lest darkness come upon you: for he that walketh in darkness knoweth not whither he goeth. 36While ye have light, believe in the light, that ye may be the children of light. These things spake Jesus, and departed, and did hide himself from them.

37¶ But though he had done so many miracles before them, yet they believed not on him: 38That the saying of Esaias the prophet might be fulfilled, which he spake, Lord, who hath believed our report? and to whom hath the arm of the Lord been revealed? 39Therefore they could not believe, because that Esaias said again, 40He hath blinded their eyes, and hardened their heart; that they should not see with their eyes, nor understand with their heart, and be converted, and I should heal them. 41These things said Esaias, when he saw his glory, and spake of him.

42¶ Nevertheless among the chief rulers also many believed on him; but because of the Pharisees they did not confess him, lest they should be put out of the synagogue: 43For they loved the praise of men more than the praise of God.

44¶ Jesus cried and said, He that believeth on me, believeth not on me, but on him that sent me. 45And he that seeth me seeth him that sent me. 46I am come a light into the world, that whosoever believeth on me should not abide in darkness. 47And if any man hear my words, and believe not, I judge him not: for I came not to judge the world, but to save the world. 48He that rejecteth me, and receiveth not my words, hath one that judgeth him: the word that I have spoken, the same shall judge him in the last day. 49For I have not spoken of myself; but the Father which sent me, he gave me a commandment, what I should say, and what I should speak. 50And I know that his commandment is life everlasting: whatsoever I speak therefore, even as the Father said unto me, so I speak.