Yeremia 44 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 44:1-30

Maafa Kwa Sababu Ya Ibada Za Sanamu

144:1 Kut 14:2; Yer 43:7-8; Isa 19:13; 11:11; Yer 46:14; Kum 32:42; Yer 24:8Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi,44:1 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. katika nchi ya Pathrosi44:1 Pathrosi ina maana Misri ya Juu. kusema: 244:2 Law 26:31; Kum 29:23; Mik 3:12; Yer 6:11; 40:5; 2Nya 34:24“Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu 344:3 Hes 25:3; Isa 19:1; Kum 32:17; Yer 19:4; Amu 2:19; Kut 32:22; Hes 11:33; 16:40kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu. 444:4 Yer 7:13, 25; Hes 11:29; Kum 18; 9; 1Fal 14:24; 1Pet 4:3Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’ 544:5 Yer 11:8-10; 25:4; Dan 9; 6; Mwa 6:5; 2Tim 2:19; Eze 8:18; 16:18; 23:41Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine. 644:6 Eze 8:18; 20:34; Law 26:31-34; Zek 7:14Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.

744:7 Yer 26:19; 51:22; Hes 16:36; Rum 1:23; 2Fal 21:14“Basi hili ndilo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki? 844:8 Isa 40:18-20; Rum 1:23; Yer 44:18; 1Kor 10:22; Za 44:13; Yer 41:5; Kut 12:12Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kile ambacho mikono yenu imekitengeneza, mkaifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani. 944:9 Yer 11:12; 32:32; Amu 2:19; 2Fal 23:11; Mit 31:10; Yer 6:12; 1Fal 21:25Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu? 1044:10 Mit 28:14; Gal 3:19; 2Fal 17:17; 1Fal 9:6-9; Mt 23:12; Flp 2:9; Kum 6:13; Mt 5:17-20Mpaka leo hawajajinyenyekeza au kuonyesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu.

1144:11 2Nya 34:24; Amo 9:4; Yer 21:10; Ufu 4:8“Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote. 1244:12 Yer 40:15; Isa 1:28; Zek 8:13; Yer 42:15-18; Kum 28:25; Yer 29:18Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa humo. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu. 1344:13 Yer 42:17; Kut 32:34; Law 26:14-17; Yer 15:2Nitawaadhibu wale waishio Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu. 1444:14 Mao 4:15; Rum 9:27; Yer 22:24-27; 49:5; Eze 6:8Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye amekwenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.”

1544:15 Mit 31:10; Yer 6:12; 18:15Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani, kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia, 1644:16 1Sam 8; 19; Ay 15:25-26; Mit 1:24-27; Lk 19; 14; Yer 11:8-11; 42:19“Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la Bwana! 1744:17 Kum 23:23; Yer 7:18; Hes 30:12; Ay 21:15; Isa 3:9; 65:3; Neh 9:34; Yer 2:26; Hes 11:4-6; Kut 16:3; Hos 2:5-13Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote. 1844:18 Mal 3:13-15; Law 23:18; Yer 42:16Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.”

1944:19 Yer 7:18; 18:15; Efe 5:22; Mwa 3:6; Law 7:12; Mdo 17:29Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”

20Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu, 2144:21 Isa 64:5; Hos 8:13; Yer 11:13; Za 79:8; Yer 14:10; 2:26“Je, Bwana hakukumbuka na kufikiri juu ya uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi? 2244:22 Mwa 19:13; Yer 25:18; Eze 33:28-29; Amo 2:13; Isa 1:14; Za 107:33-34Bwana alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo. 2344:23 Yer 40:2; Law 26:33; Dan 9:11-12; 1Fal 9:6; Law 18:4; Yer 7:13-15; Eze 39:23Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi ya Bwana, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.”

2444:24 Mwa 3:6; Yer 43:7Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno la Bwana, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri. 2544:25 Kum 32:28; Mit 20:25; Yak 1:13-15; Mit 31:10; Eze 20:29Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonyesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’

“Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu! 2644:26 Mwa 22:16; Mdo 19:13; Za 50:16; Kum 32:40; Yer 24:8; Ebr 6:13-17; Mwa 15:2Lakini sikieni neno la Bwana, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Bwana, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mwenyezi aishivyo.” 2744:27 Yer 21:10; 31:28; Eze 7:6; Yer 1:12; Ay 15:22; 2Pet 3:8-9; Dan 9:14; Amo 9:8Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Wayahudi walioko Misri wataangamia kwa upanga na njaa, hadi wote watakapoangamizwa. 2844:28 Isa 27:13; 10:19; Hab 3:2; Yer 45:5; Eze 6:8; Yer 39:16; 42:15-18Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.

2944:29 Mwa 24:14; Kut 3:12; Hes 16:38; Mt 12:38; Mit 19:21“ ‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asema Bwana, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’ 3044:30 Eze 29:3; Yer 25:19; Eze 32:32; Yer 24:8; 43:9-13; 2Fal 25:1-7Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama vile nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 44:1-30

耶和华给流亡埃及之人的信息

1论到那些住在埃及境内的密夺答比匿挪弗巴特罗地区的犹大人,耶和华的话传给了耶利米,说: 2以色列的上帝——万军之耶和华说,‘你们已看见了我降在耶路撒冷犹大各城的灾祸。如今它们一片荒凉,杳无人迹。 3这都是因为那里的居民犯罪作恶,向他们、你们和你们祖先都不认识的神明烧香祭拜,惹我发怒。 4我屡次差遣我的仆人——众先知警告他们不要再做令我深恶痛绝的事, 5他们却毫不理会,不肯改掉向假神烧香的恶行。 6因此,我的怒火在犹大的城邑和耶路撒冷的街上燃烧,使它们沦为废墟,正如今日一样。’ 7以色列的上帝——万军之上帝耶和华说,‘你们为什么自招大祸,使你们当中的男人、女人、孩童和婴儿都从犹大灭亡,无一幸免呢? 8你们为什么在埃及向别的神明烧香,惹我发怒,自招毁灭,成为天下万国咒诅和羞辱的对象呢? 9难道你们忘记了你们的祖先、犹大列王及其嫔妃,以及你们自己和妻子在犹大耶路撒冷街上的恶行吗? 10你们至今既不悔悟也不惧怕,不遵行我给你们和你们祖先设立的律法和诫命。

11“‘因此,看啊,我必严惩你们,毁灭整个犹大。这是以色列的上帝——万军之耶和华说的。 12我要毁灭那些执意去埃及住的犹大余民。他们必死于战争和饥荒,无论尊卑无一幸免。他们的下场将很可怕,成了被人责骂、咒诅和羞辱的对象。 13我要像惩罚耶路撒冷一样用战争、饥荒和瘟疫惩罚那些住在埃及的人。 14那些去埃及住的犹大余民没有几个能活着从埃及返回他们渴望的故乡。’”

15许多人知道自己的妻子曾向别的神明烧香。他们和他们的妻子以及住在埃及巴特罗地区的人对耶利米说: 16“我们不会听从你奉耶和华的名对我们说的话。 17但我们必照所许的愿向天后烧香奠酒,正如我们和我们的祖先、君王和官长在犹大各城和耶路撒冷街上所做的一样。那时,我们食物充足,生活幸福,无灾无祸。 18但自从我们停止向天后烧香奠酒后,我们便一无所有,不断有人死于战争和饥荒。” 19那些烧香的妇女说:“你以为我们的丈夫不知道我们向天后烧香奠酒、照着她的形象做祭饼吗?”

20于是,耶利米对在场所有答复他的男女说: 21“你们和你们的祖先、君王、官长及其他所有百姓在犹大各城和耶路撒冷的街上烧香,耶和华岂不记得,岂能遗忘? 22你们的可憎恶行令耶和华忍无可忍,以致祂使你们的土地一片荒凉,无人居住,被人咒诅,正如今天的情形。 23你们遭遇今天的灾祸是因为你们向别的神明烧香得罪耶和华,不听从祂的话,不遵行祂的律法、诫命和教诲。”

24耶利米又对在场的男女说:“你们住在埃及犹大人都要听耶和华的话。 25以色列的上帝——万军之耶和华说,‘你们和你们的妻子曾许愿向天后烧香奠酒,并且身体力行。你们继续还所许的愿吧!’ 26住在埃及犹大人啊,你们都要听耶和华的话。耶和华说,‘看啊,我以自己伟大的名起誓,再没有一个住在埃及犹大人会凭永活的主耶和华起誓。 27看啊,我一定要给你们降下灾祸而非祝福,使所有住在埃及犹大人死于战争和饥荒。 28刀下余生、从埃及返回犹大的人必寥寥无几。那时,你们这些去埃及住的犹大人必知道谁的话会实现,是我的还是你们的。 29我必在这地方惩罚你们,我要给你们一个预兆,好叫你们知道我言出必行。这是耶和华说的。 30我必把埃及王法老何弗拉交在想杀他的仇敌手中,就像我把犹大西底迦交在想杀他的仇敌巴比伦尼布甲尼撒手中一样。这是耶和华说的。’”