Yeremia 22 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 22:1-30

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

1Hili ndilo asemalo Bwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko: 222:2 Lk 1:32; Amo 7:16‘Sikia neno la Bwana, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya. 322:3 Law 25:17; Hos 12:6; Yer 21:12; Za 72:4; Isa 1:17; Amo 5:24; Eze 33:14; Mik 6:8Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa. 422:4 Yer 17:25Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao. 522:5 Yer 17:25; Mwa 22:16; Ebr 6:13Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema Bwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

622:6 Mik 3:12; Mwa 31:21; Wim 4:1; Isa 33:9; 1Fal 7:2Kwa kuwa hili ndilo Bwana asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,

kama kilele cha Lebanoni,

hakika nitakufanya uwe kama jangwa,

kama miji ambayo haijakaliwa na watu.

722:7 Yer 6:4; Isa 10:34; Za 74:5; Isa 21:14; Yer 4:7; Zek 11:1; 2Nya 36:16Nitawatuma waharabu dhidi yako,

kila mtu akiwa na silaha zake,

nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi

na kuzitupa motoni.

822:8 Kum 29:24-26; 1Fal 9:8-9; Yer 16:10-11“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 922:9 2Fal 22:17; Yer 16:11; Eze 39:23; 1Fal 9:9Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

1022:10 Mhu 4:2; Eze 24; 16; Yer 24:9; 29:18; 42:18Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;

badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu

yule aliyepelekwa uhamishoni,

kwa sababu kamwe hatairudia

wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

1122:11 2Fal 23:30-31; 1Nya 3:15Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu22:11 Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi. mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 1222:12 2Fal 23:34Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”

1322:13 Mik 3:10; Hab 2:9; Law 19:13; Yak 5:4; Isa 5:8“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,

vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,

akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,

bila kuwalipa kwa utumishi wao.

1422:14 Isa 5:8-9; 2Sam 7:2; Eze 23:14Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,

na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’

Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,

huweka kuta za mbao za mierezi,

na kuipamba kwa rangi nyekundu.

1522:15 2Fal 23:25; Za 22:21; Kum 9:7; Yer 3:13; Sef 3:2; Isa 3:10; Za 128:2“Je, inakufanya kuwa mfalme

huko kuongeza idadi ya mierezi?

Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?

Alifanya yaliyo sawa na haki,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

1622:16 Za 72:1-4, 12-13; Yn 8:19; Tit 1:16; Yak 1:22; Za 82:3; Mit 24:23Aliwatetea maskini na wahitaji,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”

asema Bwana.

1722:17 Eze 19:6; 2Fal 24:4; Isa 56:11; Eze 18:12; Mik 2:2; Kum 28:33“Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

katika mapato ya udhalimu,

kwa kumwaga damu isiyo na hatia,

kwa uonevu na ukatili.”

18Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

“Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’

Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

1922:19 2Fal 24:6; Yer 36:30Atazikwa maziko ya punda:

ataburutwa na kutupwa

nje ya malango ya Yerusalemu.”

2022:20 Hes 27:12; Isa 57:13; Za 68:15; Yer 30:14; Eze 16:33-34; Hos 8:9“Panda Lebanoni ukapige kelele,

sauti yako na isikike huko Bashani,

piga kelele toka Abarimu,

kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa.

2122:21 Yer 3:25; 3:13; Sef 3:2; Za 25:7; Zek 7:7; Kum 9:7; Isa 54:4; Yer 7:23-28Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’

Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;

hujanitii mimi.

2222:22 Yer 7:19; 10:21; Ay 27:21Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni.

Kisha utaaibika na kufedheheka

kwa sababu ya uovu wako wote.

23Wewe uishiye Lebanoni,

wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,

tazama jinsi utakavyoomboleza

maumivu makali yatakapokupata,

maumivu kama yale ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa!

2422:24 2Fal 24:6-8; Yer 37:1; Hag 2:23; Mwa 38:18“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia22:24 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 2522:25 2Fal 24:16; 2Nya 36:10; Yer 34:20Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 2622:26 1Sam 25:29; Isa 22:17; Eze 19:9-14; 1Fal 2:19; 2Fal 24:8; 2Nya 36:10Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

2822:28 Za 31:12; Hos 8:8; Yer 17:4; 48:38; 2Fal 24:6; Yer 19:10Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,

chungu kilichovunjika,

chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?

Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,

na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

2922:29 Yer 6:19Ee nchi, nchi, nchi,

sikia neno la Bwana!

3022:30 1Nya 3:16-18; Mt 1:12; Yer 10:21; 38:23; 52:10; Ay 18:19; Za 94:20Hili ndilo Bwana asemalo:

“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,

mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,

kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,

wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi

wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 22:1-30

警告犹大的王

1耶和华对我说:“你下到犹大王的宫殿,这样宣告, 2‘坐在大卫宝座上的犹大王啊,你和你的臣仆以及进出这城门的百姓都要听耶和华的话。 3耶和华说,你们为人要公义正直,要从欺压者手中解救受剥削的人。不要欺凌、虐待异乡人和孤儿寡妇,不可在这地方滥杀无辜。 4如果你们遵守我的命令,大卫的子孙必继续做王,并乘车、骑马率领臣民进出王宫。 5但如果你们不遵守我的命令,我凭自己起誓,这王宫必沦为废墟。这是耶和华说的。’”

6论到犹大王的宫殿,耶和华说:

“虽然它在我眼中美如基列

又像黎巴嫩的山峰,

但我必使它变成不毛之地,

变成杳无人烟的城邑。

7我要派人拿着兵器来摧毁它,

他们要砍下它最好的香柏木,

扔进火里。

8“各国的人经过这城时都会彼此议论说,‘为什么耶和华这样对待这座大城?’ 9有人会回答,‘因为城里的人背弃了他们的上帝耶和华的约,供奉、祭拜其他神明。’”

10你们不要为死去的王哀哭,

要为被掳走的王哀哭,

因为他必一去不返,

再也看不到自己的家园。

11论到接替父亲约西亚犹大王、后来被掳走的沙龙22:11 沙龙”也叫“约哈斯”。,耶和华说:“他必一去不返, 12客死异乡,永别故土。”

对约雅敬的审判

13耶和华说:

约西亚的儿子犹大约雅敬啊,你有祸了!

你以不公不义的手段建造宫廷殿宇,

不给工人发工钱。

14你说要为自己建造宏伟的宫殿、宽敞的房间。

你安上窗户,

镶上香柏木,

涂上红漆。

15难道你大肆使用香柏木就能显出你做王的气派吗?

你父亲也吃也喝,

但他秉公行义,

所以他凡事顺利;

16他为困苦和贫穷的人申冤,

所以他凡事顺利。

这才是真正认识我。

这是耶和华说的。

17可是,你一心贪图不义之财,

滥杀无辜,横征暴敛。”

18因此,论到犹大约西亚的儿子约雅敬,耶和华说:

“没有人会为他哀悼说,

‘唉,我的弟兄啊!

唉,我的姊妹啊!’

没有人会为他哀悼说,

‘唉,主人啊!

唉,他的尊荣!’

19你必像死驴一样被拖到耶路撒冷的城门外,暴尸荒野。”

对耶路撒冷的警告

20耶路撒冷人啊,

你们要上黎巴嫩大声哭喊,

巴珊哀号,

亚巴琳痛哭,

因为你们的盟友被消灭了。

21在你们兴盛的时候,

我曾警告过你们,

你们却不听。

你们从小就叛逆,

不听我的话。

22你们的首领都要被风卷去,

你们的盟友都要被掳走,

你们必因自己的恶行而蒙羞受辱。

23住在黎巴嫩、安居在香柏木宫殿中的人啊,

当妇人分娩般的痛苦临到你们的时候,

你们将怎样呻吟呢!”

对哥尼雅的审判

24耶和华说:“犹大约雅敬的儿子哥尼雅22:24 哥尼雅”即“耶哥尼雅”,又叫“约雅斤”。啊,我凭我的永恒起誓,即使你是我右手上盖章的戒指,我也要把你摘下来, 25交给那些想杀你的人,交给你所惧怕的人,就是巴比伦尼布甲尼撒和他的迦勒底军队。 26我要把你和你母亲赶到异乡,那里不是你们的出生之地,却是葬身之处。 27你们渴望回到故乡,却不能如愿以偿。”

28难道哥尼雅是个被人鄙视、无人理睬的破瓶子吗?

为什么他和他的子孙被赶到陌生之地?

29大地啊,大地啊,大地啊,

要听耶和华的话!

30耶和华说:

“你要把这人作为无儿无女、

一生失败的人记录下来,

因为他的后裔中无一人能成功地继承大卫的宝座,

统治犹大。”