Yeremia 19 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 19:1-15

Gudulia La Udongo Lililovunjika

119:1 Hes 11:17; Yer 18:2Hili ndilo asemalo Bwana: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani 219:2 Yos 15:8; 2Fal 23:10na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia, 319:3 Yer 17:20; 6:19; 1Sam 3:11nawe useme, ‘Sikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe. 419:4 Kum 28:20; 31:16; Law 18:21; 2Fal 21:16; Isa 65:11; Kut 20:3; Yer 1:16Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wameiteketezea sadaka miungu ambayo wao wala baba zao wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia. 519:5 2Fal 3:27; Za 106:37-38; Yer 32:35; Eze 16:36; Yer 7:31Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kama sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu. 619:6 Yos 15:8; Yer 7:32; 2Fal 23:10Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asema Bwana, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo.

719:7 Law 26:17; Kum 28:25-26; Yer 16:4; Za 79:2; 33:10-11; Yer 34:20“ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. 819:8 Kum 28:37; Yer 25:9; Mao 2:15-16; Sef 2:15; Yer 18:16; Law 26:32Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kudharauliwa. Wote wapitao karibu watashangaa na kuudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote. 919:9 Law 26:29; Mao 4:10; Isa 9:20; Kum 28:49-57; Yer 21:7Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’

1019:10 Yer 13:14; 51:63; Za 2:9“Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia, 1119:11 Yer 7:32; Za 2:9; Isa 30:14uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi. 12Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale waishio ndani yake, asema Bwana. Nitaufanya mji huu kama Tofethi. 1319:13 Yer 52:13; Eze 16:41; Ay 38:32; Mdo 7:42; Eze 20:28; Yer 7:18; 32:29; Eze 20:28Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”

1419:14 2Nya 20:5; Yer 7:2; 26:2Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali ambapo Bwana alikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu la Bwana na kuwaambia watu wote, 1519:15 Zek 7:11-14; Mdo 7:51-52; Neh 9:16; Yer 11:11; 22:21“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

耶利米书 19:1-15

瓦瓶的比喻

1耶和华对我说: 2“你去向陶匠买一个瓦瓶,带着百姓和祭司中的一些首领到哈珥西19:2 哈珥西”意思是“碎陶片”。城门旁的欣嫩子谷,在那里宣告我的话。 3你要说,‘犹大王和耶路撒冷的居民啊,你们要听耶和华的话!以色列的上帝——万军之耶和华说,看啊,我要在这里降下灾祸,听见这消息的人都必耳鸣。 4因为他们背弃了我,玷污了这地方。他们向自己、自己的祖先及犹大君王都不认识的神明烧香,使这地方流满了无辜人的血。 5他们为巴力建丘坛,烧死自己的儿子作燔祭献给巴力。我从未吩咐他们这样做,连提都没提过,连想都没想过。 6因此,看啊,时候将到,这地方不再叫陀斐特欣嫩子谷,要叫杀戮谷。这是耶和华说的。 7我要在这地方挫败犹大人和耶路撒冷居民的计谋,使他们丧身在敌人刀下,死在仇敌手中,尸体成为飞鸟和野兽的食物。 8我必摧毁这城,使它令人惊惧、嗤笑,它的满目疮痍必令路人惊惧、嗤笑。 9我必使他们在敌人的围困之下陷入绝境,吃儿女和亲友的肉。’

10耶利米啊,你要在同去的人面前打碎瓦瓶, 11然后告诉他们万军之耶和华说,‘我要把这百姓和这城打得粉碎,正如人打碎瓦瓶一样,再也不能修复。人们要在陀斐特埋死人,直到无处可埋。 12我必这样惩罚这城和其中的居民,使这城像陀斐特一样。这是耶和华说的。 13耶路撒冷的房屋和犹大君王的宫殿将被玷污,像陀斐特一样,因为他们在房顶向天上的万象烧香,向别的神明奠酒。’”

14耶利米奉耶和华之命到陀斐特说预言回来后,站在耶和华殿的院子中对百姓说: 15以色列的上帝——万军之耶和华说,‘看啊,我要把我说过的灾祸降在这城及其周围的村庄,因为他们顽固不化,不肯听我的话。’”