Warumi 13 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Warumi 13:1-14

Kutii Mamlaka

113:1 Tit 3:1; 1Pet 2:13, 14; Dan 2:21; 4:17; Yn 19:11Kila mtu na atii mamlaka inayotawala, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, nazo mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu. 213:2 Kut 16:8; Tit 3:1Kwa hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe. 313:3 1Pet 2:14; 3:13Kwa kuwa watawala hawawatishi watu wale wanaotenda mema bali wale wanaotenda mabaya. Je, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Basi tenda lile lililo jema naye atakusifu. 413:4 1The 4:6; Za 82:6; Rum 12:19Kwa maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa ajili ya mema. Lakini kama ukitenda mabaya, basi ogopa, kwa kuwa hauinui upanga bila sababu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu wa kutekeleza adhabu juu ya watenda mabaya. 513:5 Mit 24:21, 22; Mhu 8:2; 1Pet 2:19Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu iwezayo kutolewa, bali pia kwa ajili ya dhamiri.

613:6 Mt 22:17Kwa sababu hii mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu, ambao hutumia muda wao wote kutawala. 713:7 Mt 17:25; 22:17, 21; Lk 23:2Mlipeni kila mtu kile mnachodaiwa. Kama mnadaiwa kodi lipeni kodi, kama ni ushuru, lipeni ushuru, astahiliye hofu, mhofu, astahiliye heshima, mheshimu.

Kupendana Kila Mmoja Na Mwingine

813:8 Mt 5:43; Yn 13:34; Kol 3:14Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. 913:9 Kut 20:13-15; Kum 5:17; 19:21; Law 19:18; Mt 17:19Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 1013:10 Mt 22:39, 40; 1Kor 13:4; Rum 13:8, 9Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

1113:11 Yak 5:8; 1Pet 4:7; Efe 5:14; 1The 5:5, 6Nanyi fanyeni hivi, mkiutambua wakati tulio nao. Saa ya kuamka kutoka usingizini imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu umekaribia zaidi kuliko hapo kwanza tulipoamini. 1213:12 Ebr 10:25; 1Yn 2:8; Efe 5:11; 6:11, 13; 1The 5:8Usiku umeendelea sana, mapambazuko yamekaribia. Kwa hiyo tuyaweke kando matendo ya giza na tuvae silaha za nuru. 1313:13 Efe 5:18; Lk 21:34; Gal 5:20, 21; 1Pet 4:3Basi na tuenende kwa adabu kama inavyopasa wakati wa mchana, si kwa kufanya karamu za ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 1413:14 Gal 5:16Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.

King James Version

Romans 13:1-14

1Let every soul be subject unto the higher powers. For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God. 2Whosoever therefore resisteth the power, resisteth the ordinance of God: and they that resist shall receive to themselves damnation. 3For rulers are not a terror to good works, but to the evil. Wilt thou then not be afraid of the power? do that which is good, and thou shalt have praise of the same: 4For he is the minister of God to thee for good. But if thou do that which is evil, be afraid; for he beareth not the sword in vain: for he is the minister of God, a revenger to execute wrath upon him that doeth evil. 5Wherefore ye must needs be subject, not only for wrath, but also for conscience sake. 6For for this cause pay ye tribute also: for they are God’s ministers, attending continually upon this very thing. 7Render therefore to all their dues: tribute to whom tribute is due; custom to whom custom; fear to whom fear; honour to whom honour. 8Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law. 9For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself. 10Love worketh no ill to his neighbour: therefore love is the fulfilling of the law. 11And that, knowing the time, that now it is high time to awake out of sleep: for now is our salvation nearer than when we believed. 12The night is far spent, the day is at hand: let us therefore cast off the works of darkness, and let us put on the armour of light. 13Let us walk honestly, as in the day; not in rioting and drunkenness, not in chambering and wantonness, not in strife and envying. 14But put ye on the Lord Jesus Christ, and make not provision for the flesh, to fulfil the lusts thereof.