Waefeso 1 – NEN & NIRV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Waefeso 1:1-23

Salamu

11:1 1Kor 1:1; 2Kor 1:1; Kol 1:2Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu:

Kwa watakatifu walioko Efeso, walio waaminifu katika Kristo Yesu:

21:2 Rum 1:7; Kol 1:2; Gal 1:3; Tit 1:4Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

Baraka Za Kiroho Katika Kristo Yesu

31:3 2Kor 2:1, 3; Efe 3:10; 6:12Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo. 41:4 Za 15:2; Kol 1:22; Efe 4:2, 15, 16Kwa maana alituchagua katika yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele zake. Kwa upendo 51:5 Rum 8:29, 30; Lk 12:32; 1Kor 1:21alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe. 61:6 Mt 3:17; Efe 1:12, 14; Kol 1:13Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa. 71:7 Rum 3:24; Kol 1:14, 20; Efe 2:7; 3:8, 16; Mdo 20:28; Ebr 9:14; 1Pet 1:16Ndani yake tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake 81:8 Kol 1:9aliyotumiminia kwa wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. 91:9 Rum 16:25; Efe 2:7; 3:9Naye alitujulisha siri ya mapenzi yake sawasawa na uradhi wa mapenzi yake, ambayo alikusudia katika Kristo, 101:10 Mk 1:15; Kol 1:20ili yapate kutimizwa wakati mkamilifu utakapowadia, yaani, kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja, chini ya kiongozi mmoja, ndiye Kristo.

111:11 Rum 8:28Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake, 121:12 Efe 1:6, 14; 2The 2:13; Yak 1:18ili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu wake. 131:13 Efe 4:21; 4:30; Yn 1:17; 2Kor 6:7Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa muhuri, yaani, Roho Mtakatifu mliyeahidiwa, 141:14 Mdo 20:32; 1Kor 1:22; 5:5yeye ambaye ni amana yetu akituhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu kwa sifa ya utukufu wake.

Shukrani Na Maombi

151:15 Kol 1:4; Flm 5Kwa sababu hii, tangu niliposikia juu ya imani yenu katika Bwana Yesu na upendo wenu kwa watakatifu wote, 161:16 Rum 1:8; Flp 1:3, 4; Kol 1:3; 1The 1:2; 2The 1:3sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. 171:17 Rum 15:6; Kut 28:3Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 181:18 Ay 42:5; Ebr 6:4Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu 191:19 Kol 1:29; Efe 6:10na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 201:20 Mdo 2:24; Za 110:1; Mdo 7:55, 56; Kol 3:1; Ebr 1:3; 10:12aliyoitumia katika Kristo alipomfufua kutoka kwa wafu, na akamketisha mkono wake wa kuume huko mbinguni, 211:21 Flp 2:9, 10; Kol 2:10; Ebr 1:4; Rum 8:38juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia. 221:22 Mt 28:18; 1Kor 11:3; Kol 2:19Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote.

New International Reader’s Version

Ephesians 1:1-23

1I, Paul, am writing this letter. I am an apostle of Christ Jesus just as God planned.

I am sending this letter to you, God’s holy people in Ephesus. Because you belong to Christ Jesus, you are faithful.

2May God our Father and the Lord Jesus Christ give you grace and peace.

Praise God for His Spiritual Blessings in Christ

3Give praise to the God and Father of our Lord Jesus Christ. He has blessed us with every spiritual blessing. Those blessings come from the heavenly world. They belong to us because we belong to Christ. 4God chose us to belong to Christ before the world was created. He chose us to be holy and without blame in his eyes. He loved us. 5So he decided long ago to adopt us. He adopted us as his children with all the rights children have. He did it because of what Jesus Christ has done. It pleased God to do it. 6All those things bring praise to his glorious grace. God freely gave us his grace because of the One he loves. 7We have been set free because of what Christ has done. Because he bled and died our sins have been forgiven. We have been set free because God’s grace is so rich. 8He poured his grace on us. By giving us great wisdom and understanding, 9he showed us the mystery of his plan. It was in keeping with what he wanted to do. It was what he had planned through Christ. 10It will all come about when history has been completed. God will then bring together all things in heaven and on earth under Christ.

11We were also chosen to belong to him. God decided to choose us long ago in keeping with his plan. He works out everything to fit his plan and purpose. 12We were the first to put our hope in Christ. We were chosen to bring praise to his glory. 13You also became believers in Christ. That happened when you heard the message of truth. It was the good news about how you could be saved. When you believed, he stamped you with an official mark. That official mark is the Holy Spirit that he promised. 14The Spirit marks us as God’s own. We can now be sure that someday we will receive all that God has promised. That will happen after God sets all his people completely free. All these things will bring praise to his glory.

Paul Prays and Gives Thanks

15I have heard about your faith in the Lord Jesus. I have also heard about your love for all God’s people. That is why 16I have not stopped thanking God for you. I always remember you in my prayers. 17I pray to the God of our Lord Jesus Christ. God is the glorious Father. I keep asking him to give you the wisdom and understanding that come from the Holy Spirit. I want you to know God better. 18I pray that you may understand more clearly. Then you will know the hope God has chosen you to receive. You will know that what God will give his holy people is rich and glorious. 19And you will know God’s great power. It can’t be compared with anything else. His power works for us who believe. It is the same mighty strength 20God showed. He showed this when he raised Christ from the dead. God seated him at his right hand in his heavenly kingdom. 21There Christ sits far above all who rule and have authority. He also sits far above all powers and kings. He is above every name that is appealed to in this world and in the world to come. 22God placed all things under Christ’s rule. He appointed him to be ruler over everything for the church. 23The church is Christ’s body and is filled by Christ. He fills everything in every way.