Ufunuo 13 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 13:1-18

113:1 Dan 7:1-6; Ufu 16:13; 12:3; Dan 11:36; Ufu 17:3Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari.

Mnyama Kutoka Baharini

Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake, na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru. 213:2 Dan 7:6; 7:5; 7:4; Ufu 16:10Mnyama yule niliyemwona alifanana na chui, lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa. 313:3 Ufu 17:8Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama. 413:4 Kut 15:11Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”

513:5 Dan 11:36; 2The 2:4; Ufu 11:2Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kiburi na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 613:6 Ufu 12:12Akafungua kinywa chake ili kumkufuru Mungu, akilitukana Jina lake na mahali aishipo na wale wakaao mbinguni. 713:7 Dan 7:21; Ufu 11:7; 5:9Pia akaruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Akapewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa. 813:8 Ufu 3:10; 3:5; 20:12; Mt 25:34Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

913:9 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie.

1013:10 Yer 15:2; 43:11; Hes 6:12; Ufu 14:12Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka,

atachukuliwa mateka.

Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga,

atauawa kwa upanga.

Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu.

Mnyama Kutoka Dunia

1113:11 Ufu 13:1, 2Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka. 1213:12 Ufu 19:20; 20:4Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. 1313:13 Mt 24:24; 2Fal 1:10; Lk 9:54Naye akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi. 1413:14 2The 2:9, 10; Ufu 12:9Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kuzifanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 1513:15 Dan 3:3-6Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa. 1613:16 Ufu 19:5; 14:9Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, 1713:17 Ufu 14:9; 14:11; 15:2ili kwamba mtu yeyote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake.

1813:18 Ufu 17:9; 15:2; 21:17Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

启示录 13:1-18

两只怪兽

1我又看见一只怪兽从海中上来,有七头十角,每只角上都戴着一个冠冕,每个头上都写着亵渎上帝的名号。 2它看起来像豹,却有熊的脚和狮子的口。巨龙将自己的能力、王位和大权柄都交给了怪兽。 3我看见怪兽的一个头似乎受了致命伤,这伤却复原了。全世界的人都惊奇地跟从了它。 4他们拜巨龙,因为巨龙将自己的权力给了怪兽。他们又拜怪兽,说:“有谁比得上这兽呢?谁能与它对抗呢?” 5巨龙又使怪兽说狂妄、亵渎的话,并给它权柄,可以任意妄为四十二个月。 6怪兽开口亵渎上帝的名、上帝的居所和一切居住在天上的。 7它又获准去攻打圣徒,征服他们,并得到权柄制服各民族、各部落、各语言族群、各国家。 8凡住在地上的人,就是从创世以来名字没有记在被杀羔羊的生命册上的,都会崇拜怪兽。

9凡有耳朵的都应当听。

10该被掳的人必被掳,

该被刀杀的必被刀杀。

因此,圣徒需要坚忍和信心。

11我又看见另一只怪兽从地里窜出来,它的两只角像羔羊的角,说话却像龙, 12在头一只怪兽面前行使头一只怪兽的一切权柄。它命令世上的人拜曾受了致命伤但已复原的头一只怪兽, 13又行大奇迹,当众叫火从天降到地上。 14它在头一只怪兽面前获准行奇迹,欺骗了普世的人,并吩咐他们为受了刀伤却仍然活着的头一只怪兽塑像。 15它又获准给怪兽的塑像生命气息,使它不但能说话,还能使所有不敬拜那像的人遭害。 16它又强迫所有的人,不论老少、尊卑、贫富、自由人或奴隶,都在右手或额上接受印记。 17凡没有盖上怪兽印记的,就是没有怪兽的名字或代号的,都不能做买卖。 18这里藏有玄机,聪明的人可以计算那怪兽的代号,因为那是一个人的代号,是“六百六十六”。